Kina Mdee wataadhibiwa kwa kuvuliwa vyeo tu kwenye chama, wataendelea na Ubunge wao

Hakuna maazimio yatakayowaacha wabunge 19 salama, Maamuzi yanayokwenda kufanyika yataangazia zaidi ajenda za chama katika Uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, Kwamba hatutambui matokeo yoyote katika ule uchaguzi uliofanyika mwaka 2020.Kitendo cha wabunge 19 kuingia bungeni kwa milango ya nyuma ni kukiuka misimamo ya chama kuhusu uchaguzi.
Utasubiri sana. Leo utaijua chadema
 
Kamati kuu ya chadema inakaa Leo kujadili kuhusu kuapishwa wabunge wa viti maalumu 19 dodoma bila ridhaa ya chama.lakini kati ya wabunge hao 19, wabunge 5 ni wajumbe wa kamati kuu.
Yetu macho na masikioView attachment 1635571View attachment 1635572View attachment 1635575

Mkuu IFRS na Pascal Mayalla ninachokiona hapa ni kama "Press Release", je ilirushwa katika Chombo gani cha Habari?
Neno la Siku : Maendeleo ya Watanzania hayataletwa na vyama vya Siasa bali watanzania wenyewe.

Ahsante
 
Kama itathibitika alipigiwa simu na mwenyekiti ambao sio utaratibu rasmi zaidi ya ule wakuteuliwa na kamati kuu nitauona huo ujasiri wake..
Sio mara ya kwanza kwa Mbowe kuteua kwa simu viti maalum. Kama hujui habari ndio hiyo
 
Mungu mpe afya njema jembe letu Halima mdee na wenzie,wape ulinzi kama uliowapa wana wa Israel kutokana na madhara ya mafarao wa Misri wakina farao Erythrocyte ,farao Mmawia ,farao tindo ,farao imhotep ,farao Braza j .
"Aamin"
Hivi bongo neno Mungu ni kiungo kama na nini? Mbona anatajwa sehem zisizo sahihi wakati usio sahihi kwa mtindo usio sahihi. Tafadhali mnaeza jenga hoja bila kumuhusisha creator kwa mizaha.
 
Nitabakia kuwa Tomaso hadi dk ya mwisho kuamini kwamba Mwenyekiti ameshiriki dhambi hii.


Ambacho hakiniingi akilini ni kwamba CHADEMA wanahitaji Ruzuku zaidi kuliko dhurma na hila zote hizo walizofanyiwa kwemye uchaguzi Mkuu kumfanya Mwenyekiti atumie mbinu za gizani kuwapeleka kina Mdee bila idhini ya Kamati Kuu?. no no no Mwenyekiti Mbowe si mtu chiep kiasi hiki.
 
Ndio, mfano CHADEMA wabaki na mbunge mmoja tu bungeni ruzuku inapungua sana au inaweza isiwepo. Ila kikubwa zaidi ni utamaduni uliowekwa kwenye katiba ya chama ya wabunge kukatwa pesa kwenye mishahara kila mwezi kuchangia maendeleo ya chama. Kwa 2015 - 2020 wabunge wa CHADEMA wa viti maalum walikuwa wanakatwa mil.1.5 kila mwezi na wa kuchaguliwa wanakatwa laki 5 kwa mwezi kwa miaka mitano. Sasa hawa 19 wakipewa baraka na chama kimyakimya wakaambiwa itabidi wakatwe wachangie milioni 2 kila mwezi hawawezi kukataa. Kwenye mshahara wa mbunge wa mil.12 wanabakiza 10 ni nyingi sana. So, mil.2 x 19 = 38,000,000(mil.38) x 12(mwaka 1)= 456,000,000(mil.456) kwa mwaka. Almost nusu bilioni. Ndo maana tunasema uongozi wa chama hauwezi kukubali kuzikosa hizi pesa sababu hauna vyanzo vya pesa. CHADEMA itajiendeshaje bila michango Kama hiyo na ruzuku ya kueleweka!?. Ndo maana tunawaambia wale wafuasi maandazi kuwa akina Mdee hawawezi kufukuzwa CHADEMA. Ni rahisi Lissu kuhama chama au Mnyika kuambiwa ajiuzulu kuliko kuwafukuza uanachama hawa wamama 19. Kesho ndo utanielewa vizuri mkuu.
Kwa hiyo kiongozi ndugai anaipenda sana chadema isife wakati mkuu wa nchi anataka kuua upinzani kabisa?
 
Mnyika ajiuzulu hii nafasi kulinda heshima yake. Mnyika na Lissu wakiunda chama chao wana wafuasi wengi mno.
Kwamba mbowe kahusika? Hem tuje hapa mbowe alikuwa na uwezo gani wa kumtoa nusrat gerezani maan majina yalipelekwa tarehe 20(kwa mujibu wa ndugai) au unamaanisha mbowe anashirikiana chombo kikuu?
 
Kwanza kabisa ifahamike kwamba yote yaliyofanyika yana baraka zote za Mwenyekiti.

Sasa ili kujikosha na kuwazuga wafuasi sugu wa CHADEMA, Mbowe atakuja na blah! blah! kibao kisha atahitimisha kwa maneno yafuatayo:

"Kitendo kilichofanywa na viongozi wa BAWACHA ni cha utovu wa nidhamu na hivyo chama kinawavua uongozi katika ngazi zote za chama!"

Basi , watu wanaendelea kula mpunga na maisha yanaendelea.
Fukuzilia mbali ,hao 19 kwasasa sio wanachadema ,washanunuliwa na MEKO.
 
Hivi bongo neno Mungu ni kiungo kama na nini? Mbona anatajwa sehem zisizo sahihi wakati usio sahihi kwa mtindo usio sahihi. Tafadhali mnaeza jenga hoja bila kumuhusisha creator kwa mizaha.
Bila Mungu akuna linalowezekana.
kama auamini Mungu basi polesana.
 
Ili kulinda msimamo na heshima ya chama mbele ya watanzania na jumuia ya kimataifa kutokana na Uchaguzi haramu uliofanywa ni bora Chama kiwafukuze kabisa hata kama hawatafukuzwa ubunge!
Waswahili wanasema bora lawama kuliko fedheha!
 
Bila Mungu akuna linalowezekana.
kama auamini Mungu basi polesana.
Hhhh mkuu hujaelewa nachosema hapo? 2angalie sehemu tunazomtaja hasa sehemu za kuchagua pande katika mabishano kama haya ya kisiasa tusije mkwaza labda kama tunatofautiana imani. Kama pale umemtaja kimzaha sana. Anyways kila mtu ana njia za kumuabudu ila ushauri 2 hizi sehem sio salama sana. Ahsante.
 
Hhhh mkuu hujaelewa nachosema hapo? 2angalie sehemu tunazomtaja hasa sehemu za kuchagua pande katika mabishano kama haya ya kisiasa tusije mkwaza labda kama tunatofautiana imani. Kama pale umemtaja kimzaha sana. Anyways kila mtu ana njia za kumuabudu ila ushauri 2 hizi sehem sio salama sana. Ahsante.
Kila jambo ni lazima umtangulize na kumshukuru Mungu kwanza.
kwake yeye kila jambo anatimiliza.
 
Kamati kuu ya CHADEMA inakaa Leo kujadili kuhusu kuapishwa wabunge wa viti maalumu 19 dodoma bila ridhaa ya chama.lakini kati ya wabunge hao 19, wabunge 5 ni wajumbe wa kamati kuu.
Yetu macho na masikioView attachment 1635571View attachment 1635572View attachment 1635575
Kama kweli HAYO yanatoka kwake HALIMA basi atapewa nafasi ya kuyaelezea vizuri ndani ya kikao.
Wasaliti na wabia wao ndani ya chama lazima KWANZA wawekwe bayana na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Wale WANAOTAKA kuwalinda wajifunze kuheshimu na kwa upolee wangojee mchakato wa ndani ya CHADEMA ukamilike. Amen
 
Kweli Laana imeshaanza kuwala. Halima wa kutueleza kuwa wameteuliwa kwa Simu ya Mbowe kweli??

Huyu si Mwanasheria na Mwanachama Mkongwe wa Chadema huyu? Hivi kweli hafahamu kuwa Kamati Kuu ndio inayoteua wabunge wa Viti maalum na sio Mbowe?? Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.

Halima anajiaminisha kwamba yeye ana akili kubwa kuliko watu wote wanaomshangaa kwa upuuzi alioufanya. Yani kasaliti Chama chake lakini bado anajamba maneno.

Naweza kuwahakikishia kuwa mismanagement ya hii issue itakiua na kukipoteza Chadema na kukiacha Kama kilivyo Chama Cha CUF, TLP na NCCR.
Ushetani wazidi kujifunua mpaka kufika kwenye utakuwa wazi na mawakala wa shetani kokote waliko watakuwa wazi. CHADEMA iwateme wasaliti na washirika wao.
 
Back
Top Bottom