Kilimo kwa njia ya mtandao

My Joash

JF-Expert Member
May 31, 2020
270
213
Wakuu salam, kuna mtu kanisimulia kuhusu kampuni inayofanya kilimo kwenye mtandao.kwamba unatuma hela wao wanalima na kushughulikia mazao,yakiwa tayari wanauza unapewa hela yako,je ni kweli? Au ni jamii ya akina DECI ?

Naomba mwenye ufahamu zaidi anijulishe.Jamaa aliyeniambia anaanza kushawishika kujiunga nao,mimi napata mashaka na hii kitu.

Karibuni wakuu.
 
Njia hiyo haijawahi kufanikiwa mkuu, kuwa makini wengi ni matapeli, ni walewale akina Mr. Kuku farm tofauti ni version tu,
 
Wasomi wapo wengi ajira hakuna sasahivi wanatumia elimu waliyoipata ili kutapeli maana hakuna namna nyingine. Ni Kama Nigeria tu vijana wanapambana namna ya kutapeli kwa njia ya mtandao.
 
Wasomi wapo wengi ajira hakuna sasahivi wanatumia elimu waliyoipata ili kutapeli maana hakuna namna nyingine.
Ni Kama Nigeria tu vijana wanapambana namna ya kutapeli kwa njia ya mtandao.
Shukrani mkuuu
 
Yale yale ya Mr.kuku watu wanaliwa hela kwa kupenda mteremko, Nani aende shambani akalime aoteshe'apalilie'aweke mbolea'alinde wafugaji wasiingize mifugo,alinde ndege waharibifu aje avune halafu mgawane? Sahau.
Hata mimi nilishangaa boss,nitamshauri jamaa aachane nao
 
Hata mimi nilishangaa boss,nitamshauri jamaa aachane nao

Hao watakuwa na shamba la kuzugia tu kuoneshea watu.​

Kinachofanyika unaweza kuta Kuna mafisadi, wahalifu, wauza madawa ya kulevya nyuma ya pazia wanaficha pesa zao kwa mgongo wa hiyo biashara baada ya muda wanaenda wanavuna pesa Ni sawa na kuvunja kibubu sema inakuwa zamu zamu mwezi huu anachukuwa huyu mwezi ujao anachukua fulani hivyo hivyo mzunguko unaendelea.​

Serikali inasikilizia kibubu kijae zikiwa nyingi kufikia mabillion tayari inapiga pin account na kushitakiwa kwa kosa la kutakatisha pesa Kama Mr Kuku alichofanyiwa.​

Kesi Kama hizi walalamikaji wa kutapeliwa wanakuwa wachache kwa kuwa wanajua mchezo waliokuwa wanaufanya na hawawezi kujitokeza maana ukijitokeza nawe unapigwa pingu.​
 
Boss kwa kukusaidia achana na hiyo kitu,, ni biashara ya upatu, utarudi hapa ukilia. Mshauri na huyo mwenzako kuwa mafànikio hayajawahi kuja kwa style hiyo.

Huo ni utapeli kama wa Mr Kuku! Tafuta shamba lima mwenyewe kama unapenda sana kilimo.
 
Mkuu easy come easy go!! Usipumbazwe na hela chap chap kazi nzuri ifanyike either ukiwepo au unapita kukagua ila pesa ya kumpa mtu wewe una kaa unangoja mavuno mazuri hapo sio kweli.

Waambie wakuonyeshe project wanapo fanyia na uchunguze uhalali wa hiyo project kama kweli ni yao, kz una weza pelekwa kwenye mashamba ya watu uka aminishwa kumbe na wao wanapita tu.

Kuna uhitaji ya kutafuta kazi za ziada kuongeza kipato ila nyingine niza kumizana mkuu kuwa makini kwa hilo.
 
Back
Top Bottom