simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,698
- 9,590
Wantazania someni novels za kingereza na kutizama movie za Hollywood pamoja na kisikiza BBC english. English lazima kupanda.
Mkuu umenivunja mbavuExperience yangu ni opposite. Mara ya kwanza nimetia mguu kwa Trump najitambulisha darasani hakuna mtu ananielewa utafikiri naongea Kisukuma. Nikajaribu kuongea pole pole ndiyo njemba zinaniuliza "You are from Taiwan?" Nikaitamka Tanzania kwa uangalifu jamaa hazielewi basi nikaamua kutumia mifano ya Mlima Kilimanjaro na Serengeti + "Hakuna Matata" kuwa ni Kiswahili na ni lugha yetu ya Tanzania ndo nikaona vichwa vinatikiswa. Kuingia darasani Prof mmoja mashuhuri sana wa Economics aisee simwelewi kabisa. Lafudhi yao ajabu ajabu. Jioni hiyo binti mmoja Mzungu akaja kuniongelesha basi nikamganda nikamwambia awe ananisemesha mara kwa mara ili nizoee lafudhi yao. Miezi sita ya mwanzo was hell mpaka nilitamani kupanda ndege kurudi Misungwi. Mpaka leo huwa naamini kwamba siye tuko majiniazi aisee kwani kuweza kusoma na kufaulu kwa lugha ambayo hatuielewi sawasawa (Kiingereza) siyo kazi rahisi jamani.
Shukrani kwa ufafanuzi mkuu, umenifurahisha sana kugusia kimombo cha mnigeria ile ndo babu kubwa.Kimombo halisi ni kipi mkuu? Uzuri/ubaya ni kwamba kwa sasa Kiingereza tunaweza kusema kuwa ni lugha "isiyo na mwenyewe" kwa sababu kila mmoja ana lafudhi yake haijalishi kama lafudhi yenyewe inatambuliwa kuwa ndiyo rasmi ama la! Ni wazi kuwa viingereza rasmi vya Uingereza, Marekani, Australia, New Zealand, Afrika Kusini, India, huku kwetu Afrika Mashariki, Wanigeria kule na kwingineko ni tofauti mno na pengine hakuna haja ya kuchekana. Kinachotatanisha kwetu sisi ni hii sera yetu ya ajabu ya elimu ya kufundishia ambayo inamwacha mtoto njia panda akiwa siyo mbobezi wa Kiswahili au Kiingereza.
Roommate wangu huko kwa Trump alikuwa Mchina na alikuwa anasoma Nuclear Physics. Kiingereza chake kilikuwa hopeless kabisa lakini makabati yake yalikuwa yamejaa mavitabu manene ya Kichina na alikuwa anahangaika nayo usiku kucha. Mwenzangu huyu ingawa Kiingereza chake kilikuwa cha shida lakini angalau alikuwa na marejeo ya masomo yake katika lugha ya mama anayoielewa vizuri. Sisi masikini Kiingereza ndo hivyo na huna mahali pa kukimbilia mtu inabidi ukomae tu ikibidi kukariri unakariri ili mambo yaende. Ndiyo maana elimu yetu haina manufaa sana kwa sababu kuna mpishano mkubwa kati ya maarifa na lugha ambayo kupitia kwayo maarifa hayo yanatufikia. Tunajidhulumu na kujidogosha wenyewe!
Habari zenu bandugu!
Hebu wale waliowahi kufundishwa na wazungu mpite hapa kutoa ushuhuda wenu wa siku zenu za awali mlivyokuwa mkipokea pindi la mzungu...
Binafsi naanza kutoa ushuhuda wangu pale tulipokuwa A-level ktk moja ya shule za serikali tukipigishwa Inorganic Chemistry na mwalimu wa Kimarekani wa kujitolea aliyekuwa akiitwa Sir Briszzcky. Jamaa alikuwa hamisi pindi na hachelewi hata dkk1 ila wengi tulikuwa twatoka kapa kutokana na ung'eng'e wake na hivyo kudoji pindi zake kwa madai ya kuwa jamaa alikuwa shallow...!
Mshua alichangia sana ktk lugha yako kwa kweli na hivyo ndio yatupasa tuwe twafatilia watoto wetu...Sio mzazi akomaa tu na ripoti za kila baada ya miezi 6!Daah mie nakumbuka naenda kuanza form I shule moja ya Catholic..tuna walimu mapadre na masista...
Dah...kuna mmoja alikuwa wa Biology..Ni muhindi ila kakaa sana Ulaya..pata picha..
V na W kuzielewa ni mziki..
Kuna wa Physics..Mmarekani..ni sheedah..Yaani the first six months..Nilimwambia bi mkubwa nahisi kama shule inanishinda.
Kuna wa Kiingereza..mmoja Mganda,mwingine Mkenya...matamshi ya a na o..
Ila inshallah after a year nilikuwa natiririka vizuri..
Kimbembe ukirudi home..mshua anakuja na migazeti yake mikubwa Daily News,Guardian,the East africcan.
Anachagua yale mavitabu ya Nyerere na columns ya kina Jenerali Ulimwengu,Onyango Obbo,Makwaia..et al..
Ananiambia nisome,niandike comprehension summary..Daah..Nguvu zilikuwa zinaisha.
Yeye he doesn't give a damn umefaulu history,maths au chemistry..so long you cant write or speak properly you don't understand..
Halafu hata hazisomi..sasa bhana mie nkawa najisahaulisha kumbe mzee ananilia timing..
Akauliza za wiki mbili ziko wapi..
I wont forget that day in my life...
Ila all in all..Nawashukuru wote kwa juhudi zao..Leo walau naeza ongea dakika 20 mbele ya umati..
Lakini tuna Language Crisis kwenye hii nchi.. Kiswahili hatukiju,cha Malkia ndo kabisa..
Tumebaki na Singeli tuu...
Sisi waswahili ni shida Mkuu.Yah ni kweli rafiki...tatizo sisi ndo twajifanya kumcheka na kumdhihaki mtu anayebangaliza kimombo na ndio maana watu wengi wanaishia kukata tamaa kuendeleza jitihada za kuzungumza kimombo. Sentensi yako moja tu ya kiingereza itazua post lukuki ktk mitandao ya kijamii bila kusahau JF. Na watu wanaweza tamani kukukwapua kadigree kako, inabidi ujivishe vazi la uzalendo tu kwa kuzungumza kiswahli na kuchomekea misamiati ya kimombo.
Hujauelewa mhimili wa hoja yangu!Kukariri sio ugeneous..
Me si mwalimu ila kazini kuna wazungu wa kwa malkia. Accent yao ngumu bora Americans! Akija offisin kuongea anavyoteleza ile lafudhi yao huelewi yani me ni pardon Pardon haziishi!
Hawa ndugu kama wanakuongelesha unaeza kutamani uombe subtitlescDNA said:Habari zenu bandugu!
Hebu wale waliowahi kufundishwa na wazungu mpite hapa kutoa ushuhuda wenu wa siku zenu za awali mlivyokuwa mkipokea pindi la mzungu...
Binafsi naanza kutoa ushuhuda wangu pale tulipokuwa A-level ktk moja ya shule za serikali tukipigishwa Inorganic Chemistry na mwalimu wa Kimarekani wa kujitolea aliyekuwa akiitwa Sir Briszzcky. Jamaa alikuwa hamisi pindi na hachelewi hata dkk1 ila wengi tulikuwa twatoka kapa kutokana na ung'eng'e wake na hivyo kudoji pindi zake kwa madai ya kuwa jamaa alikuwa shallow...!