Kilimo ni mkombozi kwa Watanzania

Kilimo ni mkombozi kwa Watanzania

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2020
Posts
341
Reaction score
303
Habari ndugu zangu!

Leo naomba tuiangalie sekta ya kilimo na namna gani inaweza saidia vijana kujiajiari.

Kilimo ni mkombozi kwa watanzania. Jamii nyingi ya watanzania wanafanya shughuli za kilimo. Waziri wa kilimo nchini Tanzania Mh. Japhet Hasunga akiwakilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 alisema

“Sekta ya kilimo imechangia kwa asilimia 28.7 na kuajiri 65.5% ya watanzania wote hadi mwaka 2017, ambapo sekta ndogo ya mazao ilichangia asilimia 16.58%, huku sekta ya kilimo ikichangia asilimia 65% ya malighafi za viwanda”.

Toka tupate uhuru mwaka 1961 kilimo kimekuwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu ya Tanzania. Nchi yetu imepiga hatua kubwa katika sekta nyingi za uchumi lakini bado kwenye kilimo tunasonga kwa mwendo wa konokono.

Matatizo na changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo tangu tulipoyarithi kutoka kwa mkoloni Mwingereza bado hatujayapatia suluhu. Bado wakulima wengi wanatumia jembe la mkono huku wakipiga magoti kwa Mungu mvua inyeshe. Vyama vya ushirika navyo vimeshindwa kuwa mkombozi kwa wakulima.

Watanzania bado akili zetu zinakumbuka namna sekeseke na sakata la korosho lilivyoteka Bunge mwaka jana. Wabunge wanaotoka maeneo ya kusini( Lindi na Mtwara) waliweka itikadi ya vyama vyao pembeni na kuungana kwa pamoja kupigania maslahi ya wakulima wa zao la korosho.

Ardhi inayoizunguka nchi yetu ya Tanzania ni fursa kubwa kwa vijana kujiajiri. Wengi wetu tumetokea katika familia za wakulima.
Kilimo kimetulisha na kutulipia ada za shule.
Neema hii tuliyopewa na Mwenyezi Mungu ya ardhi yenye rutuba na kuzungukwa na mito mingi na maziwa kila pembe ya nchi yetu ni tunu kubwa inayoweza kubadilisha maisha ya vijana wa Tanzania.

Fursa ipo waziwazi kwa vijana lakini changamoto kwa vijana wengi wa kitanzania tunatoka katika familia duni. Hali zetu za kiuchumi na historia ya familia zetu ni kikwanzo kikubwa kwetu.

Hatuna sifa za kukopesheka kwenye taasisi za kifedha na sera za serikali sio rafiki kwetu. Wengi wetu tumebaki na chaguo la kuzunguka na bahasha kila ofisi kuomba kazi. Hii ndiyo njia pekee inayomwenzesha kijana anayejitambua kukusanya mtaji wa kujiajiri katika kilimo.

Ni kweli baadhi ya vijana wamejaribu kujiajiri katika kilimo, wachache wamefanikiwa lakini wengi wameangukia mikono mitupu. Nilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Haule Juma( kumbuka hili sio jina lake halisi).

Haule Juma ni kijana mwenye shahada ya Takwimu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Baada ya kuhitimu chuo mwaka 2017 alijiajiri kwenye kilimo cha viazi pamoja na vitunguu saumu maeneo ya nyumbani kwao mkoani Iringa.

Haule anasema “nilijiajiri kwenye kilimo baada ya kuhitimu chuo, sikuwa na mtaji mkubwa na nilitumia mashamba ya nyumbani, mtaji mdogo ndio changamoto kwangu kwani bei za pembejeo ziko juu sana.

Nilikuwa na mtaji wa laki tano lakini nilijikuta natumia zaidi ya pesa ambayo nilikuwa nayo. Mfano nilipokuwa naanza nilijua mbolea mfuko ni shilingi elfu 60 lakini wakati naenda kununua nikakuta mbolea bei yake ni shilingi elfu 80.

Mwaka 2019 nilitumia gharama kubwa kwenye vitunguu saumu lakini ilipofika wakati wa mavuno bei yake ilikuwa chini sana kiasi kwamba niliambulia hasara tupu na mtaji wangu wote umeisha kiasi ya kwamba siwezi tena kumudu gharama za pembejeo”.

Ndugu zangu watanzania tuna mifano mingi ya watu kama kina Haule wenye nia ya dhati ya kujiajiri katika kilomo. Changamoto kubwa wanazokumbana nazo kina Haule ni mtaji na sera za kilimo zisizokuwa na msaada kwao.

Haule kwa uzoefu alioupitia kama kijana ana ushauri huu kwa serikali yetu. “Kuna maeneo ambayo ni potential kwa kilimo cha umwagiliaji, lakini serikali inakataza sisi wakulima tusiyatumie. Ninaishauri serikali iweke utaratibu mzuri wa kulinda vyanzo vya maji ili watu waendelee kuyalima”

Itoshe kusema kwamba Taifa letu lipo katika uchumi wa kati lakini bado wakulima wengi wa Tanzania hawanufaiki na uchumi wa kati. Hali za kiuchumi za wakulima wa jembe la mkono ni mbaya sana na wengi wamekata tamaa.

Watanzania wenzangu naombeni tuwakumbushe wale wote wanaoomba tuwapigie kura Oktoba 28 kwamba wakulima wana hali mbaya sana. Tunawaomba kipaumbele kwao kiwe ni kilimo kwanza. Binafsi ninawakumbusha kwamba asilimia 65.5% ya watanzania tegemeo na tumaini lao la kuishi ni kilimo.
 
Provided jembe la mkono linaendelea kutumika kwa 70% kilimi bado kipo primitive.Serikali inashindwa kuvipa vijiji zana za kisasa za kilimo kwa mkopo ? Wanachojua ni kuwatungia wakulima sheria ngumu za kuuza mazao yao.Unalima halafu ukivuna huna Uhuru na mazao yako, inaingia akikini!
 
Kilimo ndio chanzo chetu kikuu cha chakula, chakula ndio afya. Ila tu kilimo iwe Plan A kwa anayependa na kuchagua kujiajiriri au kuajiriwa huko; na sio Plan X yaani mtu asome shule ya msingi miaka 7, O-level miaka 4, A-level miaka 2 na chuo kikuu miaka 3 hadi 5 kisha atafute ajira weeee halafu akichoka ndipo ageukie kilimo.... Zaidi ya miaka 5 itakuwa imepotea bure!
 
Provided jembe la mkono linaendelea kutumika kwa 70% kilimi bado kipo primitive.Serikali inashindwa kuvipa vijiji zana za kisasa za kilimo kwa mkopo ? Wanachojua ni kuwatungia wakulima sheria ngumu za kuuza mazao yao.Unalima halafu ukivuna huna Uhuru na mazao yako, inaingia akikini!
Kweli hii ndo changamoto kubwa wakulima wanayopitia hakuna sera wezeshi kbsa kwa wakulima
 
Kilimo ndio chanzo chetu kikuu cha chakula, chakula ndio afya. Ila tu kilimo iwe Plan A kwa anayependa na kuchagua kujiajiriri au kuajiriwa huko; na sio Plan X yaani mtu asome shule ya msingi miaka 7, O-level miaka 4, A-level miaka 2 na chuo kikuu miaka 3 hadi 5 kisha atafute ajira weeee halafu akichoka ndipo ageukie kilimo.... Zaidi ya miaka 5 itakuwa imepotea bure!
Nami nazungumzia hasa wale wenye nia ya kujiajiri katika kilimo lakini mazingira hayawaruhusu.
 
Back
Top Bottom