Kilio cha wafugaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilio cha wafugaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Feb 3, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Habari za leo Dan,

  Rejea mazungumzo yetu ya jana. Kwa kipindi kisichopungua miaka kumi, baadhi
  ya wafugaji kutoka wilaya ya Hanang, Babati, na Mbulu walihama na mifugo yao
  kutafuta malisho baada ya hali ya hewa kuendelea kubadilika mwaka hadi mwaka
  na malisho ya ng'ombe kukosekana. Katika kuhama huko wamepitia wilaya na
  mikoa mbalimbali ya Tanzania. Kwa sasa baadhi yao wako kijiji cha Batini na
  kijiji cha Gongoni, Tarafa ya Kimamba, wilaya ya Kilosa, mkoa wa
  Morogoro. Katika kijiji cha Batini kuna Kaya 12, na kijiji cha Gongoni kuna
  kaya 40. Kaya hizi ni mchanganyiko wa Wabarabaig (Tatoga) na
  Wairaqw(famously known as wambulu). Watu hawa walifika katika vijiji hivi
  vya Kata ya Batini, Tarafa ya Kimamba, wilaya ya Kilosa kwa nyakati
  tofauti. Baadhi yao wamekaa hapo zaidi ya miaka minne hadi sasa, wengine
  mitatu,na wengine miaka miwili. Tofauti na jamii ya Wairaqw na Watatoga,
  pia kuna Wasukuma na Wamaasai waliofika Kilosa kwa nyakati tofauti.

  Siku za karibuni kulitokea ugomvi kati ya wamaasai na wakulima katika wilaya
  ya Kilosa eneo la Msowero. Kutokana na ugomvi huo, serikali ya wilaya ya
  Kilosa iliwaamuru wafugaji kuondoka katika maeneo ya wilaya ya Kilosa kama
  njia ya kutatua ugomvi unaojitokeza mara kwa mara kati ya wafugaji wa
  kimaasai na wakulima. Kufuatia amri ya serikali ya wilaya ya Kilosa kutaka
  wafugaji waondoke, askari wametumwa kuwakamata ng'ombe na kuwakushanya
  katika eneo maalum ili wapakiwe kwenye gari kurudi walikotoka. Katika zoezi
  hilo kila ng'ombe aliyekamatwa anaachiwa kwa faini ya shilingi elfu
  thelathini, na kulipa shilingi elfu tano kwa kila ng'ombe kila siku
  waliyokaa baada ya kukamatwa. Kana kwamba hiyo haitoshi, baada ya kulipa
  faini, gari aina ya fuso na canter zinaletwa na kulazimisha wafugaji wapakie
  ng'ombe wao kwenye gari bila kuambiwa mahali pa kuwapeleka. Gari hilo, si
  bure linalipiwa na mfugaji, kwa bei wanayokubaliana mwenye gari na serikali
  na siyo mfugaji.


  Kufuatia hatua hiyo, wafugaji walioko kijiji cha Batini na Gongoni
  wameyakimbia makazi yao ili kuokoa mifugo yao, huku baadhi yao
  wakiwaacha akina mama na watoto wakiteseka kwa njaa. Kinachoshangaza zaidi
  ni kwamba watu hao walipohamia hapo walipokelewa na wameendelea kushiriki
  katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia
  michango mbalimbali. Zaidi ya kushiriki katika shughuli za maendeleo, watoto
  wa jimii hizi za wafugaji wanasoma katika shule za vijiji hivyo.


  Maadhara yaliyosabibishwa na operesheni hii ya serikali ni (i) watoto wa
  wafugaji kuacha shule baada ya familia hizo kuamua kuondoka kwenda porini
  zaidi, (ii) Baadhi ya kaya zimewaacha akina mama na watoto na mbaya zaidi
  walipokutwa na askari walichapwa ili waeleze ng'ombe wamepelekwa wapi, (iii)
  kukumbwa na njaa, kwani kabla ya hapo wafugaji walikuwa wakinunua mazao
  kutoka kwa wakulima baada ya kuuza mifugo yao. Hivi sasa, mnada wa Mvumi
  unaoendeshwa takriban mara mbili kwa mwezi haupo kwa sababu ya hali
  hatarishi iliyosababishwa na serikali, (iv) Kunyeshewa na mvua, kwani watu
  hao walishajikita katika vijiji hivyo na kwa sasa hawana namna ya kujikinga
  na mvua baada ya kuyakimbia makazi yao. (v) kutelekeza kuku n.k., (v) msongo
  wa mawazo na kuishi kwa hofu.


  Kama taarifa ilivyotolewa katika vyombo vya habari, ukweli ni kwamba ugomvi
  kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya ya Kilosa ni kati ya Maasai na
  wakulima katika eneo la Msowero. Wafugaji katika eneo la Batini na Gongoni
  hawajawahi kugombana na wafugaji, na, pale ilipotokea ng'ombe wamevamia
  shamba, suluhu ilipatikana, na wafugaji walilipa faini. Swali la kujiuliza
  katika sakata hili ni, ng'ombe na mifugo kwa ujumla kama mmojawapo ya mazao
  ya chakula na biashara serikali imeyaundia wizara kwa sababu zipi kama
  mfugaji anakosa mahali pa kuwalisha mifugo wake? Je, mkulima ni bora kuliko
  mfugaji? Serikali inapoamuru wafugaji warudi walikotoka, imesahau kwamba
  watanzania hata hao walioko Kilosa na kwingineko wametoka nje
  ya mikoa wanayokaa na hata nje ya Tanzania kama historia inavyotueleza?
  Je, sote tulioko nje ya wilaya zetu turudi tuliko toka? Ukweli ni kwamba
  hata tulioko mijini na wote wanaofanya kazi maofisini ni sawa na wafugaji
  tu, kwani sote tunatafuta maisha ila tu mfugaji anayatafuta porini penye
  malisho bora.


  Kinachotia uchungu zaidi ni kwamba baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo
  wanatumia nafasi hiyo kuwatapeli hao wafugaji, kwa kuwaomba watoe fedha
  kiasi kisichopungua laki tatu, ili waendelee kukaa. Mwisho wa siku bado
  wanaambiwa waondoke. Haki yao iko wapi?


  Naomba msaada wako wa kisheria na namna ya kuwahabarisha wanaharakati wa
  haki za binadamu ili kusitisha operesheni hii chafu ya serikali yenye
  kumnyanyasa na kumdhalilisha mfugaji na watu wake kana kwamba yeye
  hachangii chochote katika pato la taifa. Naomba nikutafute kesho mchana
  kuanzia saa nane kwa maongezi zaidi.


  Asante sana
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu SHY kwa vile umepost hii habari we might as well tell you our piece of mind.
  Hawa jammii ya wamasai wanajaribu kuishi maisha ya karne ya 10 wakati tuko katika karne ya 21.Ni vyema wakaelimishwa kuwa nyasi zote duniani si mali yao na mifugo yao.Tazama uharibifu waliosababisha huko kwao Arusha, Kiteto,Manyara nk. Unachoweza kuwasaidia ni kuwaelimisha ufugaji wa kisasa si kuswaga ngombe dunia nzima.Wao wanaenda kule ambako hakuja haribiwa,jaribu kuwarudisha kwao iili ile ardhi itumike vizuri.La sivyo ile ardhi yao wikane ili wakulima wahamie huko!!!
   
Loading...