Kimbunga Kenneth Kuikumba Tanzania

Habari za hivi punde :

24 Apr 2019
TMA yatoa tahadhari ya kimbunga Kenneth kasi ya kilometa 80 kwa saa kinaweza kuikumba Tanzania katika eneo la Pwani ya Mashariki na uwezekano wa mafaa haya kutokea :
  1. Mafuriko makubwa ya kina kirefu
  2. Upepo mkali kuezua mapaa ya nyumba
  3. Miundo mbinu ya usafiri kuharibiwa
  4. Mashamba na mazao kuharibiwa
  5. Miundo mbinu ya usambazaji umeme kukatika na kutishia maisha
  6. Vyombo vya usafiri wa baharini kuharibiwa
  7. Usafiri wa anga kusitishwa


Source : EastAfricatelevision
 
Pamoja na kitisho cha kimbunga Kenneth kwa wananchi wake sijaona popote Rais Magufuli akiungana na wananchi wake kwa maandalizi ya kuupokea ugeni korofi.

Akiongea tukingali hai huku Namatumbusi mtufikishie alichosema (sijui kama viredio vitapona kulowa na mvua)

Makaratasi ya kumbukumbu za korosho ndio basi tena!!

So Long.
 
Ameshaongea huko Malawi HAPA KAZI TUU means only Work... kwani Kimbunga kakileta yeye not more than two days

Wonders never end
 
Hahaaa

Utamskia

"Ndugu zanguu.....(huku akirekebisha mawani yake) naomba tujifunze kuwa wazarendo...

(Huku kakunja sura) hivi ni nani aliekipa jina la Kenneth hiki kimbunga chetu....?? (Huku akiangalia huku na huko akisubiri yeyote ajitokeze) hakuna...??, mkuu wa mkoa wa Mtwara ni nani ameruhusu hiki kimbunga kiitwe Kennneth....?? (Huku mkuu wa mkoa akiwa amehamaki hajui cha kujibu) sasa nakutumbua kuanzia leo ww sio mkuu wa mkoa wa mtwara.

Ndugu zangu tujifunze kuwa WAZALENDOO hiki kimbunga ni cha kwetu sote sisi watanzania ni mali yetu sisi watanzania sasa sioni sababu ya kukipa jina la kidhungu, mngekipa hata jina la wenzetu wa kusini kulee ili japo na sisi itutangaze kimataifaa

Mamlaka ya hali ya hewa MMENISIKITISHA SANA KWA HILI, mkurugenzi kwa hili nakupa masaa sita ujitathmini kama unafaa kuendelea na hiyo nafasi yakoo..

Na naamuru kuanzia sasa hiki kimbunga kiitwe "MWAKITOPILE" full stop. Na nitalikabidhi jeshi likilinde na kuhakikisha kinapita mikoa yote ya kusini bila kupingwa..... na ikiwezekana na kule kwangu kifike maana kitatusaidia kututangaza kimataifaa
 
"Oniry weki" Yaan not than a day msikilizeni angejua jinsi hilo sauti lake lilivo baya khaaa.............
Yaani ile hotuba imemtoa kwenye reli! Muda huu ni hallucinations mpaka anasahau kuwatakia wananchi wake ukakamavu na nusura ya Mwenyezi Mungu kuelekea ziara ya mkorofi "kenneth" (kimbunga)
 
Yaani ile hotuba imemtoa kwenye reli! Muda huu ni hallucinations mpaka anasahau kuwatakia wananchi wake ukakamavu na nusura ya Mwenyezi Mungu kuelekea ziara ya mkorofi "kenneth" (kimbunga)


Huyu wala hana habari kama anaongoza binadamu kabisa wanaohitaji busara na hekima... Nawaambieni refer kule Bukoba kwenye lile tetemeko refer mssada uliopelekwa nchi jirani waliopatwa na natural disaster km Tanzania refer kweli huwa hajui kama anaongoza binadamu wenye uelewa kuliko yeye. si sio rahisi akumbuke vitu kama hivyo
 
Huyu wala hana habari kama anaongoza binadamu kabisa wanaohitaji busara na hekima... Nawaambieni refer kule Bukoba kwenye lile tetemeko refer mssada uliopelekwa nchi jirani waliopatwa na natural disaster km Tanzania refer kweli huwa hajui kama anaongoza binadamu wenye uelewa kuliko yeye. si sio rahisi akumbuke vitu kama hivyo
Inasikitisha kwa kweli
 
Kipige tu uli tuone uwezo wetu wa kukabiliana na majanga makubwa makubwa! @TanzaAid
 
April 25, 2019
Wavuvi wahoji taarifa za Mamlaka za hali ya hewa Tanzania TMA kuhusu kimbunga Kenneth
 
25 Apr 2019
Wakazi wa baadhi ya maeneo mkoani Mtwara wameendelea kuyahama makazi yao, baada ya kuwepo kwa tahadhari ya kuwepo kwa kimbunga kikubwa cha Keneth katika maeneo hayo.
 
Up dates
April 25, 2019
Za hivi punde siku ya alhamisi mwendo wa saa saba mchana taarifa ya hali ya Kimbunga Kenneth kilichopo nje baharini kilometa 150 toka pwani ya kusini mwa Tanzania
 
25 Apr 2019
Kimbunga chaongezeka nguvu sana kufikia hatua ya kuwa na 'Jicho' - The Eye of the Storm :

Taarifa ya mwenendo wa Kimbunga "Kenneth" katika bahari ya Hindi tarehe 25-04-2019 Mchana na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini kama inavyowasilishwa na Dkt Agness Kijazi, Mkurugenzi Mkuu - Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)

Source : Meteo Tanzania
 
April 25, 2019
HABARI ZA SAA, SAA SABA NA DAKIKA 55...APRILI 25, 2019



Source : Capitaltvtz
 
April 25, 2019

Mwenendo , Kasi , Umbali toka Pwani ,mwelekeo Kimbunga Kenneth

Mwenendo kwa kimbunga Kenneth kuelekea siku ya Ijumaa kesho tarehe 26 April 2019 katika bahari ya Hindi kusini mashariki mwa Afrika maeneo ya visiwa vya Reunion, Comoros, kisiwa cha Mafia Tanzania, pwani za Mtwara Tanzania na Pemba Mozambique.

Source: Meteo Tanzania
 
April 2019
Hivi punde taarifa ya TMA

Kimbunga Kenneth kuelekea muda wa usiku wa manane kuamkia tarehe 26 April 2019 maeneo ya mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma nchini Tanzania

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom