Kinacho fanywa na mawakala wa TRA

Kinacho fanywa na mawakala wa TRA

Wamenisimamisha kwenye taa sa Sarender Bridge, wakasema wanataka wakague Mafuta. Akaangalia gauge kwenye dashboard akakuta kuna nusu tank, akauliza risiti. Nikamuuliza risiti ya nini? Eti ya nilijiwekea mafuta. Uzuri nilikuwa nayo, akaisoma kisha akaondoka.
Swali:-
Je huu ni utaratibu rasmi wa TRA au ndio utapeli na upigaji mpya jijini?

Kuliko kupoteza muda wao kihivyo hii kazi wangeikabidhi kwa wale wazee wa tochi ukikutwa hauna risiti faini na ukikutwa taa ya mafuta inawaka faini
 
Sidhani kama mkuu unachosema kina ukweli wowote. Mimi napita hapo si chini ya mara 16 kwa siku na ni kila siku. Sijawahi ona kitu kama hicho.
Ni kweli. Hata boss wangu alikamatwa hapo hapo akaja kutusisitiza tukiweka mafuta tusisahau risiti
 
Duh nikijaza full tang itanibidi nitembe na risit mwezi mzima..????
 
Sidhani kama mkuu unachosema kina ukweli wowote. Mimi napita hapo si chini ya mara 16 kwa siku na ni kila siku. Sijawahi ona kitu kama hicho.
Yawezekana, ila kama ni kweli basi @TRA wako very desperate, yaonyesha bado hawajajuwa hasa kodi wazipate kivipi, inanisoikitisha sana na kuona kweli vyeti feki bado vinasumbua...
 
Yawezekana, ila kama ni kweli basi @TRA wako very desperate, yaonyesha bado hawajajuwa hasa kodi wazipate kivipi, inanisoikitisha sana na kuona kweli vyeti feki bado vinasumbua...
c850695958684a3bd9c09c6156400279.jpg
 
Vipi geji Ikiwa mbovu au Inasoma empty?
 
Yani tuanze kuzurura na risiti? Yelewiiii
 
Hio proposal watakua wameiandika YONO AUCTION MART....maana road licence imefutwa, kazi ya kusaka Magari yasionayo imeisha... Wameomba wahamie huku kwenye mafuta na risiti waweze kuishi mjini.... Njaa mbaya walaiiiii
 
Kama mafuta umeyajaza wiki nzima, say ilikuwa fulltank na umetumia yamebaki nusu na risiti umeshatupa watakufanya nini?
 
Ungekosa risit ungepigwa faini mkuuu huja sikia tangazo lao???
 
Sidhani kama mkuu unachosema kina ukweli wowote. Mimi napita hapo si chini ya mara 16 kwa siku na ni kila siku. Sijawahi ona kitu kama hicho.
Mara 16 kwa siku? Kwani jamaa amesema wanakagua watu wa bodaboda?
 
Back
Top Bottom