Kimombo cha wazungu na changamoto zake

cDNA

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
353
348
Habari zenu bandugu!
Hebu wale waliowahi kufundishwa na wazungu mpite hapa kutoa ushuhuda wenu wa siku zenu za awali mlivyokuwa mkipokea pindi la mzungu...
Binafsi naanza kutoa ushuhuda wangu pale tulipokuwa A-level ktk moja ya shule za serikali tukipigishwa Inorganic Chemistry na mwalimu wa Kimarekani wa kujitolea aliyekuwa akiitwa Sir Briszzcky. Jamaa alikuwa hamisi pindi na hachelewi hata dkk1 ila wengi tulikuwa twatoka kapa kutokana na ung'eng'e wake na hivyo kudoji pindi zake kwa madai ya kuwa jamaa alikuwa shallow...!
 
Kwi kwi kwii...Hapo mkuu ndio utaona tofauti ya kimombo cha teacher wa kimatumbi na mzugu.
Kweli mkuu Afu yule Prof alikuwa na tabia flan hv ukikaa mbele anauliza swali afu anakupa mic ujibu so one day akamuuliza mshikaji do you have notochord??? kwa ile lafudhi yake Jamaa kwa ujasiri na sauti akasema YES but I leave at MABIBO kilichofuata mkuu unaelewa kabisa
 
Ha ha haaa...inafurahisha sana ndugu huo ndio uhalisia wenyewe.
 
Uzuri wa hawa watu wanajua kiingereza sio lugha yako so wanakusikilza kwa makini na hawakucheki bali hukutia moyo tofauti na sisi tunaochekana
Yah ni kweli rafiki...tatizo sisi ndo twajifanya kumcheka na kumdhihaki mtu anayebangaliza kimombo na ndio maana watu wengi wanaishia kukata tamaa kuendeleza jitihada za kuzungumza kimombo. Sentensi yako moja tu ya kiingereza itazua post lukuki ktk mitandao ya kijamii bila kusahau JF. Na watu wanaweza tamani kukukwapua kadigree kako, inabidi ujivishe vazi la uzalendo tu kwa kuzungumza kiswahli na kuchomekea misamiati ya kimombo.
 
Experience yangu ni opposite. Mara ya kwanza nimetia mguu kwa Trump najitambulisha darasani hakuna mtu ananielewa utafikiri naongea Kisukuma. Nikajaribu kuongea pole pole ndiyo njemba zinaniuliza "You are from Taiwan?" Nikaitamka Tanzania kwa uangalifu jamaa hazielewi basi nikaamua kutumia mifano ya Mlima Kilimanjaro na Serengeti + "Hakuna Matata" kuwa ni Kiswahili na ni lugha yetu ya Tanzania ndo nikaona vichwa vinatikiswa. Kuingia darasani Prof mmoja mashuhuri sana wa Economics aisee simwelewi kabisa. Lafudhi yao ajabu ajabu. Jioni hiyo binti mmoja Mzungu akaja kuniongelesha basi nikamganda nikamwambia awe ananisemesha mara kwa mara ili nizoee lafudhi yao. Miezi sita ya mwanzo was hell mpaka nilitamani kupanda ndege kurudi Misungwi. Mpaka leo huwa naamini kwamba siye tuko majiniazi aisee kwani kuweza kusoma na kufaulu kwa lugha ambayo hatuielewi sawasawa (Kiingereza) siyo kazi rahisi jamani.
 
Fantastic...vijana inabidi wajifunze kupitia uzi huu kuwa ung'eng'e ambao wengi wawatambia wenzao Bongo ukikumbana na baadhi ya wazungu au ukienda mamtoni utakuwa kila wakati sorry...sorry...unaomba warejee maneno na wewe unapojaribu kuzungumza hawakuelewi kabisa kuonesha matamshi yako ni tofauti kabisa na kimombo halisi...
 
Wakati niko A-level na HKL yangu, mwl wa English alitoka Finland (Madam Katrin). Hachelewi na hakuwahi kudoji kipindi chake.
Alipokuwa anafundisha Phonetics and Phonology, kwa wengi yalikua majanga. Ukimgeukia mwenzio utakuta kakunja uso kama anakamuliwa jipu vile.

Ki ukweli alinisadia sana kupata walau kiingereza cha ugoko
 
Fantastic...vijana inabidi wajifunze kupitia uzi huu kuwa ung'eng'e ambao wengi wawatambia wenzao Bongo ukikumbana na baadhi ya wazungu au ukienda mamtoni utakuwa kila wakati sorry...sorry...unaomba warejee maneno na wewe unapojaribu kuzungumza hawakuelewi kabisa kuonesha matamshi yako ni tofauti kabisa na kimombo halisi...
Kimombo halisi ni kipi mkuu? Uzuri/ubaya ni kwamba kwa sasa Kiingereza tunaweza kusema kuwa ni lugha "isiyo na mwenyewe" kwa sababu kila mmoja ana lafudhi yake haijalishi kama lafudhi yenyewe inatambuliwa kuwa ndiyo rasmi ama la! Ni wazi kuwa viingereza rasmi vya Uingereza, Marekani, Australia, New Zealand, Afrika Kusini, India, huku kwetu Afrika Mashariki, Wanigeria kule na kwingineko ni tofauti mno na pengine hakuna haja ya kuchekana. Kinachotatanisha kwetu sisi ni hii sera yetu ya ajabu ya elimu ya kufundishia ambayo inamwacha mtoto njia panda akiwa siyo mbobezi wa Kiswahili au Kiingereza.

Roommate wangu huko kwa Trump alikuwa Mchina na alikuwa anasoma Nuclear Physics. Kiingereza chake kilikuwa hopeless kabisa lakini makabati yake yalikuwa yamejaa mavitabu manene ya Kichina na alikuwa anahangaika nayo usiku kucha. Mwenzangu huyu ingawa Kiingereza chake kilikuwa cha shida lakini angalau alikuwa na marejeo ya masomo yake katika lugha ya mama anayoielewa vizuri. Sisi masikini Kiingereza ndo hivyo na huna mahali pa kukimbilia mtu inabidi ukomae tu ikibidi kukariri unakariri ili mambo yaende. Ndiyo maana elimu yetu haina manufaa sana kwa sababu kuna mpishano mkubwa kati ya maarifa na lugha ambayo kupitia kwayo maarifa hayo yanatufikia. Tunajidhulumu na kujidogosha wenyewe!
 
Experience yangu ni opposite. Mara ya kwanza nimetia mguu kwa Trump najitambulisha darasani hakuna mtu ananielewa utafikiri naongea Kisukuma. Nikajaribu kuongea pole pole ndiyo njemba zinaniuliza "You are from Taiwan?" Nikaitamka Tanzania kwa uangalifu jamaa hazielewi basi nikaamua kutumia mifano ya Mlima Kilimanjaro na Serengeti + "Hakuna Matata" kuwa ni Kiswahili na ni lugha yetu ya Tanzania ndo nikaona vichwa vinatikiswa. Kuingia darasani Prof mmoja mashuhuri sana wa Economics aisee simwelewi kabisa. Lafudhi yao ajabu ajabu. Jioni hiyo binti mmoja Mzungu akaja kuniongelesha basi nikamganda nikamwambia awe ananisemesha mara kwa mara ili nizoee lafudhi yao. Miezi sita ya mwanzo was hell mpaka nilitamani kupanda ndege kurudi Misungwi. Mpaka leo huwa naamini kwamba siye tuko majiniazi aisee kwani kuweza kusoma na kufaulu kwa lugha ambayo hatuielewi sawasawa (Kiingereza) siyo kazi rahisi jamani.

Kukariri sio ugeneous..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom