Kilio Kisichotarajiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilio Kisichotarajiwa

Discussion in 'JF Doctor' started by Kichankuli, Feb 23, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Kuna mazingira ambayo mtu kuangua kilio au kumwaga machozi ni kitu cha kawaidana watu hawapati na mshangao au tukio lenyewe kuwa na uzito mkubwa; sehemu za msiba au mtu anapatiwa kichapo cha nguvu. Lakini kuna mazingira mengine mtu anapoangua kilio au kumwaga machozi inaweza kutomvutia mhusika achilia mbali kuwa gumzo (big deal) kwa watu wengine na vyombo vya habari. Hali hii huwatokea watu wa rika na hadhi mbalimbali. Mathalan, hivi karibuni hali hii ilimkumba Mh. Waziri Mkuu wa TZ wakati anajibu maswahi ya wabunge lakini pia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu aliangua kilio kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani na kupelekea kikao hicho kuahirishwa. Nakumbuka pia kumwona kwenye Runinga Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa TZ akifuta chozi wakati akisikiliza hotuba ya Mwanaharakati wa Marekani (nadhani alikuwa Jese Jackson, alikuwa akielezea jinsi Mwalim Nyerere alivyomwandaa JK kuja kuwa kiaongozi tangu kwenye Umoja wa Vijana), achilia mbali kwenye hitimisho za mashindano ya Ulimbwende ambapo machozi humwagika pasipo kizuizi.

  Kwa kuzingatia ukweli kwamba wapo baadhi ya watu ambao kumwaga chozi kwao huwa ni ngumu sana, maswahi yangu kwa Matabibu na Wataalamu wanaohusiana na mambo haya ni haya:
  (1)Je, mtu kushindwa kuhimili hisia na kujikuta anaangua kilio au kumwaga machozi inaashiria udhaifu wowote?
  (2) Kuna namna namna yoyote ya kitabibu ya kuizuia hali hii isimtokee mtu?
   
 2. D

  Darling Member

  #2
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  it is all about personal emotional feeling.

  kama ulishawahi fiwa na loved one jibu unalo, na kama ulishawahi kufurahishwa; jibu unalo. Kama vyote havijakupata keep on waiting sinse it is all part of life.

  Darling
   
Loading...