Hapa kifutu ndio huwa ananiacha hoi sana.Sipingi yeye kuwa kiongozi ila napinga sera zake za kikomunisti ambazo zimepitwa na wakati japo Vietnam nayo ni ya kikomunisti ila sera zao za kisasa.
Huyu dogo angebadirisha hizo sera zake za kiimla sasa hivi nchi yake ingekuwa mbali sana kiuchumi au kuwa sawa na ndugu zao wa kusini.
Unachokisema kwa upande mmoja ni sawa lakini kwa upande mwingine sio sawa.
1:Korea Kaskazini wanaamini katika uimara/ubora wa jeshi na ndicho walichokifanya tangu enzi za mababu zao.
2:Korea Kaskazini sio kwamba hawana mpango wa kuboresha uchumi wao kwa kiwango kikubwa na chakutishia Mataifa mengine, Kim Regime wameanza na nguvu za kijeshi ili isiwe rahisi kuvamiwa na Mataifa ya Mabepali yanayofahamika kwa ulaghai na unafiki wa kisiasa kwa kupandikiza vibaraka watakao shirikiana nao katika kuvunja uchumi wa kitaifa na kuanzisha uchumi wa Kibepari ambapo wachache ndiyo watakao nufaika. Na mbaya zaidi ukishashirikiana na hawa jamaa(Mabepali) watakupelekesha kama wanavyotaka.
3:Korea Kaskazini mpaka sasa mpango wao kwenye nguvu za kijeshi wameisha kamilika kwa kiasi kikubwa sana, naamini kabisa kitu kinachofatia ni kuimarisha, kuboresha na kujikita kwenye uchumi shindani.
4:Korea Kaskazini kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa ubora wa Kijeshi kuna Mataifa Makubwa yamepigwa na mshangao wakustajabisha na ni aibu kwao, walichokifanya ni kukimbilia kwenye vikwazo vya kiuchumi kwasababu wanafahamu Kim Regime baada ya kufanikiwa KIJESHI inaelekea kwenye kuimarisha uchumi wake.
5:Kwa maoni yangu hakuna haja ya Korea Kaskazini kubadirisha Sera zao, ila mataifa ya kimaghalibi hasa Marekani inabidi ibadirishe Sera zake za kimataifa ili na Mataifa mengine yawe huru ili yajijenge na kujitegemea. Korea Kaskazini imetumia fedha nyingi sana kulijenga na kuliimarisha jeshi, sio kwamba wanapenda kuimarisha jeshi afu uchumi uwe mbovu, ila imewaladhimu kuanza na Jeshi kwanza ili mijizi ya kimataifa isilete hujuma potoshaji kwenye nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii na hata kama ikitokea mijizi ya kimataifa imepenyeza figisu dhidi ya taifa lao basi inakuwa rahisi kujibu mapigo kwa namna yoyote ile hata kama ni kwa ubabe kama unahitajika.