Kilimo ni uti wetu

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,205
4,403
KILIMO NI UTI WETU.




1)Alipoumbwa adamu,alikabidhiwa jembe.
La kale la zama damu,alime hadi maembe.
Kilimo ndie nidhamu,ugumu katwa na wembe
Kilimo ni uti wetu,dira ya maendeleo.


2)lima hadi mboga mboga,familia ijigambe.
Usiseme kakuloga,kwa huo wako uzembe.
Chukia kula mizoga,kalime hadi ngarambe.
Kilimo ni uti wetu,dira ya maendeleo.



3)kilimo kufa kupona,juhudi siyo uzembe.
Familia itanona,watala na wajilambe.
Utenda hadi uchina,nyimbo nzuri uiimbe.
Kilimo ni uti wetu,dira ya maendeleo.




4)taifa lautukuza,ukulima si upambe.
Uchumi unaukuza,kwa kuuza unga sembe.
Mpunga bei wauza,kesho utaitwa jembe.
Kilimo ni uti wetu,dira ya maendeleo.

Shairi:kilimo ni uti wetu.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0624010160
 
Back
Top Bottom