Kimeeleweka Dulla Mbabe vs Twaha Kiduku 2

Safi sana Twaha Kiduku umemkalisha mpuuzi huyo misifa miingi. Ila fanyia kazi pumzi ungekua na pumzi imara Dulla angekaa kwenye raundi za katikati pale.

Kinacho mshinda kiduku ni combinations yaani hili pambano dula round ya tano lilikuwa KO endapo kiduku angekuwa na combination za ngumi
 
Kiduku yuko vizuri ila Dulla mbabe naye si wa kumpuuzi pamoja na ngumu zote za usoni bado yupo tu kama Kenge anayepigwa mawe
 
Twaha Kiduku ana ndonga nzito kuliko Dulla mbabe , ila wafuate ushauri wa Mwakinyo watafute mapambano mengi ya nje .
Twaha Kiduku akijifua zaidi hasa akiboresha shabaha na balance za miguu , ndonga zake ni hatari sana .
Dullah Mbabe ameshindwa kutumia advantage aliyokuwa nayo;
1. Ni mrefu ambao ungemsaidia kumshushia makonde mpinzani wake kirahisi lakini alishindwa , Kiduku alitumia mbinu ya kuinama sana na kuinuka kwa ghafla na kumchangabya mbabe Dulla , Dulla akajikuta anajichekea hajui afanye nini.
2.Urefu wake unaenda na urefu wa mikono yake ambayo ilijidhihirisha ni ronyo ronyo pamoja na kupata reach nyingi usoni kwa Kiduku lakini hazikuwa na madhara kwa Kiduku.
3.Dullah anaonyesha kurudhika sana wakati kimataifa hajulikani
Kifupi Dulla mbabe namshauri aangalie sana mapambano ya Lenox Lewis akajifunze jinsi ya kutumia vizuri urefu wa mwili na mikono , na Twaha Kiduku akaangalie mapambano ya Mike Tyson alipokiwa moto maana uchezezaji wake na kimo kama wanafanana itamsaidia hasa katika mapambano makubwa ya kimataifa , mwenzao Mwakinyo kajiwekea malengo kila baada ya miezi 3 anapigana pambano la kimataifa na imeonyesha kumsaidia na kumjenga.
 
Back
Top Bottom