Kinachojengwa Mbezi mwisho ni kuchezea kodi za Watanzania

Hao wanaojiita sijui tumesoma ndo mbumbumbu hawana hata exposure,,sio kila kitu kipo kwenye madesa,toka kwenye madesa ji update na ulimwengu wa kisasa
Watu wametoka kolomije huko na njaa kibao Basi wakabebwa hapo tanroads ndo hao wanafanya utumbo tu bila kujielewa,badala ya kujibu hoja wanakimbilia kusema eti anayekosoa aeleze alivyochangia kwenye fani yake,huu si undezi sasa
 
Ile rentention wall ya lile daraja pale Mbezi mwisho nafikiri inahitaji kuangaliwa. Kama barabara itamaliziwa hivyo ilivyo kwa sasa na kwa mvua kidogo iliyonyeesha imeshusha udongo kiasi kile toka kwenye hilo barabara; basi uimara na uhai wake hautakuwa mzuri sana.

Pili ni aina au tuseme ubora wa lami inayotumika, ukiangalia hiyo round about na barabara ya pembeni kuelekea kwa wafanya biashara ndogo ndogo hapo Mbezi, lami iliyowekwa inaacha maswali mengi sana ikiwemo pia suala la ubora na uimara wake. Ubora wake unashabihiana na ile lami iliyowekwa kwenye daraja pale Mbezi ambayo tayari kwa muda mfupi wa magari kupita imeshaanza kupukutika.

Lengo la haya si kubeza bali ni waweze kurekebisha kabla ya hali kuwa ndiyo sivyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uhakika kuwa kazi imeisha,? Layer zote zimeshawekwa hapo darajan unapopasema? Una taarifa sahihi toka chanzo sahihi?
 
Tazama pale ubungo, baada ya kuweka mzunguko wa mabati. Hakuna foleni.
Kumbe foleni ilikuwa inaletwa na yale mataa mabovu mabovu. Sijui kwanini hawakuweka mzunguko tangia miaka yote

Sent using Jamii Forums mobile app


Na siku ukikuta kuna foleni lazima kuna askari mjinga mjinga kasimama hapo na kuruhusu upande mmoja tuu shame on us aisee khaaa akili mfubao haswa
 
Mkuu inapo kutana morogoro road na njianya goba wanaweka mataa.. ndio maana round about ya chini inakaribia kuisha.

Sijawahi ona taasisi isiyo jua majukumu yake kama tanroad
Una uhakika kuwa kazi imeisha,? Layer zote zimeshawekwa hapo darajan unapopasema? Una taarifa sahihi toka chanzo sahihi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uchochezi....Watumiaji wa Morogoro road na Sam Nujoma road wanajua round about ya Ubungo ndiyo imepunguza foleni. Hizo njia mbadala (mbezi-tangi bovu, kimara-udsm, mbezi-segerea etc) mbona zipo tangu mwaka juzi na foleni ilikuwa vilevile hadi round about ilipowekwa. Wakati round about haipo foleni ilikuwa inasababishwa na Trafic police pamoja na taa ambazo hazifanyiwa synchrozation inayoendana na trafic load.....elimu....elimu....elimu....
kilicho ondoa foleni pale sio mzunguko bali ni watukutumia njia mbadala!
unakumbuka mzunguko wa pale kariakoo? vipi kuhusu mzunguko wa kigogo na m.city mbona bado kuna foleni??
mzunguko haujawahi kua dawa ya foleni zaidi watanufaikia mafundi garage maana watu ni full kupasuana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hayo yanayojengwa sasa hivi yajengwe kwa kuangalia hali itakuwaje 30 years after being constructed..population itakuwa imeongezeka plus yaweze kustahimili hali zote,sio kikija kimbunga keneth daraja chali...LOL
 
hayo yanayojengwa sasa hivi yajengwe kwa kuangalia hali itakuwaje 30 years after being constructed..population itakuwa imeongezeka plus yaweze kustahimili hali zote,sio kikija kimbunga keneth daraja chali...LOL
Unafaa kuwa mshauri wa Tanroad maana wenyewe wanaona max 3 years.
 
TANROADS ni headache aisee.
Nakumbuka wanavojenga station ya mizani ya vigwaza vile vinjia vya kutoka na kuingia mizani waliweka vidogo sana vya kutosha gari moja.
Nikajiuliza ina maana tanroads na contractor hakuna aliefikiria kwamba vile vinjia ni vidogo havifai incase gari likazima linasababisha upotevu wa muda mwingi bila sababu.
 
Kwa kweli hata mimi naunga mkono hoja kwa mbezi mwisho ni kichekesho kujenga mzunguko.Kulitakiwa kuwa na interchange fulani hv ili kutobughuzi gari zinazotoka town kwenda kibaha.Sijui lakini kwa design ile sijui kama foleni itapungua ngoja tuone mwisho wake.
 
Tazama pale ubungo, baada ya kuweka mzunguko wa mabati. Hakuna foleni.
Kumbe foleni ilikuwa inaletwa na yale mataa mabovu mabovu. Sijui kwanini hawakuweka mzunguko tangia miaka yote

Sent using Jamii Forums mobile app
ha ha ha

Waafrika tukiambiwa bado tunahitaji kutawaliwa kunang'aka.

Ushahidi ndiyo huu; hata haya masuala madogo madogo ya ku address wenyewe tunakwama.
 
Nadhani mwisho itafutwa na tarura watachukua kazi.. wanajengaga tuvitu fulani hivi huwezi kutupata sehemu yeyote.


Vigwaza walifeli sana.
TANROADS ni headache aisee.
Nakumbuka wanavojenga station ya mizani ya vigwaza vile vinjia vya kutoka na kuingia mizani waliweka vidogo sana vya kutosha gari moja.
Nikajiuliza ina maana tanroads na contractor hakuna aliefikiria kwamba vile vinjia ni vidogo havifai incase gari likazima linasababisha upotevu wa muda mwingi bila sababu.
 
Kwanza naomba kusema wazi naunga mkono wazo la upanuzi wa barabara ya Kimara Kibaha.

Pili nailaumu sana tena sana Tanroad na wizara ya ujenzi kwa kuchezea kodi za wananchi kwani kila baada ya miaka 10 miundombinu hufumuliwa na kujengwa upya.


Kinachojengwa pale Mbezi Mwisho hakitaishi zaidi ya miaka 10 kila kitu kitabomolewa na kujengwa upya.

Mbezi Mwisho ni makutano ya pande mbili za Dar es Salaam

Mbezi mwisho ni mji unaokua kwa kasi kuliko mji wowote hapa Dar.

Mbezi mwisho ni lango la kuingia na kutoka Dar.

Kwanini Tanroad hamtaki kufikiria design nzuri walau kwa miaka 50.

Hamjifunzi mkoloni alivyoweka mita 240 upana wa barabara toka Kimara hadi Kibaha.

Hivyo viraundi abauti mnavyovijemga hapo Mbezi ni kupoteza kodi za wananchi.

TANROAD INAHITAJI NEW BRAIN

Uzi huu tutakuja kuukumbuka siku wakianza kubomoa wanachokijenga
Uzi wote ila haujasema tatizo ni nini...
1. Barabara ya kiwango cha chini....
2. Nyembamba...
3. Mataa...
4. Etc
Ila umekuja tu na UTAALAM wako na kulalamika.
 
Tatizo hujaelewa .. wenzio wengi wameelewa.. any way hata darasani ninkawaiada wenhine kuto elewa.
Uzi wote ila haujasema tatizo ni nini...
1. Barabara ya kiwango cha chini....
2. Nyembamba...
3. Etc
Ila umekuja tu na UTAALAM wako na kulalamika.
 
Mkuu una utaalam wowote katika civil engineering?
Unajua sheria ya barabara?
Hata mwendokasi wakati inajengwa,kulikua na wataalam elekezi feki kama wewe wengi tu
Hawa ndio walikuwa wako bize mitandaoni wakisema vituo vya mwendokasi vimekosewa kujengwa sababu milango ya mabasi itakuwa upande ambao sio sahihi. Walijua kwa akili zao kuwa milango ya mwendo kasi iko kama ya daladala na watashusha kama daladala. Na walikomaa kweli humu na kupeana likes...
 
Back
Top Bottom