Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,344
- 9,845
Kampeni ya Magufuli imekuwa ya kukatisha tamaa kwakweli, nilitegemea ingetoa angalau upinzani wa karibu kwa Lowassa lakini matamaanio hayo yanafifia kila kukicha.
Kwa mtazamo wangu, mambo yanayodhoofisha kampeni ya Magufuli ni:
1.Kukosekana kwa mtazamo chanya kwenye jukwaa: Magufuli hawapi watu moyo,anaogopesha kila mtu. kampeni imekuwa ya kulalamika sehemu kubwa na Magufuli amekosa Kuonyesha ujasiri wa kuwa rais baada ya tarehe 25 October.Ukiangalia jukwaa la Magufuli utaona watu waliokata tamaa tu.
2. Kukosekana kwa ubunifu: Ukiona mgombea anaongea kisukuma, anapiga pushap jukwaani,anaapa bila sababu unaona picha ya ndege anayehangaika ndani ya chumba chenye dirisha ila haoni pakutokea. Mbaya zaidi hana uzoefu wa kampeni level ya urais na hii inafanya akose cha kuiambia timu yake ya kampeni inapomfuata kwaajili ya maelekezo.Kuiga nembo ya M4C, wimbo wa mchaka mchaka na kaulimbiu ya mabadiliko ni alama tu za kukosa ubunifu.
3. Kukosekana kwa uaminifu: Magufuli mwenyewe anasema kuna watu wakonae mchana ila usiku wako UKAWA.Hii kauli inaonyesha kuwa team ya Magufuli ya kampeni hawaaminiani.Siri zote wanazopangilia zinachukuwa dk.5 tu kuwa kwenye mitandao ya kijamii.Hii inavunja moyo mno wale wenye nia ya dhati na Magufuli.
4. Tabia ya Magufuli kupenda kusifiwa peke yake.Unaposema Tanzania ya Magufuli una maanisha nini? Unapoita wenzako kwenye chama kunguni tukueleweje? Magufuli anataka aonekane yeye tu katika chama na hata kwenye mabango yake mengine hamna utambulisho wa chama.
Ujumbe kwa team campaign ya Magufuli: You could still make this loss less embarrassing, you could make it respectable.Don't panic, reorganize and address these very obvious issues.