kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,686
"Kwa muda mrefu tulikuwa hatujatangaza kima cha chini cha mshahara, lakini nafurahi kuwajulisha tu kwamba mwezi ujao tutatangaza rasmi,"alisema Kabaka.
Dar es Salaam. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amesema mwezi ujao wanatarajia kutangaza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa sekta zote.
Akizungumza jana wakati wa mkutano kuhusu sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), alisema kwa muda mrefukiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa sekta zote kilikuwa hakijabadilishwa.

Pia alitahadharisha kuhusu utitiri wa vyama katika sehemu moja ya kazi kushauri waajiri wasiruhusu wafanyakaziwaanzishe kwa sababu vitakosa nguvu ya kujadiliana na mwajiri katika kufunga mikatabaya hiyari .
Waziri huyo alisema sekta ya hifadhi ya jamii ina idadi ndogo ya wanachama waliojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ukilinganisha na idadi ya nguvu kazi iliyopo ambayo ni milioni 22.
Awali Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Irene Isaka alisemahadi sasa michango katika mifuko hiyo imefikia Sh 1.4 trilioni nakwamba mafao yanayolipwa yamepandakutoka Sh500 bilioni hadi kufikia Sh 724 bilioni.
CHANZO: MWANANCHI