Kinachoendelea Tunduma: Chama cha Mapinduzi, Tume ya Uchaguzi na Vyombo vya Dola Vinainajisi Demokrasia Nchini

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kinachoendelea Tunduma: Chama cha Mapinduzi, Tume ya Uchaguzi na Vyombo vya Dola Vinainajisi Demokrasia Nchini.

Kwa mwenendo wa mambo unavyokwenda, ni dhahiri kwamba Chama cha Mapinduzi kimejipanga kuuvuruga uchaguzi wa marudio kwenye jimbo la Buyungu na kata mbalimbali nchini.

Huko nyuma, kilio kikubwa katika mchakato wa uchaguzi nchini kilikuwa hasa kwenye hatua za kampeni, upigaji kura na utangazaji wa matokeo. Awamu hii, CCM imejipanga kwa kutumia vitisho, mabavu na hila za wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kwamba wapinzani hawapewi fomu, wakipewa hawazirejeshi na wakizirejesha zinatiwa dosari wasiteuliwe.

Mkakati huu umeiwezesha CCM kupita bila kupingwa kwenye kata kadhaa kinyume na taratibu.

Mfano mzuri unapatikana Tunduma. Pazia la kuchukua fomu lilipofunguliwa, jeshi la polisi lilitumika kuwakamata na kuwatisha wagombea wa vyama vya upinzani ili kuhakikisha kwamba CCM wanabaki peke yao. Wale ambao hawakukamatwa wamefanyiwa hila za kila namna kuenguliwa. Mathalani, baada ya kujificha kwa muda mrefu, wagombea watatu wa chama chetu kwenye kata za Kaloleni, Mpemba na Mwakakati walifanikiwa kurejesha fomu siku ya tarehe 14 Julai. Ajabu ya mambo, Msimamizi wa uchaguzi ameiandikia Idara ya Uhamiaji kuwaomba uthibitisho wa uraia wa wagombea wote wa upinzani wapatao nane. Idara ya Uamiaji ikajibu kuwa wagombea wote wa vyama vya upinzani (Rejea barua iliyoambatanishwa) kuwa si raia wa Tanzania. Swali la kujiuliza, ni wapinzani pekee ambao wanastahili tuhuma za kutokuwa raia na kufanyiwa njama za kupokonywa uraia?

Maajabu zaidi, wagombea hao wanapopeleka ushahidi wa uraia wao wakiambatanisha vielelezo vya uraia wao, msimamizi wa uchaguzi anagoma kuvipokea. Njama zote hizi zimefanywa ili kuhalalisha CCM wanapita bila kupingwa kwenye kata nyingi nchini. Kwa nini uchaguzi unaitishwa kama CCM hawapo tayari kushindana?

Swali la kujiuliza, CCM imefilisika kiasi kwamba haiwezi kuwakabili wapinzani kwenye majukwaa ya kisiasa na uchaguzi wa huru na haki? Kama chama cha siasa kinajivunia nini kushinda kwa mbeleko ya dola? Kuna raha gani kula vya kunyonga?

Hitimisho

1. Chama chetu kitasimama kidete kwa njia za kisheria kuhakikisha kwamba wagombea wetu waliopokwa uraia wao na CCM kwa uchu wa madaraka wanapata haki yao.

2. Chama chetu kitashirikiana na vyama vingine vya upinzani kuhakikisha kwamba wapinzani tunatuma ujumbe madhubuti kabisa kwa CCM kuwa tumechoka na ubakaji wao wa demokrasia.

3. Tunatoa wito kwa waangalizi wa ndani kufuatilia kwa karibu vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa misingi ya kidemokrasia ulioshamiri kwenye uchaguzi huu wa marudio hata kabla ya kampeni kuanza.

Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi
ACT Wazalendo
16 Julai 2018
 
Pole sana mkuu sisi wana cdm tulisha piga kelele siku nyingi lkn wenzetu walituona ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa sasa tuungane tujikomboe na ushetani wa ccm
 
ni wapinzani pekee ambao wanastahili tuhuma za kutokuwa raia na kufanyiwa njama za kupokonywa uraia?
Kama kuna mgombea wa ccm uraia una utata,si muweke pingamizi?Kulia mitandaoni hakusaidii kitu mnatakiwa muwe makini wakati mnateua watu
Hili ni gonjwa sugu kwa upinzani wa Tanzania,kuteua wagombea aidha wasio raia au sio wakazi wa eneo stahiki kunakosababisha mgombea kukosa hata kujipigia kura,mfano Salum Mwalimu,alitaka achaguliwe kinondoni,wakati si mkazi wa kinondoni,matokeo yake alishindwa hata kujipigia kura.
 
Mbona nyinyi viongozi wenu siyo raia?mbona unajitia upofu?
 
Mbona nyinyi viongozi wenu siyo raia?mbona unajitia upofu?
Acha kulia lia ili uonewe tu huruma kwenye mambo ya msingi,lete facts hapa.Sheria ipo wazi kabisa kuhusu asikua raia haruhusiwi kuchagua wala kuchaguliwa.Mnatuletea wazambia halafu mnataka wawe madiwani?hamna adabu kabisa nyie watu
 
Nipo Tunduma, kwa kweli siasa zinazoendelea hapa zinahitaji moyo wa ujasiri kuzivumilia....

Imefikia kipindi hata wanaccm wenyewe wanashangazwa na hizi siasa....

Haki inaporwa mchana kweupe tena kwa unyanyasaji mkubwa na wa hali ya juu.

Siku haya madukuduku yakija kupasua vifua vya watu tutapoteana.....

Busara ni heri serikali ipeleke mswada bungeni kufuta vyama vya upinzani nchini kuliko hiki kinachoendelea.
 
Hawana ubavu huo wa kupitisha huo mswaada maana hata walivyokubali kujiunga na huu mfumo ilikuwa ni kutii shinikizo la wakubwa wa dunia
 
umeona ile shughuli waliokuwa wanaifny ccm na ndugu zao pale kibaha hii leo? ule ndo ukoloni mamboleo wa china, nchi zote zilizokuwepo pale leo ni km zna mfumo wa chama kimoja vile vyama vingi ni zuga tu
 
Back
Top Bottom