kimya chenye mshindo!...

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
when the man is silent it is easy for the woman to imagine the worst

Women misinterpret a man's silence. Depending on how she feels that day, she may begin to imagine the worst- "He hates me, he doesn't love me, he is leaving me forever". This may trigger her deepest fear, which is " I am afraid that if he rejects me then I will never be loved. I don't deserve to be loved." - John Gray

...kina baba, ...muwe na huruma kwa wake zenu/wapenzi wenu. Mnawapa wakati mgumu sana kina kina mama mkinuna bila kuwaambia 'kulikoni', au wewe unaonaje?
 
ushauri tu kwa wanaopata mchecheto 'mtu wako wa karibu' asipowasiliana nawe ... badala ya kufikiria the worst fikiria minor things like perhaps yuko bize, simu haina airtime, charge etc, na sometimes people need to be left alone kidogo kutafakari maisha!
 
...mikoa ya pwani, pamoja na kule visiwani husemwa; "...ameolewa chuo cha ngapi?..." kwa maana kwamba maisha ya ndoa (kwa mwanamke) ni sawa na elimu!

Kwa waliobahatika kudumu kwenye "chuo kimoja" mpaka kifo kitapowatenganisha, huitwa waliofuzu...! ama kwa hakika, Ustahmilivu na busara za mke ni ngao kubwa katika kudumisha ndoa za kikwetu.

Men argue for the right to be free while women argue for the right to be upset. Men want space while women want understanding." -John Gray

...Badala ya kujiliwaza nyumba ndogo au kwa kinywaji, tuwajali kina mama kwenye manung'uniko yao, ili nao wajali uhuru wetu wa 'kuuchuna' pale (wanaume) tunapokuwa kwenye msongo wa mawazo.
 
Mbu,
Mimi nilijua kuwa kukaa kimya na kununa ni tabia ambazo wanawake wanaambiwa kuwa wanazo.Sikujua kuwa hata wanaume wananuna!
Sasa mwanaume unaponuna, unataka mwanamke afanye nini? Nilifikiri mwanaume anapaswa kusema kama kuna kitu hakiendi sawa na siyo kununa.Akinuna na mwanamke akanuna halafu wanakaaje?
Kuna hadithi nilisikia kuwa mke na mume kwenye nyumba walikuwa hawasemezani.Wanapeana ujumbe kwa maandishi tu( bora na sasa kuna sms ambapo ikiingia angalau utasikia mlio na utajua kuna ujumbe).Ikafika siku bwana anasafiri.Akamwandikia mkewe kwenye karatasi " kesho uniamshe saa 11 ili niwahi ndege airport"..mke akaisoma, wakalala.Ilipofika saa 11, mke akamwandikia kinote
" amka,imefika saa 11" akakiweka juu ya meza akarudi kulala.Mume anashtuka ni saa 1 asubuhi! Akakurupuka na kuanza kumgombeza mkewe kwa makelele..." mbona hukuniambia ilipofika saa 11?" mke naye akajibu kwa kupayuka , "angalia mezani, nilikuandikia ujumbe ,Hukuusoma?"
Hayo ndiyo matokeo/hasara ya kununiana!
 
bwana gray hajakutana na wanawake ngangari.
unauchuna na wao wanauchuna kisha mawasiliano yanakuwa
kupitia kwa mtoto/watoto (kama wapo) au vi-note tu kama
hakuna third party ndani ya nyumba.

kasheshe mzee mzima umelala usingizi mzito na ulimwomba madamu,
kupitia kinote, akuamshe asubuhi kwani unataka kuwahi unapoachiwa kinote pembeni ya kitanda "amka utachelewa basi/ndege" halafu yeye anaendelea
kuuchuna akidai ndo ameshakuamsha lol
 
Kama mume akiuchuna na mwanamke akianza kupatwa na wasi wasi basi lazima kuna jambo baya atakuwa amelifanya shidi ya mume wake. Mume anaweza kuwa amejichokea na kuamua kujipumzisha tu, lakini hisia za mabaya aliyoyafanya ndizo zitamtesa mke
 
...hizo za mume na mke kuandikiana vi note, kuna mwanamama aliamka, kakoga, kaandika ki note kisha huyoooooo kazini...

...saa sita anapigiwa simu na mawifi kuuliziwa yupo wapi. Kumbe muda wote ule asubuhi, mumewe alikuwa keshafariki!...

si mshindo huo?
 
Kuhusu mwanaume kukaa kimya....

Kuna wakati mimi nilikuwa na mawazo kiasi ya kwangu ambayo niliona siwesi ku"share" na wife kwasababu mitazamo yetu ingekuwa tofauti na nilihisi majibu atakayotoa kuhusu mawazo yangu yangeniudhi.

Hivyo nikaamua kukaa kimya na kuyatafakari mawazo hayo peke yangu. Ilinichukua siku kadhaa....kila nikirudi kazini...baada ya salamu mimi nilikaa kimya na kuwaza mpaka nikapitiwa na usingizi.

Wife alianza kulalamika kwamba " I don't Love her any more".. Pia alianza kujihisi kwamba "maybe she's not good enough for me....and that I might have found someone else better than her .........to replace her".
Sitafanya hivyo tena kwani ilikuwa ni kama adhabu kwake.
 
Hadi kununiana kwenye ndoa kulikoni? mie siwezi kukaa na dume ananuna maana sasa itakuwa kero tena, raha ya ndoa furaha daima.
 
Hadi kununiana kwenye ndoa kulikoni? mie siwezi kukaa na dume ananuna maana sasa itakuwa kero tena, raha ya ndoa furaha daima.

...Pretty, pretty, pretty,...! maisha ya ndoa ni sawa na mawimbi baharini, kuna siku za kaskazi, na kuna siku za shwari tamu kama peremende...

Hebu msome Rodelite hapa chini...

Kuhusu mwanaume kukaa kimya....

Kuna wakati mimi nilikuwa na mawazo kiasi ya kwangu ambayo niliona siwesi ku"share" na wife kwasababu mitazamo yetu ingekuwa tofauti na nilihisi majibu atakayotoa kuhusu mawazo yangu yangeniudhi.

Hivyo nikaamua kukaa kimya na kuyatafakari mawazo hayo peke yangu. Ilinichukua siku kadhaa....kila nikirudi kazini...baada ya salamu mimi nilikaa kimya na kuwaza mpaka nikapitiwa na usingizi...

...bwana John Gray anatuambia;

"...when the man feels appreciated for listening and he doesn't feel rejected for not sharing more, he will gradually open up"
 
"when a woman's wave crashes is a time of emotional cleansing or emotional housecleaning.

One study revealed that a woman's self esteem generally rises and falls in a cycle between 21 and 35t days" -John Gray

...kwa wenye ndoa naamini hakuna mgeni wa hali hii. Mpo nyumbani wikiendi mara mkeo bila sababu yeyote anakurupuka kupangua makabati na usafi hapa na pale huku akitoa shutuma na lawama kibao.

... ukijaribu kuulizia kulikoni, au kumtuliza ndio kwanza unachochea ghadhabu zake!
 
Akufukuzae hakuambi toka. kuna kununa kwa hali nyingi .uchovu.wivu.njaa.kukosa pesa.kumjaribu anipenda.hiyo yote ni kununa.hayo ni majukumu ya mke kujua mumeo anapenda kipi amfanyie ili amfuhishe mumeo .sasa unapoolea tu.anza deko yakumuuliza wewe mume wangu kipi unapenda nakipi hupendi.na kwavile ni kipya kipya. atakwambi.hapo unajua leo kanuna nija wahi mlo.pesa mliwaze.uchovu masagi.mhakikishie ukitoka mpaka akuruhusu .ukikosa kabla hjasema omba msamaha .HAUTASIKIA UGOMVI .utusikia kwajirani. uzingatie ushauri huu.
 
...ami hapo wanena hasaaaaaa....! usemayo yote sawia, ilmu yako imesheheni kusema in'toka n'tambile kupita chake, mzambarauni mpaka konde!

lakini yakhe 'nikuume sikio!' ...wanawake wa kileo (wakimjini) kwayo hayawezeka-ni!
 
...kina baba, ...muwe na huruma kwa wake zenu/wapenzi wenu. Mnawapa wakati mgumu sana kina kina mama mkinuna bila kuwaambia 'kulikoni', au wewe unaonaje?
Upo sahihi sheikh.
Shemeji yako alinikorofisha kidogo(mambo ya kawaida tu,ila yalihitaji ni-ESTABLISH position yangu kama baba)
Yeye yupo kwenye contraceptives,takribani miezi mitano alikuwa hajaingia kwenye period.

Kilichotokea mkulu, sikuzungumza wala kununa,JUST KIMYA, mkulu nafanya mambo kwa vitendo kwa siku mbili,you know what happened?

Siku ya pili alipata bleeding ya nguvu na kasi isiyo ya kawaida.

So,you are right mkulu.

Hakuna sababu ya kupigana mpaka mtoane ngeu au mkusanye majirani.

Another advantage, ni risk ya kutamka maneno yasiyofaa ambayo baadaye utayajutia is kept at a minimal level.
 
Hilo nalo neno
Mbu,
Mimi nilijua kuwa kukaa kimya na kununa ni tabia ambazo wanawake wanaambiwa kuwa wanazo.Sikujua kuwa hata wanaume wananuna!
Sasa mwanaume unaponuna, unataka mwanamke afanye nini? Nilifikiri mwanaume anapaswa kusema kama kuna kitu hakiendi sawa na siyo kununa.Akinuna na mwanamke akanuna halafu wanakaaje?
Kuna hadithi nilisikia kuwa mke na mume kwenye nyumba walikuwa hawasemezani.Wanapeana ujumbe kwa maandishi tu( bora na sasa kuna sms ambapo ikiingia angalau utasikia mlio na utajua kuna ujumbe).Ikafika siku bwana anasafiri.Akamwandikia mkewe kwenye karatasi " kesho uniamshe saa 11 ili niwahi ndege airport"..mke akaisoma, wakalala.Ilipofika saa 11, mke akamwandikia kinote
" amka,imefika saa 11" akakiweka juu ya meza akarudi kulala.Mume anashtuka ni saa 1 asubuhi! Akakurupuka na kuanza kumgombeza mkewe kwa makelele..." mbona hukuniambia ilipofika saa 11?" mke naye akajibu kwa kupayuka , "angalia mezani, nilikuandikia ujumbe ,Hukuusoma?"
Hayo ndiyo matokeo/hasara ya kununiana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom