Kilimo kwanza bila mfano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo kwanza bila mfano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by everybody, Aug 16, 2011.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Historia inatuambia kwamba enzi za mwalimu, viongozi wa wilaya, vijiji, nk. ilikuwa ni lazima wawe mfano katika kilimo kwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na shamba zuri lenye mazao yaliyostawi vizuri na wanakijiji wengine walifuata mfano kutoka kwa viongozi. Hata mwalimu mwenyewe alionyesha mfano kwa kuwa na shamba lenye mazao yaliyostawi vizuri na wanakijiji wengine waliiga kutoka kwake.

  Kwa sasa serikali ya CCM inapigia kelele kilimo kwanza wakati katika viongozi wake ni wachache ambao wanaitekeleza hii sera kwa vitendo. Wengi wao wanaishia kula starehe mijini hasa jijini Dar na kusahau kurudi vijijini kwao kushirikiana na wananchi katika kilimo kwao. Hili naona ndo kikwazo kikubwa katika maendeleo ya kilimo Tanzania na siku zote itaishia kuwa wimbo kama ulivyo wimbo wa kuhamishia serikali Dodoma. Kama kweli serikali imedhamiria kuendeleza kilimo, iweke mazingira ambapo viongozi wake wakuu watakua mfano kwa kumiliki na kulima mashamba katika vijiji vyao ambapo wananchi wataiga kutoka kwao. Huwezi kusema unahamasisha kilimo kwanza ukiwa kwenye stuli ndefu mikocheni huelewi hata jembe linashikwaje. Wakati umefika sasa tuache siasa za kutoana barabarani na viongozi watekeleze kwa vitendo wanachokisema.

  Kama viongozi hawajihusishi kwenye kilimo ni saa ngapi watajua pembejeo hazijafika kwa wanavijiji wao? nitoe ombi kwa wabunge na viongozi wengine wa serikali washiriki kilimo kwanza kwa vitendo sio kutupigia kelele za kinafki bungeni. Nategemea hata Rais siku moja atuonyeshe jinsi shamba lake la minazi pale Chalinze lilivyostawi ili wanakijiji wengine wajue kua inawezekana.

  Naomba kuwasilisha.
   
Loading...