Kama nilivyowaeleza jana kuwa DC wa kilolo bw.Gerald Guninita amemweka ndani mwenyekiti wa kijiji cha udekwa (CHADEMA) bila kosa,lakini madai yake DC yalikuwa ni mwenyekiti huyo kurekodi mazungumzo ya kikao hicho cha DC kwa njia ya simu.Ukitafakari hapa huwezi ona kosa kwani mara nyingi tunavyohudhuria vikao vya serikali huwa tunakuwa na notebook kwaajili ya kuchukua notes za kumbukumbu,hivyo basi nimfahamishe ndugu Dc kwamba kurekodi sauti kwa njia yeyote ile ni njia ya kuhifadhi kumbukumbu kama ilivyo kwa maandishi.
Lakini cha kushangaza leo asubuhi amerudia kauli yake wakati akihojiwa na kituo cha redio cha ebony fm kwamba, amemkamata mwenyekiti huyo kwa kosa la kurekodi kikao chake kwa njia ya simu, huku akisisitiza kwamba hairuhusiwi kurekodi mazungumzo ya DC,akaongeza kuwa anatarajia kumfikisha mahakamani mwenyekiti huyo kwa kosa hilo.Jambo hili limeacha maswali mengi kwa wasikilizaji,je? ni kosa kwa kiongozi wa serikali ya kijiji kurekodi mazungumzo yanayofanyikia ofisini kwake na hususani yale yanayomhusu yeye mwenyewe,je wanaoandika nao wana makosa? na kama hawana kuna tofauti gani kati ya anayerekodi na anayeandika ikizingatiwa kuwa wote wanatunza kumbukumbu za msemaji mmoja.
Hata hivyo vijana wa CHADEMA waliofika kumwekea dhamana ndg,Obadia Lubugo mwenyekiti wa kijiji wameshangazwa pale walipouliza shitaka la mtuhumiwa wakaambiwa na polisi shitaka lake liko kwenye uchunguzi ili hali simu yake alinyang'anywa tangu jana na DC, baadaye wakakabidiwa polisi, hata hivyo amepewa dhamana na ameambiwa aripoti kesho asubuhi kituoni mbigili huku simu yake ikibakia mikononi mwa polisi. Swali hapa ni kwamba kwanini shitaka lake halijajulikana ili hali jana aliambiwa kosa lake ni kurekodi kikao cha DC?