Kinachoendelea Zimbabwe: Nchi yawekwa chini ya Jeshi, Mugabe kung'olewa?!

Mkuu, Grace Mygabe bado yupo chini ya ulinzi kwenye Ikulu ya Zimbabwe. Pale ikulu yao pamegawanyika hivyo yeye Grace Mugabe na wanafamilia wengine wapo chini ya ulinzi sehemu ingine. Hizo taarifa za kukimbilia Namibia nadhani bado hazijathibitishwa. Kumbuka wanajeshi walipozingira Ikulu Grace alikuwemo ndani na mzee Mugabe.
Ila mama zetu achana nawo kabisa, Comrade alihonga kila kitu maishani mwake, utashi wake, itikadi zake, marafiki, bado haikutosha, ikabidi atake kuhongo NCHI! Wanaume wenzake wakaona sasa Comrade unasikilizia sana utamu sana, hatuendi hivyo babu, ebu kaa pembeni kidogo!
 
Kuna uzi ntaushusha hivi karibuni nikidadisi kama kweli huyu mama hakuwa jasusi hatari kabisa kuwahi kutokea Afrika.

Alikuwa na kazi maalum au "special mission" ambayo endapo Mugabe ataondoka basi mission itakuwa accomplished.

Grace Mugabe alizaliwa Afrika Kusini na akahamia Zimbabwe akiwa na miaka 14.
 
ZANU-PF kimeitisha maandamano ya kumtaka Comrade Robert G. Mugabe, Supreme Leader and founder wa chama kujiuzulu! Haya mavyama kongwe na yaliyochoka huku Afrika ni tabu sana; huwa yanawaona wananchi kama mazezeta vile. Waache usanii pumbavu zao!
 
Huyu Jenerali hayupo kawaida, yaani wamejipnga vizuri kindani na kiintelejensia na ndio maana hawakuwa na papara kwenye actions, ndio maana tunasema information is power, na idara zake zinafanya kazi vizuri bila unafiki kwa Mkuu Wao, na hiyo ni kwa sababu wanajitambua, hawaendi kama manyumbu
Nilipenda ripoti kuwa special forces walienda airport na kuvaa kama watumishi wa "Swissport" ili kuzuia jaribio la kumkamata Jenerali Chiwenga akitokea China. Alipotua tu wakavua magwanda ya "Swissport" ya huko na kumlinda jemedari. Askari Polisi wakashindwa kumkamata.
 
Hapo inatuonyesha wazi ni namna gani jeshi la Zimbabwe limekomaa ktk mipango yake... Ninaamini, kama akikataa kujiuzuru basi jeshi litakishawishi tena chama kumnyang'anya kadi na huo ndio utakuwa mwisho wa mwisho wa Mugabe. Jiondokee tu mzee ukalee vitukuu Jeshi, Chama, Wananchi wameshakuchoka, utapata uungwaji mkono toka wapi?
Hivi kwanini mnalisifu sana hili jeshi??hamjui ama hamuelewi ni hili jeshi ndilo limemuweka madarakani mugabe muda wotee huo???na ndilo linalokwamisha upinzani katika nchi hiyo??

Hivi hamtambui kuwa hili jeshi ndilo linamuweka rais wao wanaomtaka Emerson baada ya Mugabe,na sio maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura?

Zimbabwe inatoa dikteta anawekwa dikteta, anatoka Simba anaingia The Crocodile....
 
Kuna uzi ntaushusha hivi karibuni nikidadisi kama kweli huyu mama hakuwa jasusi hatari kabisa kuwahi kutokea Afrika.

Alikuwa na kazi maalum au "special mission" ambayo endapo Mugabe ataondoka basi mission itakuwa accomplished.

Grace Mugabe alizaliwa Afrika Kusini na akahamia Zimbabwe akiwa na miaka 14.
Asante kwa taarifa mkuu, usisahau kuni tag ukipandisha huo uzi wa Bi Grace Mugabe.
 
Back
Top Bottom