Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,156
Kila naposikiliza au kusoma chambuzi za baadhi ya watu mashuhuri, wanasiasa, wanasheria na baadhi ya wasomi wenye maono chanya katika nchi hii mapigo ya moyo yanaongeza kasi yakiashiria woga wa kinachotabiriwa kutokea!
Ripoti ya Prof. Mruma imeamsha hisia za wengi kiasi kwamba mihemko imetawala kuliko mantiki. Nimemsikiliza Zitto Kabwe, Tundu Lisu, Benson Bana, na nimesoma baadhi ya chambuzi za wanasheria mbalimbali kuhusu mchanga wa madini na hawa wawekezaji wa kimataifa.
Kwa mujibu wa Rais na tume yake, ni kwamba tunaibiwa tena saana tu na kweli huo ndo ukweli na ndio uhalisia na wala si jambo geni na pia hata mtoto mdogo au mtu wa kawaida kabisa ukimuuliza kuhusu Tanzania kunufaika na madini atasema "tunanyonywa" tena hadi tone la mwisho.
Swala la kujiuliza, hivi ni kweli hawa wanyonyaji kina ACACCIA na wenzake ni wazembe kiasi hicho kuiba hadharani tena milango ikiwa wazi!? Hapa ndo kwenye mashaka makubwa!
Hawa kina ACCACIA mitaji yao wanadhaminiwa na kina WORLD BANK na IMF au mataasisi MAKUBWA ya wakubwa huko majuu ambayo ndo washinikizaji wakubwa wa watunga sera wetu! Hivi ni wazembe kiasi hicho cha kutopenyeza vipengere vinavyowalinda kwa lolote wanalolifanya kama MAGUFURI anavyotaka tuamini!?
Mapigo ya moyo yanaenda mbio kwa sababu naona kama tunaingia wazima wazima kwenye mtego kama yale ya meli ya samaki! Utawala wa sheria ni jambo linalohitaji umakini wa hali ya juu sana! Unapoingia mkataba na mtu (achilia mbali nchi au kampuni) masharti yamkataba lazima yaheshimiwe na unapotaka kuuvunja au kuingilia mkataba huo lazima ufanye tafakari ya kina sana kuona faida au hasara ya jambo hilo!
Watanzania tumeibiwa miaka mingi sana, kwa vile Rais ameamua kushughulika na hili la madini hapaswi kwenda moja kwa moja kwenye kukamata na kuzuia na kutuhumu moja kwa moja bali akae chini na tume zake wapitie kipengele baada ya kipingele halafu waje watwambie kwamba ni vipengere vipi vimekiukwa vinavyotupa nguvu ya kugombana nao hao mabwana WAKUBWA!
Hili litatusaidia sana kuepuka kuingia kwenye hasara ya kulipa fidia na kupoteza diplomasia ya nchi katika uwekezaji. Tusipokuwa makini, tutaingia hasara kubwa kuliko faida tunayoitarajia!
Rais afahamu kuwa si kila pongezi za wabungi na mawaziri hasa wa chama tawala zinatoka moyoni! Wengine wanapongeza tu ili waonekana wako upande wako!