Kimbunga JOBO kimepita, lakini je, serikali na wananchi tunajiandae kwa vimbunga vijavyo?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Historia inatuonyesha mara ya mwisho kimbunga kilichowahi kuikumba nchi yetu kilitokea mwaka 1952(miaka 69 iliyopita).Hii maana yake vimbunga kama hivi bado vinaweza kuja kutukumba tena huko mbeleni.

Vimbunga vinavyoendelea kutokea miaka hii ya karibuni kikiwemo hiki cha JOBO kilichotokea siku chache zilizopita, ni ushahidi kuwa vimbunga bado vitaendelea kutokea na hivyo kuna hatari kimbunga kimojawapo huko mbeleni kitakuja kutukumba na kuleta madhara.

Vimbunga husababisha upepo mkali, upepo unaoweza kunangusha miti, kuezua mapaa ya nyumba, kung'o nguzo za umeme, kuharibu miundombinu ya mawasikiano, n.k

Vile vile vimbunga husababisha phenomenon inayojulikana kama storm surge ambayo ni mawimbi yanayotokana na kuongezeka kwa kina cha maji baharini kunakosababishwa na kimbunga. Mawimbi haya yanayoweza kufikia mpaka urefu wa mita 6, yanaweza kuingia nchi kavu na kufunika eneo kubwa la nchi na kusababisha madhara makubwa.

Vimbunga hivi pia huweza Kuleta au kusababisha mvua kubwa inayoweza kuleta mafuriko makubwa, mafuriko yanaweza kusababisha hasara kubwa kama vile upotevu wa mali pamoja na maisha ya watu na wanyama.

Kwa kifupi, vimbunga hivi vya baharini ( cyclones) ni very devastating kiasi kwamba kwa nchi zetu hizi masikini tunaweza kujikuta tunachukua muda mrefu kurekebisha madhara yatokanayo na vimbunga hivi (kurejesha mawasiliano, n.k hasa tunapokuwa hatujajiandaa.

Ni ukweli ulio wazi kuwa hatuwezi zuia vimbunga hivi kutokea bali tunachoweza kufanya ni kuchukua hatua au tahadhari zinazoweza kusaidia kupunguza madhara ya hivi vimbunga iwapo vitajitokeza.

Binafsi najiuliza, sisi wananchi na hasa serikali, imejipanga vipi kukabiliana na madhara ya vimbunga hivi iwapo yatatokea?

Kwa mfano, serikali imejiandaa vipi kutoa huduma za dharuea za uokoaji baharini na nchi kavu endapo majanga haya yatatufika?

Ni kwa kiasi gani serikali inaimarisha taasisi zake zinazohusika na majanga kama haya?

Kwa mfano,serikali inajipanga vipi kuiongezea uwezo taasi yake ya Mamlaka ya Hali ya Hewa katika kukabiliana na utoaji wa taarifa za majanga haya kwa maana ya kuipatia vifaa bora na vya kisiasa zaidi pamoja na rasilimali watu(wataalamu)?

Inafahamika kuwa serikali inajitahidi kuiwezesha taasisi yake hii kwa kuipatia vifaa na wataalamu..Lakini je, huu si wakati wa serikali kuongeza maradufu ushiriki wake katika kuisaidia taasisi yake hii?

Je,serikali haioni umuhimu wa kuja na sera au sher inayoweza kutoa incetive kwa watu kujenga majengo yanayoweza kupunguza madhara ya vimbunga katika maeneo hasa ya Pwani mfano kuachana na ujenzi wa majengo kwa kutumia matofali na badala yake kutumia material mbadala yanayoweza kupunguza damage ya vimbunga?

Kwa ujumla, mambo ya kutazama ni mengi. Swali ni je, tunachukua tahadhari gani kupunguza madhara ya vimbunga hivi iwapo vitatokea huko mbeleni au kimbunga kimoja kikipita na sisi ndio tunasahau?

Iko siku tunaweza kuja kujiulaumu na kusema tungejua tungefanya hivi au vile madhara yasingekuwa makubwa kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom