Kinachoendelea Zimbabwe: Nchi yawekwa chini ya Jeshi, Mugabe kung'olewa?!

Babu sasa hivi ana hasira za mazee wake kunyaswanyaswa na wanajeshi, akipewa nafasi tena japo ya masaa 2 tu kushika hatamu za uongozi kazi ya kwanza katika dakika 30 za kwanza nadhani itakuwa kumkamata mkuu wa majeshi akiwa hai au mfu.
Mkuu wa majeshi hakamatiki jua na yeye tayari amejipanga. Na ikiwa hivyo nchi ndo itapinduliwa kiukweli.
 
Hilo sio wazo la wazimbabwe kwa sasa.

Mugabe anapaswa kuondoka mwenyewe kwa hiyari na hatifanywa lolote.

Ni mtu tajiri sana utajiri alojitengenezea kwa miaka 37.
Alitakiwa awe ameondoka miaka 10 iliyopita.
Kwa sasa afikishwe tu hapo ICC ili iwe mfano kwa viongozi madikteta wengine barani Afrika.
 
Tupia kapicha mkuu
Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe, akiwemo mke wa jenerali aliyemzuia siku ya Jumatano. BBC
_98794237_b3a06108-fefe-4a75-be18-f99e8c3a6047.jpg
 
Kweli kabisa mkuu, nimestaajabu baada ya kumuona Mugabe uraiani kwenye mahafali!!! Sidhani kama Jeshi linaweza kufanya mistake hiyo ya kumrudisha madarakani babu.
Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe, akiwemo mke wa jenerali aliyemzuia siku ya Jumatano.

Marry Chiwenga alipata shahada ya MBA kulingana na shirika la habari la Zimbabwe.

Awali Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.

Alihudhuria sherehe za kuhitimu kwa mahafala kwenye mji mkuu Harare.

Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.

Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo.

Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.

Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais. BBC
 
Deal Done, Makubaliano yameshafikiwa, Majibu wanasubiri Mkutano wa ZAN PF December. Au Mwenyewe ajitangaze kwamba umri umeenda.
 
Exactly! Inategemewa CDF akionekana mbele ya camera ni jambo zito la kitaifa na sio habari za kutishia sijui wanaotaka kuandamana kudai haki mikutano ya kisiasa au kumpinga mweneyekiti wa mtaa. Issues za kutoa progress ya mapigano mbele ya vyombo kama Bunge nchi inapokuwa vitani; issues kama mabadiliko yasiyo ya kawaida ya kiutawala; yaani issues nzito mno za kitaifa ndio majukumu yake hayo kutoa progress tena very briefly zaidi ni action. Lakini unapoona CDF anapiga soga mbele ya waandishi wa habari; kuwashauri wasioridhika waende mahakamani; kuwaonya wahalifu sijui wa Kibiti na wapi huko dah! hizo ni press za Advera Senso or junior officers.
Unanikumbusha kipindi cha Dk 45 Mkuu
 
Heshima wanayoendelea kumpa Mugabe itamtia kibri na inaweza kuwacost jeshi. Mtu yupo supposedly kwa house arrest lakini anakwenda kuhudhuria graduation ceremony? I hope wana plan B jinsi ya kumdhibiti Mugabe na mkewe kama watakaidi
Huyu Jenerali hayupo kawaida, yaani wamejipnga vizuri kindani na kiintelejensia na ndio maana hawakuwa na papara kwenye actions, ndio maana tunasema information is power, na idara zake zinafanya kazi vizuri bila unafiki kwa Mkuu Wao, na hiyo ni kwa sababu wanajitambua, hawaendi kama manyumbu
 
Back
Top Bottom