Kama hizi tuhuma ni za kweli, then sanaa ya Tanzania inauliwa na Basata. Basata inapaswa kusimamia na si kujihusisha moja kwa moja na shughuli hiyo. Hivi ikitokea tatizo, nani atasimama katikati kama msuluhishi? Taasisi ambayo wasanii wanapaswa kwenda kupeleka malalamiko yao eti ndiyo inakuwa mstari wa mbele kuvuruga wasanii. Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Hii taasisi ilipaswa iwe mstari wa mbele katika kusimamia haki ili kutengeneza wasanii wengi watambulike kimataifa na kuiletea heshima nchi yetu. Bahati mbaya hii taasi inakubali kutumika katika kuua vipaji vya wasanii, mambo ya kipuuzi kabisa.