KILOLO: DC Guninita amweka Lock up Mwenyekiti wa Kijiji bila sababu!

Mbunge wa ilula

JF-Expert Member
Jun 3, 2012
211
195
Ni katika kuendeleza ubabe wake na ulevi wa madaraka DC wa kilolo bw.Gerald John Guninita amemweka rock up ya mbigili police station mwenyekiti wa kijiji cha udekwa bila sababu ya msingi.

DC huyu alifika kijijini hapo kwaajili ya kuendesha mkutano wa kumng'oa mwenyekiti huyo wa kijiji (CHADEMA) ambapo fununu zilishavuja siku chache kuwa ujio wake utakuwa maalumu kwaajili ya kuja kumng'oa mwenyekiti huyu ambaye hana hatia yoyote zaidi ya kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Lakini gafla alibadilisha mkutano na kuwa kikao cha ndani hali iliyowashangaza wengi na wakiwa ndani ya kikao alimuuliza mwenyekiti huyo kwanini anarekodi kikao kwa njia ya simu,ambapo mwenyekiti alijibu kuwa anarekodi kwa kumbukumbu hivyo DC akaamuru polisi walioongozana nao wamkamate mwenyekiti huyo ili akamtie adabu.

Hata hivyo mmoja ya askari waliomkamata amekiambia chanzo changu kuwa DC amewaamuru wamweke ndani kwa siku mbili na baadaye wamwachie kwa masharti ya kuripoti kituoni kila siku assubuhi kwa muda wa wiki moja

Ikumbukwe kuwa hoja ya DC kutaka kumng'oa mwenyekiti huyu ni baada ya wananchi wake kumzomea mbunge wa kilolo miezi kadhaa iliyopita pale alipoenda kijijini hapo kama mbunge huku akiambatana na makada wa ccm kwa lengo la kukinadi chama hali iliyomfanya m/kiti ahoji kama ziara ile ilikuwa kwa shughuli za chama au kibunge,Hata hivyo diwani wa viti maalumu kata ya mahenge aliendeleza uchama baada ya kuendeleza salamu chama huku akijua kwamba kijiji hicho kinaongozwa na mwenyekiti kutoka CHADEMA hali hii ilimfanya mwenyekiti wa kijiji kuondoka eneo la mkutano ili awaachie Mbunge na makada wake waendelee kufanya shughuli za chama chao ccm.Baada ya mwenyekiti kuondoka Mbunge alikutana na zomeazomea ya peoples power hali iliyomfanya aahirishe mkutano wake.

Hivyo baada ya tukio hilo wajumbe wa halmashauri ya kijiji ambao wote wanatokea ccm walianza kumshinikiza mwenyekiti huyu Obadia Lubugo (Chadema) kwamba aombe msamaha kwa kuondoka kwenye mkutano wa Mbunge lakini Mwenyekiti aligoma kuomba msamaha kwa madai ya kutotambua kosa lake,Lakini baadaye alifikishwa katani kwa hatua zaidi ambapo Diwani(ccm) na mtendaji kata waliendelea kumshinikiza mwenyekiti huyu aandike barua ya kuomba msamaha kwa kuondoka kwenye mkutano lakini mwenyekiti aliwajibu kwamba hataomba msamaha kwani hakuwa na kosa la kuondoka kwenye mkutano uliokuwa unafanya shughuli za chama cha ccm ili hali yeye anatokea chama kingine cha CHADEMA.Ikumbukwe kuwa mkutano huo ulikuwa na lengo la kugawa bendera za ccm na kadi za ccm zilizokuwa zimewekwa mezani kwa mbunge hali hii ilimtibua kabisa ndugu Lubugo ambaye mara kadhaa alijaribu kumshauri Mbunge kwamba kama wanataka kufanya kampeni wangeandaa mkutano mwingine wa chama lakini mkutano ule wangefuata utaratibu wa kawaida wa serikali badala ya chama.
Hivyo kutokana na hilo Diwani wa kata aliamua kumwita Mkuu wa wilaya ndugu G.Guninita ili aje amng'oe mwenyekiti huyu jambo ambalo liliishia kwa DC huyu kumweka ndani katika kituo cha polisi mbigili, mwenyekiti huyu bila sababu ya msingi na kwa muda usiojulikana.
 
Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,945
1,500
Matukio kama haya yananitia uchungu wa kufanya chochote chenye manufaa kwa taifa langu. Hakuna aliyejuu ya haki ya mtanzania yeyote kwa njia yoyote ile. Tunaweza kuendelea na ukondoo wetu, lakini Mungu hawezi ruhusu tuonewe na kondoo wenzetu.
 
Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,600
1,195
Chuki dhidi ya ccm inazidi kuwa kubwa..
Wengi wa viongozi hawa wanaoteuliwa na Rais wamekosa maadili.. Wanaweka maslahi ya chama mbele.. Upuuzi mtupu..
Ccm ni kama Panya!
 
Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,600
1,195
Yana Mwisho...Aluthacontinua... Tusonge mbele...
Mungu atawalaani ccm!
 
Kizotaka

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
561
0
Chuki dhidi ya ccm inazidi kuwa kubwa..
Wengi wa viongozi hawa wanaoteuliwa na Rais wamekosa maadili.. Wanaweka maslahi ya chama mbele.. Upuuzi mtupu..
Ccm ni kama Panya!
sikio la kufa haliskii dawa,magamba hayajistukii kabisa. Nadhani kwa kuwa yana roho za kijangili. Manake majangili yapo tu hayaishi.
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
7,680
2,000
Hivi huyu kilaza naye alipewa u-DC? Mara ya mwisho tuliambiwa anasoma kidato cha pili, kisha maliza masomo yake?
 
Noboka

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
1,208
2,000
Huyo DC, hajui kilichomkuta Dr. Kleruu nini huko Iringa? Maggid Mjengwa ukipita hapa mtumie zile makala zako yale mambo ya Mzee Mwamwindi na Dr. Kleruu (RC) enzi hizo, labda Guninita hajui historia kama inatabia ya kujirudia.
 
Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,606
0
Mobutu Seseko, Nduli Idd Amin, Adoph Hitler, Makaburu wa Africa kusini wote walifanya mambo kama huyo DC wa Kilolo, hata mkoloni wa Kiingereza hapa Tanganyika alimfanyia Nyerere na watu wake vitu kama hivi.

Kila jambo lina mwanzo lakini pia Lina mwisho wake.
Mkoloni mweusi(CCM) naye anafikia mwisho mwisho.

Ni wakati wa watanzania wote wanyonge kuungana na CHADEMA kuhakikisha CCM na serikali yake kwa gharama yoyote ya Amani tunawafuta kabisa katika ramani ya Tanzania.

Peopleeeeee's Poweeeeer!!!
 
UNDENIABLE

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
2,305
1,500
Matukio kama haya yananitia uchungu wa kufanya chochote chenye manufaa kwa taifa langu. Hakuna aliyejuu ya haki ya mtanzania yeyote kwa njia yoyote ile. Tunaweza kuendelea na ukondoo wetu, lakini Mungu hawezi ruhusu tuonewe na kondoo wenzetu.
Mungu hana muda na wale wasiojitambua! km hatujitambui na kuanza kudai haki zetu basi Mungu kamwe hawezi kuja kwa ajili ya hili, wasiwasi wa Mungu ni pale anapokupa tunu usiyoijua thamani yake hivyo kuwa kazi bure! maana hutoitunza! nakubaliana na Mungu!
 
mdeki

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
3,304
1,225
CDM na ssm ni paka na panya

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,369
2,000
Ni katika kuendeleza ubabe wake na ulevi wa madaraka DC wa kilolo bw.Gerald John Guninita amemweka rock up ya mbigili police station mwenyekiti wa kijiji cha udekwa bila sababu ya msingi.

DC huyu alifika kijijini hapo kwaajili ya kuendesha mkutano wa kumng'oa mwenyekiti huyo wa kijiji (CHADEMA) ambapo fununu zilishavuja siku chache kuwa ujio wake utakuwa maalumu kwaajili ya kuja kumng'oa mwenyekiti huyu ambaye hana hatia yoyote zaidi ya kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Lakini gafla alibadilisha mkutano na kuwa kikao cha ndani hali iliyowashangaza wengi na wakiwa ndani ya kikao alimuuliza mwenyekiti huyo kwanini anarekodi kikao kwa njia ya simu,ambapo mwenyekiti alijibu kuwa anarekodi kwa kumbukumbu hivyo DC akaamuru polisi walioongozana nao wamkamate mwenyekiti huyo ili akamtie adabu.

Hata hivyo mmoja ya askari waliomkamata amekiambia chanzo changu kuwa DC amewaamuru wamweke ndani kwa siku mbili na baadaye wamwachie kwa masharti ya kuripoti kituoni kila siku assubuhi kwa muda wa wiki moja

Ikumbukwe kuwa hoja ya DC kutaka kumng'oa mwenyekiti huyu ni baada ya wananchi wake kumzomea mbunge wa kilolo myezi kadhaa iliyopita pale alipoenda kijijini hapo kama mbunge huku akiambatana na makada wa ccm kwa lengo la kukinadi chama hali iliyomfanya m/kiti ahoji kama ziara ile ilikuwa kwa shughuli za chama au mbunge .......nitaendelea baadaye
Niuzie kesi hiyo ya false imprisonment! mbona kesi tamu!
 
Haludzedzele

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,424
1,500
huyo jamaa tangia alivyosifiwa na radio ebony alivyofanya upuuzi huo sasa imegeuka kuwa ndio tabia yake lakini atambue the day are numbered
 
Mbunge wa ilula

JF-Expert Member
Jun 3, 2012
211
195
Mdeki sasa paka ni yupi na panya ni yupi? kwa mpangilio wako unataka kuonesha kama Ccm ndo panya,je ni haki kumkamat mwenyekiti wa kijiji kisa anarekodi mazungumzo kwenye simu?
 
Mbunge wa ilula

JF-Expert Member
Jun 3, 2012
211
195
Asante Kibanga huyo ndiye DC mwenye uwezo wa kumkamata yeyote na kumweka ndani kama anavyotaka,he is above the law
 
fadisoni

Member
Dec 16, 2012
87
70
Inashangaza sana kijiji kimoja ambayo kinaongozwa na mwekiti wa chama pinzani alafu dc uende kushindana na nguvu ya uma hapo sasa inaonyesha CHADEMA inazidi kupanda chat
 
afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
1,250
Umesha sema Mwenyekiti wa kijiji ni wa CDM na Mkuu wa wilaya ni Gamba, hiyo tu inatosha kuwa sababu ya kumweka ndani. Hawa wana maagizo ya kuhakikisha viongozi wasio wa CCM wanadhalilishwa ili wengine wasiwaunge mkono au wasijitokeze kutaka kuwa sehemu ya washindani katika chaguzi zijazo.
 
Top Bottom