greater G
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 308
- 215
Leo mchana wakati natoka kibaruani kwangu kwa miguu nilipita mtaa fulani hivi.
Wakati nipo kwenye mtaa huo nilimuona Mama mmoja kama mwenye miaka 30_35, kilichonishangaza ni kusikia maneno makali tena machafu (matusi ya nguoni) akimporomoshea mwanae wa kiume ambaye kama atakuwa na umri mkubwa atakuwa na miaka 12.
Kilichonisikitisha matusi yenyewe yalikuwa yanamhusu yeye mwenyewe.
Kwa fikra zangu nikajiuliza, huyu mama;
1. Ana mtukana mwanae au anajitukana?
2. Anamfundisha nini kijana wake huyo?
3. Huyu mama, anaelewa kweli anachokifanya?
4. Huyu mama ni mzima kiakili au?
Kina mama angalieni mnayowaambia watoto wenu bana!
Sasa mfano, unapomwita mtoto wako Mbwa au Nguruwe inakuwaje hapo? Yeye ndo Mbwa/Nguruwe au wewe ndo uliyeanza kuwa hivyo.
Badilikeni bana!