Elections 2010 Kimya cha CHADEMA kikubwa

Huyu jamaa ni clean hata CCM-fisadi wakimwaga sumu hawatafanikiwa sana, hata kama atashindwa lakini atakuwa ameleta changamoto kwa siasa za baadae za tanzania.

Luteni, usisahau kwamba kuna heshima ya mtu at steak vile vile. Akishindwa kwa mara ya pili hata kama atakuwa ameleta changamoto yoyote ile huoni kwamba itakuwa imemvunjia heshima na rekodi yake nzuri? Kwa jinsi hali ilivyo sasa hivi SAS mtakuwa mnataka kumuumiza bure kutaka ajiingize kushindana na CCM iliyojaa ufisadi na mbinu chafu zisizojali utu wa mtu. CCM walimwaga sumu wakati ule wakafanikiwa watashindwa kumwaga sumu kali zaidi katika wakati huu ambao wako katika hali ya kutapatapa? Tafuteni vijana wazalendo wenye mwelekeo wa kutaka kulitumikia taifa kwa uadilifu ili wakapate nasaha na ushauri kutoka kwenye kisima cha busara za kila aina alichonacho kutokana na uzoefu wake wa siasa za ndani ya nchi na za kimataifa.
 
Sas chadema? No, no way hawezi kuhama ccm, nina hakika ni mmoja wa watanzania wachache wenye uchungu wa kweli na nchi hii, huyu namuweka kwenye kundi la kina warioba, msuya na butiku. Nina hakika hawa watu hawakubaliani na jinsi serikali inavyoendeshwa lakini mfumo wa siasa za ccm ni kikobekobe kuinama na kuangalia tu , si ndio wenzao hao !! Ni game of chance anayepata anatumia , aliyekosa anasubiri miaka kumi ya kubahatisha kijiti tena.
 
Huyo Salim hata akirushiwa bomu la machozi atakuwa hoi, sio ngangari kama Mrema, Mbowe au Salim. Hawezi, na hata siku moja hatathubutu kujiingiza kwenye siasa za mabavu, mshike mshike.

Kibaya alishindwa kihalali alipogombea 2005. Mwache aendelee kula pension yake.

Mpeni Mengi hiyo nafasi maana nimesikia anaitaka.
Tatizo letu bado tuna mawazo kuwa siasa ni ugomvi vurugu ngumi mkononi hatufikiri zaidi ya hapo
 
Daaahh siamini, but kila kitu chawezekana. The guy was the one to chair presidential sit, lakini bse ya mizengwe na majungu ya CCM hakufanikiwa.

Ni kati ya viongozi wachache bora na wenye maadili mazuri aliyebaki TZ kwetu.

Let us C and GOD bles him.
 
Luteni, usisahau kwamba kuna heshima ya mtu at steak vile vile. Akishindwa kwa mara ya pili hata kama atakuwa ameleta changamoto yoyote ile huoni kwamba itakuwa imemvunjia heshima na rekodi yake nzuri? Kwa jinsi hali ilivyo sasa hivi SAS mtakuwa mnataka kumuumiza bure kutaka ajiingize kushindana na CCM iliyojaa ufisadi na mbinu chafu zisizojali utu wa mtu. CCM walimwaga sumu wakati ule wakafanikiwa watashindwa kumwaga sumu kali zaidi katika wakati huu ambao wako katika hali ya kutapatapa? Tafuteni vijana wazalendo wenye mwelekeo wa kutaka kulitumikia taifa kwa uadilifu ili wakapate nasaha na ushauri kutoka kwenye kisima cha busara za kila aina alichonacho kutokana na uzoefu wake wa siasa za ndani ya nchi na za kimataifa.
Bibi Ntilie

Ukiogopa kuwa wa mwisho darasani usiende shule, lakini sidhani kama hiyo itasaidia kutunza heshima yako.
 
Nyie nyie. Mnaelewa mnachokizungumzaa??? Hivi ni nani mjinga ambaye umri wake umeenda na anakaribia kuf kufa anataka kujimaliza kisiasa saa hizi za magharibi? Mbona mwaongea pumba nyie??!

Hey, Hey, si jambo jema kuzungumzia ya mtu kufa, unaweza kufa wewe kabla yake!
 
Salim hana chochote cha kuogopa. Naamini ni msimamo tu ndio alionao.
Waliujua msimamo wake ndiyo maana wakamwekea mizengwe 2005 I wish angekuwa rais wa Tanzania leo nafikiri tungekuwa mbali ukilinganisha na majirani zetu Rwanda Kenya na Uganda.
 
Waliujua msimamo wake ndiyo maana wakamwekea mizengwe 2005 I wish angekuwa rais wa Tanzania leo nafikiri tungekuwa mbali ukilinganisha na majirani zetu Rwanda Kenya na Uganda.

Kwa yule anayebisha na kukejeli asubiri kama jamaa akichukua forms ila awe amejiandaa tu kama kweli hizi habari kama ni porojo au propaganda za kumvutia basi ni afadhali ajilie penseni yake tu.
 
Chadema haimuitaji...ila yeye anaihitaji Chadema kama ana nia ya kweli ya kuletea maendeleo watanzania
 
Kweli mkulu ungetusaidia kuunga hizo dots ili nasi tufunguke kiasi na twende sawa sasa.
 
LUTENI CORNEL umezipata wapi hizo nyepesi? Tusije tukachangia uwongo?
Ila kama ni kweliaje na nia Thabiti ya Kuongoza na Nia ya kuwakomboa Watanzania.
 
Henu tueleze dots chache ulizozipata umeipata wapi na unadhani zina uzito gani kulingana na ulikozichimba

Kweli mkulu ungetusaidia kuunga hizo dots ili nasi tufunguke kiasi na twende sawa sasa.

LUTENI CORNEL umezipata wapi hizo nyepesi? Tusije tukachangia uwongo?
Ila kama ni kweliaje na nia Thabiti ya Kuongoza na Nia ya kuwakomboa Watanzania.
Dots hizo hata mimi bado nazifuatilia ingawa inafanywa siri lakini wadondoaji wa mambo wanasema kuna koneksheni ya suala hili na usajili wa Ccj.
 
Popote atakapokuwepo kichama, kama akigombea urais, kura yangu tayari anayo.
Hata akisimamishwa na CCM
 
Back
Top Bottom