Kilio cha watu wa kusini ya tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilio cha watu wa kusini ya tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spartacus, Apr 22, 2011.

 1. spartacus

  spartacus JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa kipindi kirefu sasa, watu wa kusini, hasa mikoa ya mtwara na lindi wamekua na kilio kimoja, barabara, kipande cha kilometa sitini tu, ambacho utekelezaji wake umegeuzwa kuwa wa kisiasa. Viongozi wote wamekufumbia macho kipande hicho, mkandarasi aliyepewa dhamana ya kujenga barabara hiyo amebweteka, hajishughulishi, ilhali muda wa kukabidhi umeshapita miaka mingi iliyopita, bado hata robo kazi haijatimia.....
  ninavoandika post hii, saa saba na dak 10 usiku wa tar 22/04/2011, kuna watanzania wenzetu, ambao leo wanalala kwa siku ya tatu eneo hilo, bila ya huduma ya chakula, maji wala choo...cha kushangaza, hakuna hata kiongozi mmoja aliyezungumzia tatizo hili, hakuna hata chombo cha habari kilichoonyesha tatizo hili, eneo lile ni porini, linasifika kwa ujambazi....lakini viongozi wamelifumbia macho.....
  mikoa ya kusini ina mawaziri zaidi ya watatu katika serikali hii, lakini wamewasahau watu wao....wakati umefika kuwakumbuka watu wa kusini, na kumaliza kilio chao cha muda mrefu........watengenezewe barabara ile...baadhi ya mikoa kila leo wanabandua lami na kuweka nyingine wakisema ni chini ya kiwango...watu wa kusini, wanataka japo hiyo iliyochini ya kiwango ili hii adha ya kulala njiani siku tatu....safari ambayo ni ya masaa 7 iwaishe.....
   
 2. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu poleni sana
   
 3. A

  AridityIndex Senior Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Da inaniuma sana my wife yuko hapo Nyamwage amenasa tangu jana hata sijuwi cha kufanya.
   
 4. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni sana kwa matatizo hayo! Ndio serikali ya Kikwete hiyo na hiyo mikoa ni stronghold ya CCM A (CCM) na CCM B(CUF) lakini ndio serikali imewatelekeza!!!! Na nyie wananchi wa huko inabidi mbadilike muache mambo ya ndio mzee ndio maana serikali inawafanya vichwa vya wendawazimu!! Fanyeni maandamano ile serikali ijue mna matatizo vinginevyo mtabaki hivyo hivyo huku wabunge wenu wakisubiri kurudi huko 2015 kuwaomba kura zenu!!
   
 5. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mkuu wananchi wa huko hayo wamejitakia wenyewe. Wanaishi miezi miwili tu kila baada ya miaka mitano, wakidanganywa na zawadi za khanga na mia tano tano.
   
 6. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Duh mpaka leo haijatengenzwa,coz walidai baada ya uchaguzi kipande cha somanga kitakuwa kimeisha...asikuambie mtu ndugu yangu hiki kipande cha kilometa 60 kinasumbua mbaya,mimi binafsi nilichelewa interview tanesco baada ya kukwama kwenye hiki kipande,nikitoka zangu mtwara,ikabidi nianze kupiga mguu coz magari yaliyokwama yalikuwa mengi mno,isitoshe wafanyakazi wa barabara hawakufanya kazi siku ile koz ilikuwa holiday,kwa bahati nzuri(mbaya) kulikuwa na msiba unasafirishwa kwenda mtwara,ndipo wale jamaa na magreda yao wakaanza kukwangua tope....mi binafsi nilitembea kwa mguu nikafika maeneo ya mbelembele huko nikapanda trekta nikafika dar saa 1 usiku interview ilikuwa ishaisha....nikakosa shavu tanesco.
   
 7. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Nyie si ndio wapenzi na mashabiki wa CCM, mwambieni shemeji yenu M.k.were awatengenezee barabara, si ameoa huko kwani huwa haendi kuwasalimia wakwe zake?? Jaribuni kuchagua hata CUF tu 2015 kwa majaribio mpate changamoto mpya, mufti si amekataza kuifagilia CDM...
   
 8. K

  Kukaya Member

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyie ozzie7 na kimilidzo mnaowashambulia watu wa kusini kuwa wanastahili shida kwa sababu ya ushemeji na kikwete na kuviunga mkono ccm na cuf ni mbumbumbu. tatizo la JF ni kuwa si wote ni wenye tafakuri ya kina. kuna mazuzu humu wengi tu tunaenda nao. ama kweli ktk kundi la mamba hawakosekani kenge. kuna kenge wengi humu. mkoa wa kigoma ambako kuna mbunge wa chadema, tena kiongozi wa ngazi ya juu una barabara mbovu nyingi tu. wana shida nyingi tu. unasahau kuwa chama tawala ni ccm na ndio chanzo cha matatizo na si wananchi. watu wa kusini hawastahili shutuma, bali kusaidiwa. chadema wenyewe walikuwa hawaendi huko kusini, walikuwa wanarandaranda kwenye ya kaskazini na dar. wananchi hawa wangekijulia wapi chadema? ndani ya JF tunataka great thinkers si watu wenye fikra kachara.
   
 9. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli kukaya, chadema waelekeze nguvu huko kuleta ukombozi maana wanamalizia tabora. Kusini ni sehemu m himmu sasa maana wanatawala watasikilizwa tu na kuwekewa barabara hizo tuwasaidie ndg zetu pamoja na kujitakia kwa muda mrefu wasamehewe wafuatwe kuokolewa
   
 10. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo Chadema ndo wangejenga hiyo barabara? Mbona hatujaona mchango wao popote? hela zote wanatumia na wake za watu tuu? Waende zao! Waambie wakamlipe fidia yule mhanga wao wao kujitakia wa Arusha!
   
 11. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  nasikia mkandarasi hajalipwa kama walivokubaliana
   
 12. A

  AridityIndex Senior Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kikwete na awamu hii ya nne ni sawa tu na awamu zile mbili zilizotangulia walitutosa tumewaona na huyu anatutosa tunamuona. Mbaya zaidi hata upande wa upinzani unaelekea kututosa we jaribu kufuatilia matokeo ya ubunge kwenye majimbo ya Mtwara. Ni almost pinzani 40% na CCM 58% na hizo zinapatikana bila kuungwa mkono na viongozi wa kitaifa wa vyama.

  Hakika tunajua watanganyika mnavyowafanyia watu wa kusini ni kama vile si sehemu yenu ya nchi, tena wala haijalishi vyama vyenu vya siasa. Nadhani inasubiliwa siku zanzibar wakilianzisha la mgao tu jamaa wanafuatia, just wait, maana tangu uhuru wao wamekuwa wahanga wa tawala zenu.
   
 13. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hee mi nilijua watu wa kusini ndo waTanganyika namba moja. Na huko kanda ya ziwa watu wameshachoka mahela ya migodi ya huko ndo yanajenga bwagamoyo na kwingineko! Je hii ni kweli?!
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,780
  Likes Received: 5,004
  Trophy Points: 280
  ..lakini kusini wana tabia ya kuchagua wabunge hao hao miaka nenda rudi.
   
 15. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wastue ndugu na jamaa zako kaka/dada, hao mawaziri ulowataja ndo wanaowalostisha.
  jamaniiii achaneni na ccm, na ninyi watu wa kusini ndo ccm na hamwambiliki kitu.
  badilikeni jamaa.
   
 16. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  naunga mkono hoja, ngoja wale jeuri yao
   
 17. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  hivi hawawaigi wenzao wa kigoma? mambo yanaendelea kuiva mpaka sasa wanaumeme mpaka wa reserve
   
 18. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #18
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mama Salma anapokwenda kusalimia kwao Lindi huwa anatumia barabara hiyo?
   
 19. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Daraja la Mkapa lisingejengwa kwa kasi ile kama angekuwa waziri wa ujenzi ni kutoka mikoa mingine nje ya mikoa ya kusini. Ndo mana Mkapa alimpa ile wizara Bi. Anna Abdhalah na daraja ilipoisha akamhamishia wizara ya afya. Bravo Mzee Ben kwa hili ulicheza kama Pele. Leo tunashuhudia wanaopita ktk wizara hii wasivyo na uchungu na adha wanayoipata watu wa mikoa ya kusini kwa hizi 60km. Tabu tupu!
   
 20. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  anatumia helkopta aina ya makirikiri
   
Loading...