Kilo ya Sembe Tshs.1600/=

Kilo ya Sembe Tshs.1600/=

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,448
Reaction score
45,021
Tangu nifike hapa mjini miaka 16 iliyopita nikiwa mwanafunzi wa secondary, sijawahi hadi wa leo kununua kilo ya sembe kwa Tshs.1600.

Aisee haya mambo ni tafu sana, maisha hayasongi kiukweli tuacheni mzaha jamani...
 
Tangu nifike hapa mjini miaka 16 iliyopita nikiwa mwanafunzi wa secondary, sijawahi hadi wa leo kununua kilo ya sembe kwa 1600 kwa kilo.

Aisee haya mambo ni tafu sana, maisha hayasongi kiukweli tuacheni mzaha jamani...
1600 mbona bei rahisi...

Hapa kimara mwisho 1700/= , mji unaitwa miono njia ya sadani mbuga ya wanyama, kilo ni 1800/= na wadai soon itapanda....

Huko miono serikali imegawa mahindi ya msaada eti kilo moja kwa kaya moja, maaaniner hiyo kilo moja unafanyia nini ??

Muda utaongea tu.
Hali ni ngumu,
 
Unga umeshapigwa marufuku bado mnautumia tu!
Mkuu jamani hebu tuweke siasa pembeni, unajua labda nyie wenzetu unashiba, kilo ya unga wa sembe 1600 hadi 1800 jamani tunaishi kweli?? na msimu ndo bado mbichii....

Tuacheni siasa, tutakufwa....
 
hii nayo jamani iwe vita, maana hakuna adui mbaya kama njaa!! kweli tuoneane huruma hasa sisi watu wa kipato cha chini, watu mpo 6 nyumbani sasa hiyo kilo mtakulaje??
 
Tangu nifike hapa mjini miaka 16 iliyopita nikiwa mwanafunzi wa secondary, sijawahi hadi wa leo kununua kilo ya sembe kwa Tshs.1600.

Aisee haya mambo ni tafu sana, maisha hayasongi kiukweli tuacheni mzaha jamani...
Itabidi ukaripoti sentro mara moja ulishaambiwa anaetakiwa kutangaza njaa ni mmoja tu...
 
Tangu nifike hapa mjini miaka 16 iliyopita nikiwa mwanafunzi wa secondary, sijawahi hadi wa leo kununua kilo ya sembe kwa Tshs.1600.

Aisee haya mambo ni tafu sana, maisha hayasongi kiukweli tuacheni mzaha jamani...
Nimenunua juzi kilo moja 1800 wewe umeuziwa 1600 Heri yako
 
Tangu nifike hapa mjini miaka 16 iliyopita nikiwa mwanafunzi wa secondary, sijawahi hadi wa leo kununua kilo ya sembe kwa Tshs.1600.

Aisee haya mambo ni tafu sana, maisha hayasongi kiukweli tuacheni mzaha jamani...
Jamani tunahitaji msaada unga kilo elfu 2000 tunaenda wapi?viongozi wetu mko wapi msitukimbie kwenye janga hili tunajua hamleti mvua ila ebu saidieni bei zishuke tunaumia jamani.
 
Najitolea mfano una familia ya watu watano ukijumlisha na wewe mtu sita yani baba mama, mdada wa kazi watoto watatu asubuhi vifungua kinywa sii chini ya elfu tatu hapo nimepigia hesabu ya maandazi 2kila moja 500, mchana kuanzia mkaa , unga kilo 2000, mboga hapo sijaweka nyama sh 5000, jioni wali maharage, nazi na mboga za majani 6000 jumla 16, 000 pigeni wenyewe hesabu hapo bado hujabadilisha mlo ununue nyama, au samaki halafu unaishi nyumba ya kupanga unadaiwa kwa mwezi hela taka 2000, maji 4000, umeme15, 000 hapo sijajumuisha nauli za watoto shule na kodi ya nyumba halafu hawa wamiliki wa nyumba walivyo na roho mbaya eti garama za nyumba zimepanda kutokana na uendeshaji
Kwanza huwa najiuliza huo uendeahaji wa namna gani nyumba imejengwa tooka enzi za mwalimu choo ndio majanga ukarabati ziro kama sii wizi ni nini wallah atakae baki mjini kidume na hivi mvua ndio hazinyeshi ningejirudia zangu kijijini nikalime ya nini kujipa stress maisha yenyewe mafupi haya
 
Kwa hiyo miaka 16 ulitaka mambo yabaki vile vile.Basi hata wewe usingekuwa na sababu ya kukua.
 
Tangu nifike hapa mjini miaka 16 iliyopita nikiwa mwanafunzi wa secondary, sijawahi hadi wa leo kununua kilo ya sembe kwa Tshs.1600.

Aisee haya mambo ni tafu sana, maisha hayasongi kiukweli tuacheni mzaha jamani...
sembe mnapika ugali wa watu zaidi ya watano kwa kilo moja. sasa kama ni alfu mia sita, kwani bia mnanunua bei gani moja, mbona mnanunua bia zaidi ya buku mbili, mnazungusha meza yote na keep chenji ya baa medi juu. vumilieni hadi 2020.
 
Back
Top Bottom