Kilimo si kwa watu dhaifu

Ron70

Senior Member
Jan 20, 2022
106
262
Nimejaribu kufanya kilimo cha mahindi msimu huu wa kilimo and let me tell you something maina, kilimo is not for the weak.

Hamna rangi sija acha ona lakini as they say maji ukisha ya vulia nguo sharti uyaoge so we move .
 
Watu wanasema kilimo kigumu yeah hakuna urahisi kwenye kutengeneza pesa

Iko hivi ukiamua kufanya kilimo ni kama biashara panda shuka hazikosekani

Kuna msimu mtu anaweza akawa ameanza kilimo akavuna akakuta bei sokoni ni nzuri. Kundi hili kwa mfano msimu ujao soko likiwa na bei ndogo ndio huwa wanajazana mitandaoni na kusema kilimo hakilipi hakieleweki. Kawaulize wafanyabishara kama muda wote wanapiga tu maokoto kuna wakati hali si hali.

Kundi hilo juu ni sawa na hili kundi la pili wale ambao wameanza kilimo hawajakutana na soko zuri huenda msimu mmoja au miwili kama walivyotarajia nao hulalamika kilimo hakina tija.

Ukitaka kuona kilimo kinalipa wewe lima tu usikate tamaa huenda wengine wasinielewe hapa namaanisha ukiwa unalima bila kuacha utaona jinsi kilimo kinalipa usiwe mtu wa kujaribu na kuacha.

Niwape mfano rahisi tu: Mwaka jana waliolima vitunguu watanielewa jinsi tumepiga maokoto, gunia 1 limefika hadi 400,000

Msimu wa mwaka juzi wengi hawakuingiza mtonyo kwenye vitunguu bei haikuwa nzuri na mvua ziliwakwamisha waliotegemea kilimo cha mvua hivyo msimu wa mwaka jana hawakulima vitunguu.

Sasa ona yale makundi 2 niliyotaja mwanzo watakavyoingia kwa pupa msimu ujao kwenye kulima vitunguu. Wakati wa kuvuna wakikuta bei iko chini kutoka mfano 400,000 kwa gunia mpaka 100,000 kwa sababu wengi wamelima vitunguu wataanza tena kulalamika

Ikiwa kilimo kipo hivyo suluhisho ni nini? Wewe cheza na kauli mbiu ile ile wewe lima tu

Kilimo is not for the weak hasa cha biashara lazima uweke mpunga wa kutosha, usimamizi, tegemea ups and downs
 
Nimejaribu kufanya kilimo cha mahindi msimu huu wa kilimo and let me tell you something maina, kilimo is not for the weak.

Hamna rangi sija acha ona lakini as they say maji ukisha ya vulia nguo sharti uyaoge so we move .
Kaka unalima mahindi unasema kilimo sio kwa wanyonge.

Tafuta mahali ulime tumbaku ata heka mbili tuu..
Na usiombe kuwe na mvua nyingi kama msimu huu.
Pamoja na mkopo wa chama cha ushirika ila cash iliyokatika mpaka muda huu ni mil 8. Na hapo bado tumbaku haijachumwa, haijakaushwa, haujagrade, mabelo n.k.
Hapo sijaweka gharama ya kuandaa mabani. Kwa eka 8-9 mabani makubwa ni kuanzia matatu.

Hakuna kilimo kigumu Tanzania hii kama tumbaku.
 
Watu wanasema kilimo kigumu yeah hakuna urahisi kwenye kutengeneza pesa

Iko hivi ukiamua kufanya kilimo ni kama biashara panda shuka hazikosekani

Kuna msimu mtu anaweza akawa ameanza kilimo akavuna akakuta bei sokoni ni nzuri. Kundi hili kwa mfano msimu ujao soko likiwa na bei ndogo ndio huwa wanajazana mitandaoni na kusema kilimo hakilipi hakieleweki. Kawaulize wafanyabishara kama muda wote wanapiga tu maokoto kuna wakati hali si hali.

Kundi hilo juu ni sawa na hili kundi la pili wale ambao wameanza kilimo hawajakutana na soko zuri huenda msimu mmoja au miwili kama walivyotarajia nao hulalamika kilimo hakina tija.

Ukitaka kuona kilimo kinalipa wewe lima tu usikate tamaa huenda wengine wasinielewe hapa namaanisha ukiwa unalima bila kuacha utaona jinsi kilimo kinalipa usiwe mtu wa kujaribu na kuacha.

Niwape mfano rahisi tu: Mwaka jana waliolima vitunguu watanielewa jinsi tumepiga maokoto, gunia 1 limefika hadi 400,000

Msimu wa mwaka juzi wengi hawakuingiza mtonyo kwenye vitunguu bei haikuwa nzuri na mvua ziliwakwamisha waliotegemea kilimo cha mvua hivyo msimu wa mwaka jana hawakulima vitunguu.

Sasa ona yale makundi 2 niliyotaja mwanzo watakavyoingia kwa pupa msimu ujao kwenye kulima vitunguu. Wakikuta bei iko chini kutoka mfano 400,000 kwa gunia mpaka 100,000 kwa sababu wengi wamelima vitunguu wataanza tena kulalamika

Ikiwa kilimo kipo hivyo suluhisho ni nini? Wewe cheza na kauli mbiu ile ile wewe lima tu

Kilimo is not for the weak hasa cha biashara lazima uweke mpunga wa kutosha, usimamizi, tegemea ups and downs
Umemaliza kila kitu 👏🏾👏🏾👏🏾
Kilimo hakina shortcut lazima uwekeze kwenye maarifa na mtaji pia
 
Kaka unalima mahindi unasema kilimo sio kwa wanyonge.

Tafuta mahali ulime tumbaku ata heka mbili tuu..
Na usiombe kuwe na mvua nyingi kama msimu huu.
Pamoja na mkopo wa chama cha ushirika ila cash iliyokatika mpaka muda huu ni mil 8. Na hapo bado tumbaku haijachumwa, haijakaushwa, haujagrade, mabelo n.k.
Hapo sijaweka gharama ya kuandaa mabani. Kwa eka 8-9 mabani makubwa ni kuanzia matatu.

Hakuna kilimo kigumu Tanzania hii kama tumbaku.

Budget niliyo weka imepitiliza by 15% mpaka sasa na hapo nime lihudumia shamba kweli kweli kama vile mtoto yuko hospitali anaumwa.! Kwa kifupi haya mambo bila extra budget unakua na hali mbaya sana
 
Back
Top Bottom