Muda mfupi nimezungumza kwa njia ya simu na mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi jimbo la Segerea ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa kata moja wapo katika jimbo hilo.
Iko hivi:
- Majumuisho ya kura zote kutoka vituoni yanaonesha Mh. Mpendazoe anaongoza.
- Kila wakala wa chama, baada ya majumuisho anapewa nakala ya idadi ya kura kwa kila kituo. hili ni agizo la waangalizi wa kimataifa(wadhungu) ambako Bwana Mkubwa JK huenda kufanya umatonya.
Maana yake nini?
Matokeo yaliyojumuishwa na mawakala na wasimamizi hayawezi kuchezewa. Hata yakichezewa, nakala za matokeo ni vithibitisho tosha (hata mahakamani) kinachoweza kuwa matokeo yamechakachuliwa.
Kwa hiyo wana-jamvi. Tulieni. Sauti ya umma imesikika Segerea.