KILOLO: DC Guninita amweka Lock up Mwenyekiti wa Kijiji bila sababu!

Nimetafuta / search maneno "mkuu wa wilaya" na "mkuu wa mkoa" ktk rasimu ya katiba mpya .... sikupata chochote.
Hii ina maana kuwa hawa watu hawamo tena na wala hawatatambulika tena kikatiba? kAMA NDIO HIVYO, THEN GOOD RIDDANCE !!!
 
Huyu Gerald amefikia hatua ya kuwa na akili za matope kuzidi babake! Kweli chura huzaa nyoka kha!
Ukombozi wa Nchii umekaribia!
 
Nimetafuta / search maneno "mkuu wa wilaya" na "mkuu wa mkoa" ktk rasimu ya katiba mpya .... sikupata chochote.
Hii ina maana kuwa hawa watu hawamo tena na wala hawatatambulika tena kikatiba? kAMA NDIO HIVYO, THEN GOOD RIDDANCE !!!

Mzee Warioba alisema katiba za nchi husika (Tanganyika na Zanzibar) ndo zitakazoamua iwapo hao wakuu wa wilaya na mikoa waendelee kuwepo au la.
 
bado wanazidisha hacra kwa wananchi, huku kwetu mbunge wa jimbo letu vijana hawataki hata kumuona, uonevu umezidi sana jamani.
 
Magamba kama huyu tutayatia adabu yote, tumemtoa m.Kiti wetu wa udekwa leo asubuhi na kesho wakati wa kwenda kuripoti asubuhi tutakwenda kumfungulia kesi ya kumdhalilisha kamanda wetu.
 
Kama nilivyowaeleza jana kuwa DC wa kilolo bw.Gerald Guninita amemweka ndani mwenyekiti wa kijiji cha udekwa (CHADEMA) bila kosa,lakini madai yake DC yalikuwa ni mwenyekiti huyo kurekodi mazungumzo ya kikao hicho cha DC kwa njia ya simu.Ukitafakari hapa huwezi ona kosa kwani mara nyingi tunavyohudhuria vikao vya serikali huwa tunakuwa na notebook kwaajili ya kuchukua notes za kumbukumbu,hivyo basi nimfahamishe ndugu Dc kwamba kurekodi sauti kwa njia yeyote ile ni njia ya kuhifadhi kumbukumbu kama ilivyo kwa maandishi.

Lakini cha kushangaza leo asubuhi amerudia kauli yake wakati akihojiwa na kituo cha redio cha ebony fm kwamba, amemkamata mwenyekiti huyo kwa kosa la kurekodi kikao chake kwa njia ya simu, huku akisisitiza kwamba hairuhusiwi kurekodi mazungumzo ya DC,akaongeza kuwa anatarajia kumfikisha mahakamani mwenyekiti huyo kwa kosa hilo.Jambo hili limeacha maswali mengi kwa wasikilizaji,je? ni kosa kwa kiongozi wa serikali ya kijiji kurekodi mazungumzo yanayofanyikia ofisini kwake na hususani yale yanayomhusu yeye mwenyewe,je wanaoandika nao wana makosa? na kama hawana kuna tofauti gani kati ya anayerekodi na anayeandika ikizingatiwa kuwa wote wanatunza kumbukumbu za msemaji mmoja.

Hata hivyo vijana wa CHADEMA waliofika kumwekea dhamana ndg,Obadia Lubugo mwenyekiti wa kijiji wameshangazwa pale walipouliza shitaka la mtuhumiwa wakaambiwa na polisi shitaka lake liko kwenye uchunguzi ili hali simu yake alinyang'anywa tangu jana na DC, baadaye wakakabidiwa polisi, hata hivyo amepewa dhamana na ameambiwa aripoti kesho asubuhi kituoni mbigili huku simu yake ikibakia mikononi mwa polisi. Swali hapa ni kwamba kwanini shitaka lake halijajulikana ili hali jana aliambiwa kosa lake ni kurekodi kikao cha DC?
 
Ni muhimu wakati huu kufikiria kwa kina kazi na manufaa ya wakuu wa wilaya ili haya yote tuyatatue! Wakuu wa wilaya ni zaidi ya miungu watu,wanawanyanyasa wananchi over and above,ebu tutoe waliokwenye mabaraza ya katiba watoe maoni ya maana juu ya hawa watu.
 
Matukio kama haya yananitia uchungu wa kufanya chochote chenye manufaa kwa taifa langu. Hakuna aliyejuu ya haki ya mtanzania yeyote kwa njia yoyote ile. Tunaweza kuendelea na ukondoo wetu, lakini Mungu hawezi ruhusu tuonewe na kondoo wenzetu.

huyu sialishawahi kufukuzwa kama sio kusimamishwa kwenye huo mchama anaoupigania miaka ya 90?mbona amejisahau mapema hivyo?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom