Kilwa Masoko, Lindi: Zaidi ya Tani moja ya Dawa za Kulevya yakamatwa

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,901
14,368
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na kikosi cha wana maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamekamata zaidi ya tani mbili ya dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kazi iendelee,naona wauza unga wanajaribu kupima upepo,pongezi kwa serikali ya awamu ya sita

======

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na kikosi cha wanamaji cha JWTZ imewakamata watu saba wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zaidi ya tani moja kwa kutumia jahazi. Dawa hizo zimekamtwa eneo la Kilwa Masoko mkoani Lindi.

20210424_180557.jpg
20210424_180600.jpg
20210424_180603.jpg
 
Baada ya Mzee Magu kuondoka sasa watu wameamua kufanya dhihaka na zarau. Tani 2 kweli ndugu zangu?

Enzi za Magu watu kama hawa wangepotea wasijulikane wamepotelea wapi.

Wauza pembe za ndovu walipotea wengine walikimbia nchi. Ukikamatwa mbugani unahojiwa mtandao wako ukoje kisha unapotea na mtandao wako unapotea kuokoa tembo wetu.

Sasa Magufuli hayupo sijui kama tembo wetu watapona, sasa twiga watapakiwa kwenye guta ama majaji mchana kweupe badala ya ndege.

Wauza madawa ya kulevya watarudi kwa nguvu kubwa, zile njozi za viatu zitaanza kuning'inia kwenye nguzo za umeme muda si mrefu kuonyesha location ya wauza madawa ya kulevya.
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na kikosi cha wana maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamekamata zaidi ya tani mbili ya dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kazi iendelee,naona wauza unga wanajaribu kupima upepo,pongezi kwa serikali ya awamu ya sita

View attachment 1762568View attachment 1762569
Kudadadeki haaaaaaaaa.Huu mzigo aliye uagiza si mtu mdogo kama ikiwezekana waminywe hao wapuuzi wawataje.
 
Back
Top Bottom