Kinachojengwa Mbezi mwisho ni kuchezea kodi za Watanzania

Weka ushauri basi unataka iweje. Siyo unakosoa tu kwa kuwa vimeletwa hapo.
 
Hiyo ni ghubu. Yaani unakosoa kitu ambacho hukuwa nacho na kimeletwa kwa lengo zuri ila badala ya kushauri unabeza tu
 
Kwanza naomba kusema wazi naunga mkono wazo la upanuzi wa barabara ya Kimara Kibaha.

Pili nailaumu sana tena sana Tanroad na wizara ya ujenzi kwa kuchezea kodi za wananchi kwani kila baada ya miaka 10 miundombinu hufumuliwa na kujengwa upya.


Kinacho jengwa pale mbezi mwisho hakita ishi zaidi ya miaka 10 kila kitu kitabomolewa na kujengwa upya.

Mbezi mwisho ni makutano ya pande mbili za dar es salaam

Mbezi mwisho ni mji unao kua kwa kasi kuliko.mji wowote hapa dar.

Mwezi mwisho ni lango la kuingia na kutoka dar.

Kwanini tanroad hamtaki kufikiria design nzuri walau kwa miaka 50.

Hamjifunzi mkoloni alivyo weka mita 240 upana wa barabara toka kimara hadi kibaha.

Hivyo viraundi abauti mnavyo vijemga hapo mbezi ni kupoteza kodi za wananchi.

TANROAD INAHITAJI NEW BRAIN


Uzi huu tutakuja kuukumbuka siku wakianza kubomoa wanacho kijenga

Kama lilivyo jina lako Tabu tupu na akili yako ni hivyohivyo tu.unawaza kwa kukariri...elimu mliyonayo ni kukopy na kupest...hakuna ubunifu unaotoka vichwani mwenu...zaidi ya Kulaumu...toa suluhisho
 
Na ile barabara ya mwendokasi ni ya kujivunia au nayo ni mfano mojawapo wa fikra zetu ndogo?

Wala tusijifariji. Tumetembelea miji mingi Duniani na ya mataifa mengi, tena mengine ya Afrika, ukilinganisha na tunachofanya kwenye maeneo mengi upande wa barabara na mipango miji kwa ujumla, ni uthibitisho wa upeo wetu kuwa duni kabisa.

Ni aheri kutokuwa na wasomi kabisa kuliko kuwa na wasomi wasioweza kupanga tu miji na barabara.
Mkuu barabara ya mwendo kasi tumecopy na kupaste toka Joberg-Usitupe ujiko wa bure kwamba tulidesign sisi-ile ni sawa na BIG RESULT NOW-Copy and Paste
 
tatizo lipo wapi kwa mfano
Mfano watu kujazana kituoni na kwenye mabasi yasiyo na mzunguko wa hewa na kufanya watu wawe kwenye hatari ya kuambukizana magonjwa. Kwani design yenu ilikuwa watu wajazane hivo? MBONA TUNAWAONA MNAKAA KIMYA UENDESHAJI WA HIKI KIWANDA CHA MWENDO KASI? NI SAWA KINAVYOFANYA KAZI? MNACHUKUA HATUA GANI? NDIO MAANA HAKUNA HATA VIBAO VYA KUONYESHA BASI LINAFIKA WAKATI GANI KWENYE VITUO AU KUONDOKA, MMEIGA TU BASI
 
Siamini kama Tanzania ina town planners. Maana ujinga wanaoufanya kwenye miji mingi, ni afadhali hata umpate kijana aliyeishia darasa la 7 lakini mwenye akili nzuri, atafanya planning nzuri kuliko hawa wanaojiita town planners. Wanachofanya ni ujinga mtupu, na nadhani uwezo wao wa kufikiri na mipango yao haizidi miaka 5.

Leo hii ukilinganisha miji waliyoplan wakoloni ni mizuri kuliko hao wanaoitwa wazalendo. Upanga, maeneo ya ikulu na Oysterbay Dar, yalipangwa na wakoloni. Tanga mjini ilipangwa na mkoloni, Tabora ilipangwa na wakoloni. Kwenye hiyo.miji yote, walikoendeleza wazalendo ni uchafu mtupu.

Tanroad nako ni hopeless kabisa. Hata mimi naweza kupanga vizuri zaidi kuliko hao wataalam wa Tanroads.

Ukija huko CDA Dodoma nako ni takataka. Barabara nyembamba, hakuna akiba ya maeneo ya barabara wala maeneo ya wazi ya kupumzikia.

Tuna watu wa ajabu kwenye ngazi mbalimbali za serikali mpaka taasisi zake.
Kila Mara huwa nasema ukitaka kujua umaskini na ufinyu wa jamii ambayo haijastaarabika just angalia tu mpangilio wa makazi na miundombinu yetu mambo yanaenda shaghala baghala tu
Huko kwa wenzetu mfano Kenya au Ghana etc miji yao iko kwenye plan vizuri sana,Sasa tzn kila mji na everywhere ni squatters,hao viongozi hawaoni aibu? Na ujue Tzn huwa tunafanya mambo kwa kulipua au Bora liende na bila vision,ni shida sana nchi hii
 
Tanzania ndio nchi pekee duniani inayotengeneza barabara zile zile kwa miaka yote , ukifuatilia utagundua miaka michache iliyopita barabara ya Kimara - Mbezi ilijengwa , lakini leo inajengwa tena
Halafu barabara alizijenga mwenyewe mtetea wanyonge.
 
Na ile barabara ya mwendokasi ni ya kujivunia au nayo ni mfano mojawapo wa fikra zetu ndogo?

Wala tusijifariji. Tumetembelea miji mingi Duniani na ya mataifa mengi, tena mengine ya Afrika, ukilinganisha na tunachofanya kwenye maeneo mengi upande wa barabara na mipango miji kwa ujumla, ni uthibitisho wa upeo wetu kuwa duni kabisa.

Ni aheri kutokuwa na wasomi kabisa kuliko kuwa na wasomi wasioweza kupanga tu miji na barabara.
Jaribu ku Google nchi Kama Ghana tumeizidi uchumi lakini miundombinu wanayojenga ni ya adabu,cheki hapo Kampala entebe road ya maana huku dar takataka tuu
 

Attachments

  • Kasoa Interchange and Ancillary Works (Ghana) ( 360 X 640 ).mp4
    17 MB · Views: 30
  • Sofoline Interchange in Kumasi Ghana ( 480 X 854 ).mp4
    11.2 MB · Views: 25
Tanzania ndio nchi pekee duniani inayotengeneza barabara zile zile kwa miaka yote , ukifuatilia utagundua miaka michache iliyopita barabara ya Kimara - Mbezi ilijengwa , lakini leo inajengwa tena
Nakumbuka miaka ya 2001/2002 ilipasuliwa ile ya njia moja sijui mbili kuanzia ubungo hadi kimara na zikajenjwa barabara 4 haijatimia hata miaka 20 ikapasuliwa tena ikawekwa mwendokasi na hii mwendo kasi itapasuliwa muda si mrefu wataweka sijui nini kitu hata miaka 30 hakija fikisha kishapasuliwa

Inaonekana ni miradi ya watu kupiga 10%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ndio nchi pekee duniani inayotengeneza barabara zile zile kwa miaka yote , ukifuatilia utagundua miaka michache iliyopita barabara ya Kimara - Mbezi ilijengwa , lakini leo inajengwa tena
Hii mara ya Tatu,aliijenga mkapa,akaijenge JK na sasa magufuli-Hii nchi na ccm yake ilipaswa iwe sayari ya pekee yake
 
kilicho ondoa foleni pale sio mzunguko bali ni watukutumia njia mbadala!
unakumbuka mzunguko wa pale kariakoo? vipi kuhusu mzunguko wa kigogo na m.city mbona bado kuna foleni??
mzunguko haujawahi kua dawa ya foleni zaidi watanufaikia mafundi garage maana watu ni full kupasuana

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa wa wapi? Una uhakika kwamba roundabouts hazipunguzi foleni??
 
Tazama pale ubungo, baada ya kuweka mzunguko wa mabati. Hakuna foleni.
Kumbe foleni ilikuwa inaletwa na yale mataa mabovu mabovu. Sijui kwanini hawakuweka mzunguko tangia miaka yote

Sent using Jamii Forums mobile app
sababu ya kupungua foleni pae junction soyo yale mabati bali ni baada ya kustopisha route ya dala daala ya kimara kariakoo na gari zake zilikuwa nyingi sana.
 
Back
Top Bottom