Kilindi kimenuka tena

Kilindi kimenuka tena

sagemba

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
467
Reaction score
30
Kuna mapigano yanaendelea kati ya jeshi la polisi na watu wanaodhaniwa kuwa magaidi huko kilindi, Tanga.
Inasemekana kuwa polisi walikwenda kwa ajili ya kuwakamata,lakini jamaa hao walikataa kujisalimisha na kuanza kuwashambulia polisi kwa mapanga.

source: mtu aliyeko eneo la tukio
 
Si RPC alidai eti ni "Wanakijiji"! Kama hawa viongozi wetu wasipofuta unafiki kwa lengo la kuwapendeza wakubwa wao, hali kama hii itaendelea kujitokeza kila mara. Hili ni kundi la Answar sunni linalopata mafunzo maalum na lina silaha za moto limeamua kufanya ugaidi basi, hakuna cha kuficha hapo.
 
Juhudi zizidi kuimarishwa ili kukomesha hatari ya matishio kama haya ambayo tayari yameshaonesha kuwa na mlengo wa machafuko katika jamii yetu, hivyo matendo/ matukio ya aina hii kamwe si yakufumbia macho hata kidogo.
 
Kwa nini watz mwapenda sana kuimba wimbo wa "magaidi"? Kila tukio hata ujambazi sasa linabatizwa ugaidi!!!
 
wanashukiwa kuwa ni magaidi,walikuwa wanaendesha mazoezi yenye mlengo huo

okey...
nimeona page ya MARAFIKI WA RADIO IMAN huko wakitokwa povu ile mbaya.

na inasemekana polisi bado wanapambana nao huko msituni wamebaki watatu.
 
Kwa nini watz mwapenda sana kuimba wimbo wa "magaidi"? Kila tukio hata ujambazi sasa linabatizwa ugaidi!!!

sio kwamba kila kitu ni ugaidi ila walioko eneo la tukio wanasema kwamba jamaa walikuwa na sehemu za kufanyia mazoezi ya kijeshi,kitu kinachoonesha kuwa walikuwa wanajiandaa kufanya matukio yanayolenga upande huo
 
okey...
nimeona page ya MARAFIKI WA RADIO IMAN huko wakitokwa povu ile mbaya.

na inasemekana polisi bado wanapambana nao huko msituni wamebaki watatu.

inasemekana pia kuna watatu wamefariki na baadhi ya polisi wamepigwa mapanga
 
Ka walikua wanatumia mapanga sa hao ni magaidi au MANINJA..mi nachojua gaidi ni mwendo wa maguluneti na AK 47
 
Jambo unalolinuia ndilo linalokupata ccm na viongozi wake ndio waliokua wanautamani ugaidi bila ufikiria athari zake
 
Back
Top Bottom