Kima cha chini cha mshahara kuwa 180,000/= | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kima cha chini cha mshahara kuwa 180,000/=

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dosama, May 9, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Source meananchi

  NI BAADA YA MAJADILIANO YA SERIKALI NA TUCTA
  Waandishi Wetu
  KUNA taarifa kwamba Serikali imekubali kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma kwa kati ya asilimia 20 na 33.3 katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13.Hatua hiyo inamaanisha kwamba kima cha chini cha mshahara sasa kitakuwa kati ya Sh180,000 hadi Sh200,000 kutoka Sh150,000 zinazolipwa sasa.Vyanzo vya habari kutoka serikalini vimeeleza kwamba nyongeza hiyo ya kati ya Sh30,000 hadi Sh50,000 ni matokeo ya mazungumzo kati ya Serikali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta).Mbali ya kutaja kima hicho, vyanzo hivyo vimeeleza kuwa nyongeza hiyo inaweza kuvuka Sh50,000 kutegemea uwezo wa Serikali.

  Hata hivyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), George Yambesi alipoulizwa kuhusiana na taarifa hiyo alijibu kwa kifupi kuwa hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia hilo.

  “Sipo katika ‘position’ (nafasi) nzuri ya kuzungumzia hilo, nadhani suala la mishahara. Mheshimiwa Rais alishalizungumzia kwenye hotuba yake ya Sikukuu ya Wafanyakazi,” alisema.

  Katika hotuba yake kwenye kilele cha sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Rais Jakaya Kikwete alisema Serikali inatambua mazingira magumu ya kazi waliyonayo wafanyakazi na kwamba ipo tayari kuyaboresha.

  Alisema imesikia madai ya wafanyakazi na itaendelea kuyafanyia kazi. Madai aliyoahidi kuyafanyia kazi ni pamoja na kupunguziwa kodi ya mapato.

  Kwa upande wa Tucta, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Nicolaus Mgaya alipoulizwa jana alisema hajui Serikali itaongeza mshahara kwa kiasi gani lakini akasema anaamini kuwa ni sikivu.

  Alisema kwa miaka mingi wafanyakazi wamekuwa wakilalamikia mishahara midogo ambayo haikidhi mahitaji, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa migongano ya hapa na pale na Serikali akasema kutokana na hali hiyo, wanaamini kuwa wataongezewa.

  “Tunaamini linaweza kutekelezeka (suala la kuongezewa mishahara), lakini hakuna anayejua nyongeza hiyo itakuwa ni kiasi gani, kwa hiyo ukinitajia kiwango nashindwa kuelewa umekitoa wapi,” alisema Mgaya alipoulizwa kama nyongeza hiyo ni kati ya Sh30,000 na 50,000.

  Mgaya alisema mbali na kuomba nyongeza mshahara, Tucta pia imeiomba Serikali kupunguza gharama za tozo za mifuko ya hifadhi ya jamii huku ikienda pamoja na udhibiti wa mfumuko wa bei ambao umekuwa kikwazo kwa wafanyakazi na kuwafanya kuishi katika mazingira magumu kiasi cha kushindwa kujituma ipasavyo na wengine kukimbilia kwenye sekta binafsi.

  “Wafanyakazi ni tabaka kubwa, lakini limesahaulika. Hii inatokana na Serikali kushindwa kusikiliza kilio chao cha kuwaongezea mishahara jambo ambalo limechangia kulipwa ujira mdogo na kusababisha wengi wao kukimbilia kwenye sekta binafsi, kutokana na hali hiyo tunaamini kuwa Serikali itasikilia kilio chetu,” alisema.

  Madai ya wafanyakazi

  Sakata la mshahara wa wafanyakazi liliibua mgogoro mkubwa baina ya Serikali na Tucta na mwaka 2010, Shirikisho hilo liligoma kumwalika Rais Kikwete kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa kama ilivyokuwa utamaduni wake.

  Hatua hiyo ya Tucta ilitokana na kile lilichodai kuwa Serikali siyo sikivu na lilitumia siku hiyo kujadili na kutoa tamko la kuitaka kutangaza kima kipya cha mshahara cha Sh315,000 ndani ya siku mbili la sivyo wafanyakazi wa umma wangeingia katika mgomo nchi nzima.

  Hatua hiyo ilimlazimu Rais Kikwete kuitisha mkutano na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Mei 3, 2010 na kujibu hoja mbalimbali za Tucta na kuweka msimamo wa Serikali kuwa haiwezi kulipa kiasi hicho cha fedha.

  Rais Kikwete aliwatuhumu viongozi wa Tucta kuwa ni waongo na kwamba walikuwa hawasemi ukweli juu ya kile walichokuwa wanabaliana katika vikao vyake na Serikali.

  Alisema Serikali ikifanya kima cha chini kuwa Sh300,000 kwa watumishi wa umma, itabidi iwalipe Sh6.9 trilioni kwa mwaka wakati makadirio ya makusanyo ya mapato ya Serikali kwa mwaka 2010/11 ni Sh5.8 trilioni.
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mambo ya aibu sana haya, baada ya kuwa madarakani kwa miaka 7 bado kuna watu wanalipwa laki na hamsini elfu nchi hii? Maisha bora tuliyoambiwa ndiyo hayo? Hovyo kabisa!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  They can't be serious!!! 30k??? Iklimwa kodi hyo si unabaki na 24k? Mchele kilo 3000/=!! Wafanyakazi msifanye makosa 2015,kima cha chini 2015 ni 415,000/= chini ya serikali ya CDM,chagua cdm chagua Dr slaa!
   
 4. K

  Katufu JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 433
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Kwa hali hii kweli huyo atatulia na kufanya kazi kwa moyo kweli?
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kama serikali itashindwa kuthibiti mfumuko wa bei sioni sababu ya kupandisha mishahara.
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,055
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Hapa ishu si kupandisha mishahara bana,tunataka ashushe mfumko wa bei ili kama ni 10,000 irudie thamani yake ya awali kwamba ukimpatia hata mdogo wako shule anaitumia term nzima na si kwa siku 2 imekwisha ama mchele ushuke mpaka sh700/=kg na unga wa kula uhuzwe sh400/=kg tofauti na ilivyo sahivi mchele 3,000 ingali unga ni 1,500

  Nafikiri serikali ipunguze kodi za mafuta ya nishati pamoja na vifaa vya usafirishaji,lakini pia serikali iandae mpango wa kurasimisha shughuri ndogondogo kama bodaboda ili navyo vilipe kodi kama tax bila kuwasahau wasukuma maguta na machinga ili makusanyo yaweze kwendana na mahitaji halisi ukizingatia pande hizi kuna pesa nyingi bado haikusanywi kabisa

  Tuna vyanzo vingi vya mapato endapo tukiwa makini kuliko kuongeza mishahara mwisho wa mwezi mfuko umejaa noti ambazo zinaishia kununua mchicha na chinese peke yake
   
 7. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  sasa kwa 180,000 mtz na familia yake ndio ale hapo, atibiwe, apeleke watoto shule, alipe kodi ya nyumba!!!! na huu mfumuko wa bei!!! they must be kidding
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,055
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Hapa ishu si kupandisha mishahara bana,tunataka ashushe mfumko wa bei ili kama ni 10,000 irudie thamani yake ya awali kwamba ukimpatia hata mdogo wako shule anaitumia term nzima na si kwa siku 2 imekwisha ama mchele ushuke mpaka sh700/=kg na unga wa kula uhuzwe sh400/=kg tofauti na ilivyo sahivi mchele 3,000 ingali unga ni 1,500

  Nafikiri serikali ipunguze kodi za mafuta ya nishati pamoja na vifaa vya usafirishaji,lakini pia serikali iandae mpango wa kurasimisha shughuri ndogondogo kama bodaboda ili navyo vilipe kodi kama tax bila kuwasahau wasukuma maguta na machinga ili makusanyo yaweze kwendana na mahitaji halisi ukizingatia pande hizi kuna pesa nyingi bado haikusanywi kabisa

  Tuna vyanzo vingi vya mapato endapo tukiwa makini kuliko kuongeza mishahara mwisho wa mwezi mfuko umejaa noti ambazo zinaishia kununua mchicha na chinese peke yake
   
 9. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ni bora uwe dereva wa bodaboda kuliko kulipwa 180000
   
 10. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ziuzwe mali za anasa za serikari, pesa itapatikana. Na wezi wote wachukuliwe hatua ili pesa irudi serikarini.
   
 11. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  180,000? hata budget yangu ya bia kwa wiki mbili inazidi wataishije hawa watu?
   
 12. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  dereva wa bodax2 wanapiga zaidi ya hizo
   
 13. o

  oakwilini Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sh 180000 ni wastani wa sh 6000 kwa siku ambazo kwa matumizi ya mtu mmoja hivi leo hazitoshi,wamfikirie mwenye watoto wanne na mke ambaye hana ajira will they survive?mbona baba mwanaasha analipwa mil 20.000,000?Is not fair.
   
 14. Zuia Sayayi

  Zuia Sayayi JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 834
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mchoma chipsi mjanja alie ajiliwa huwa ananunua mayayi yake ya ziada ambayo yako nje na hesabu ya bosi na kuyapa kipaumbele yake kuya anzia kuka_anga kwa viazi vya bosi wake na hvyo kujitengenezea c chini Tsh. 5000/= per day
  (5000*30= Tsh.150,000/=) per mnth
   
 15. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ccm hiyo ndiyo mtetezi wa wakulima na wafanyakazi kauli za nape nauye...............
   
 16. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,477
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kua wale waliopewa dhamana ya kulifanyia kazi hili wanaishi kama wako peponi, katika hali kama hiyo inakua vigumu kuwafikiria wenzao. Hivi kwa maisha ya sasa 180,000/= inaweza kumsaidia mtu kweli?
   
 17. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,537
  Likes Received: 10,458
  Trophy Points: 280
  ni wafanyakaza wa ngazi ipi wanaolipwa 150,000 kwa mwezi.???
   
 18. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kama kima cha chini cha msharaha kwa mfanyakazi ni 180,000/= na kwa kuwa kila Mtanzania aliyehai anadaiwa 350,000/= sasa sijui deni hili litalipwaje.....
   
 19. S

  Shansila Senior Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I dont see anything new here,kima cha chini kinatakiwa kuwa around laki 5.Sasa hii laki na themanini ya Mgaya,Ayoub Jumaa na JK cjui wamepata wapi reference kuwa inaweza ikakidhi japo kwa matumizi ya chini sana.Sioni ishu hapa,tuendelee tu na harakati za ukombozi.
   
 20. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hujakosea kabisa baba collin,coz pale border Tunduma,dereva wa bajaj anapeleka laki 9 kwa mwezi kwa tajiri and simultaneously naye ana uwezo wa ku-make laki 8 mpaka milioni kwa mwezi.
   
Loading...