SoC01 Kilimo ni Kiini cha Maendeleo ya Taifa letu

Stories of Change - 2021 Competition

Noel kiona

New Member
Aug 7, 2021
1
0
KILIMO NI KIINI CHA MAENDELEO YA TAIFA LETU.

Kilimo ni mfumo wa uzalishaji unaojikita katika makundi mawili ambayo ni mazao ya mimea na mifugo. Moja ya vitu muhimu katika maisha ya viumbe hai ni kupata chakula kingi na bora kwa afya na uhai. Hivyo kilimo kinachukua nafasi kubwa sana katika ukuzaji na uboreshaji wa afya za viumbe hai ambavyo pia huwa ni chanzo cha kuyafanya mazingira yawe bora. kupitia kilimo na sehemu zake kuu tunaweza kufanikiwa na kukuza sekta nyingine nyingi zenye kutuletea tija katika uchumi wetu. Moja ya sekta inayoweza kusababishwa na kilimo ni biashara mbalimbali yaani mazao ya kilimo yanaweza kuliwa kwa namna nyingi kama vile viwandani nk.

Kilimo katika viwanda tunapata chakula na mavazi, vifaa vya malazi na vifaa vya ujenzi ikiwa ni faida ya kilimo bora. Kwa asilimia 95% ya chakula tanzania kinazalishwa na watanzania wenyewe kwa sababu tanzania ni nchi yenye rutuba na hali ya hewa ni nzuri kwa kuzalisha aina nyingi sana za mazao ya chakula na biashara yaani ( small an large scale agriculture)

Katika Nchi yetu asilimia kati ya 75% na 85% ya mazao hutumika katika biashara ambayo huliongezea taifa pato kubwa kupitia tozo za kodi zitokanazo na bidhaa zilizodhalishwa kwa kupitia kilimo hivyo hutumika kama kitega uchumi cha taifa letu.

Kilimo katika nchi yetu kimekuwa kikitengenezewa baadhi ya kauli mbiu nyingi sana kutokana na nyakati na awamu mbali mbali za uongozi kama vile kilimo ni uti wa mgongo, kilimo kwanza nk lakini bado sekta hii haijamkomboa mtanzania na taifa kwa ujumla kutokana na changamoto mbali mbali.

1. Kilimo chetu kimekua na udumavu kwasababu ya ufinyu wa miundo mbinu kama vile barabara imara toka mashambani, umeme wa kuchakatia mazao ghafi na maji ili kuimarisha kilomo cha umwagiliaji.

2. Kilimo chetu kimekua sio cha kisasa kwasababu hatuna wataalamu wa kutosha katika nyanja zote za kilimo yaani uzalishaji mazao ya mimea na wanyama.

3. Kilimo chetu kkmekua kinakabiliwa sana na magonjwa ya mfumko mfano 2015 kutokea kwa ugonjwa wa kanitangaze ambao ulipelekea kuharibiwa kwa mazao ya kilimo kwa kiasi kikubwa

4. Kukosa soko zuri kwaajili ya kuuzia mazao yetu hasa katika kipindi hiki cha janga hili la dunia la ugonjwa wa corona (covid-19) ndio limeharibu kabisa mifumo yote ya masoko hata kwa nchi jirani tu nasi hakuna biashara nzuri ya mazao inayoendelea na baadhi ya nchi hata viwanda vyao vimesimama maana watu huwa kwenye lockdown muda mwingi hivyo uzalishaji wa bidhaa za kilimo hupungua

5. Kilimo chetu kinakabiliwa na ufinyu wa teknolojia ya viwanda kwenye nchi yetu mfano tunazalisha mkonge, kahawa, chai, korosho nk lakini kwetu sisi tunafanya kazi ya kuzibangua tu mambo mengine yote ya uzalishaji bidhaa hufanywa nje ya nchi yetu hivyo hupunguza ukuzaji wa uchumi wa taifa letu.

Hivyo ikiwa tutafanyia ufumbuzi wa sababu hizo hao juu taifa letu litaingia kwenye rekodi kubwa sana ya kupata mafanikio kupitia kilimo kwa asilimia zaidi ya 89% kwasababu hali ya hewa na ardhi yetu vinaruhusu kufanya kilimo cha aina yoyote na kupata mafanikio.

Kubwa zaidi kwangu mimi mtafiti na mshauri juu ya masuala ya kilimo kwa ujumla ni kueleza umma wa watanzania namna gani wafanye na kwa wakati gani hicho watakacho fanya kitaleta tija kwenye taifa letu na kwa maisha ya mtanzania mmojamomoja.

Mfano mzuri sasa hivi jamii ya tanzania hasa mikoa ya kusini inapambana na kujikita katika uzalishaji wa zao la parachichi ( avocado fruits) na vanila kwa sababu ni mazao yaliyo onesha kuleta unafuu wa maisha ya watu, lakini huwezi kuona serikali ikihangaika na jambo hilo kama kutafuta soko zuri, kujenga viwanda na kupanga bei nzuri zenye tija kwa taifa mwisho wake tutaishia kuuzia nje kwa gharama ndogo na kununua bidhaa zao kwa gharama kubwa kwa kitu tulichozalisha wenyewe na kulifanya taifa liendelee kuwa na uchumi duni kila uchwao.

Hivyo ushauri wangu kupitia ukurasa huu wa jamii forum ambao na hakika wengi wetu hupitia kusoma mambo mbalimbali ya kijamii, uchumi, siasa nk liwe ni funzo tupate kujipambanua tunawezaje kubadili sekta ya kilimo kuwa kiini cha maendeleo ya uchumi wa taifa letu hata kama tunapitia changamoto nyingi na kubwa dumiani kama janga la corona.

Tena kwa serikali inawezaje kuwa saidia watu wake kupata wataalam wa kilimo walio bora ilikuokoa jahazi hili la anguko la kiuchumi lililopo mbele yetu hasa kutokana na janga hili la corona.

Tunaweza kudhani kuwa tumepoteza sana mwelekeo katika kupambana na janga hili lakini tunaweza jigeuza na kupata ahueni ya maendeleo kwa taifa letu ikiwa tutajikita na kuwekeza kwenye kilimo kuliko vitu vingine vyote kwa sababu kilimo kinagusa maisha ya kila mtu kote duniani.

Kutokana na umuhimu wa kilimo mataifa yakafikia hata uamuzi wa kuadhimisha shughuli mbalimbali za kilimo mfano kwetu ikateuliwa siku ya tarehe 8/8 kila mwaka ili kukumbushana namna bora ya kufanya kilimo na utunzaji, uuzaji na unufaikaji kupitia bidhaa za kilimo na kuhamasisha aina mbalimbali za kilimo kwakua hali inaruhusu kwa mazao yote kutegemea na ukanda.

Uchumi wa israel unategemea sana kilimo hata kama hali yao sio nzuri kwa sehemu kubwa kwao ni jangwa lakini wamefanikiwa sana, itakuaje kwetu sisi kwenye taifa lenye rutuba na hali nzuri ya kilimo tushindwe ikiwa tutaamua kuwekeza huko, binafsi naona hatuwezi kushindwa kikubwa tuwekeze nguvu, tutumie vizuri ushauri tunapewa kutoka kwa watalaam wetu hata kama ni wachache na kuwasihi watu wa masoko kujikita kutafuta masoko yaliyo bora na kwa bei nzuri ili kunufaika na kilimo chetu bila kusahau serikali kuruhusu wawekezaji wa viwanda ili kuhalikisha bidhaa zote za kilimo zinatengenezwa hapa hapa nchini kwetu kisha bidhaa zake ndizo ziuzwe nje zikiwa tayari kwa matumizi.​

Moja vitu ambavyo vinatufelisha watanzania ni kufanya maamuzi sahihi hilo ndio tatizo kubwa kwetu bali tulio wengi huwa tunaishi kwa kuiga nani anafanikiwa kwa kufanya nini ndio maana kila tunapogusa huwa ni pagumu sana kwasababu hatukujua hatua za hicho tunachotaka kukifanya ndio maana uchumi wetu unabaki katika hali ya udumavu, hivyo nikushauri tu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa jamiiforum kwamba katika kilimo bora na cha kisasa tunaweza kua kiuchumi na mambo mengine tukayafanya kwa uhuru na utulivu kwa msaada wa sekta hii ya kilimo. Asante kwa kusoma makala yangu.
 
Back
Top Bottom