Kimzaha mzaha

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,267
Reaction score
144,418
Salaam wadau,

Hebu tuachane kidogo na mambo ya UKUTA. Huo uliporomoka jana baada ya kuwashwa kwa tingatinga.

Sasa bana, ni hivi...na hapa nazungumzia kwa wanaume ingawa hata kwa wanawake inaweza kuwepo.

Inatokea unakutana na mtu sehemu. Mnabadilishana namba na nini nini...si unajua tena siku hizi mambo ya haya mamitandao ya kijamii. Sijui twita, instagramu, na ushuzi shuzi mwingine kama huo.

Mkishabadilisha hivyo mnaanza kuchati kikawaida tu. Mara mtu unaamua kujaribu kutongoza. Kimzaha unamuomba mtoke. Wewe hapo unadhani mwenzio atakukatalia, kwa hiyo unakuwa tayari ushajiandaa kusikia 'hapana'.

Basi unarusha ndoano yako. Unamuomba mtoko. Kabla hajakujibu, unakuwa na shauku ya kuona jibu lake licha ya kuwa unahisi atakataa.

Mara jibu hilo, linaingia. Unalisoma...mwenzio kakubali. Unapigwa na mshangao kwanza...maana ulikuwa hutegemei akubali.

Unaanza kuwaza sasa ujipange vipi maana kumwambia kuwa ulikuwa humaanishi huwezi.

Ila ndo hivyo tena, mwenzio kakubali na wewe unakuwa huna jinsi, unajipanga.

Siku ya mtoko inafika, mnakutana, mnaendelea na mambo yenu.

Mbele ya safari mtaamua wenyewe itakuwaje.

Mpo ambao imeshawahi kuwatokea hivyo?
 
umekosea mkuu muda mwingine kipindi mnaanza mawasiriano jana yake katoka kugombana na x wake wewe ukajiingiza kati ukamfanya asahau yaliyopita ingekuwa ni wewe ungejipa jina la easy going hapo?

Kwa hiyo hapo mtu unatumika kama rebound, siyo?

Damn this life.
 
umekosea mkuu muda mwingine kipindi mnaanza mawasiriano jana yake katoka kugombana na x wake wewe ukajiingiza kati ukamfanya asahau yaliyopita ingekuwa ni wewe ungejipa jina la easy going hapo?
Ukianguka amka jifute then songa mbele. Sasa mkuu huyo hata kujifuta aseeh? ?
Sometimes vuta ni kuvute inaraha zake eddy_mhando
 
Inabidi upimwe we unayemwambia unataka kutoka nae ka uko sawa kichwani kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…