Kilio cha Kigwangala

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
370,624
Reaction score
858,170
Mwandishi ni mtu wa karibu wa mlalamikaji

Nimesikiliza video ya Mh Kigwangwala nimecheka sana

Huyu alikua Rafiki yangu sana kabla hajawa Waziri. Hata alipokuja London mimi ndio nilikua mwenyeji wake na nilimpokea kwa heshima sana yeye na kamati ya Bunge aliyokua akiongoza

Alipoteuliwa kua Waziri Wizara ya Afya mimi wakati huo nilikua namuuguza Mama Mkwe wangu aliekua akiumwa Ugonjwa wa Kansa. Kwa uchovu wangu nilikua nashindwa kupata kitanda pale Ocean road hivyo nikampigia simu kumuomba msaada nipate kitamda ili Mama Mkwe wangu ahamishiwe pale kutoka Muhimbili. Huwezi amini huo ndio ulikua mwisho wa mawasiliano yetu na akanipiga bloku. Iliniuma ila nikapotezea nikakomaa kigumu kuugua mgonjwa wangu

Jamaa alipotumbuliwa mara ghafla akaanza kunitafuta. Mimi sijawahi mbloku ila hua sijibu simu wala meseji sababu naogopa nitampa ukweli wake

Najua inamuuma sasa kwa sababu hajui na sasa anajua, ila hii ndio tabia ya Wanasiasa wengi wakiishateuliwa hua wanapotezea marafiki na kuwaona kama nuksi.

Anyway. CHEO NI DHAMANA. What goes around comes around …

Your browser is not able to display this video.
 
Good kwamba amekuwa honest na ame-share huu uzoefu, japo ni kitu obvious.

Kinachonishangaza ni kwamba nje ya ubunge, nje ya uwaziri wengine huwa honest na kuonyesha 'utu' nk. Ni huyu huyu Hamisi ndio alinyanyasa watu na vitisho tele akiwa pale wizara ya maliasili.
 
M
Maisha ndivyo yalivyo,tuombe sana unyenyekevu kwa Mungu,wengi tunajisahau!Sasa mwenzio mama yake anaumwa we unaingia mitini!Malipo ni hapa hapa Duniani.
 
Huyu jamaa ni mpenda mikopo hatari.. nakumbuka alizinguana na Mo Dewji ishu za mkopo wa pikipiki. Mimi ninamshauri akae tu kimya atazoea. Akubali kuwa system imemkataa. Kila nikikumbuka alivyowarusha kichura watu wazima naona ni sahihi na yeye kuchanganyikiwa sasa hivi.
 
Hamis alijisahau. Kwenye hizi wizara kuna watu hawana umaarufu wala elimu kubwa ila wanaweza battle na waziri na huyo waziri akang'oka.
 
Alipokuwa Naibu Waziri wa Afya aliwadhalilisha wafanyakazi wakiwemo waliomfundisha kwa kuwafungia nje kwa madai ya kuchelewa kazini
 
Kuna muha alitaifishwa ng'ombe 800 pori la Runzewe kipindi cha huyu jamaa.
 
Pole sana 😢
Kwahiyo hata issue za kuisemea simba basi kumbe kweli cheo ni dhamana🤔
 
Kwani Chris Lukosi anasemaje huko londoni....🫢
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…