Dah Tanzanians brains at work. Tatizo uongozi wa kisiasa, mwanasiasa anakwenda kununua mvua ya kutengeneza Thailand eti tuitumie kwenye kilimo chetu. Tunaacha ku-invest na kuzitumia skills za watanzania wenzetu kama hawa wa Misungwi.
Naomba kuuliza, hivi maji ya kisima kirefu yanaweza kutumika kumwagilia? namaanisha yakiwa na chumvi chumvi au yataua mazao?
Dah Tanzanians brains at work. Tatizo uongozi wa kisiasa, mwanasiasa anakwenda kununua mvua ya kutengeneza Thailand eti tuitumie kwenye kilimo chetu. Tunaacha ku-invest na kuzitumia skills za watanzania wenzetu kama hawa wa Misungwi.
nafahamu yanatumika sana kanda ya kati yakiwa na chumvi ya wastani lkn kama ni maji ya kisima kinachovuta maji ya chumvi kali ya bahari mizizi huwa inaoza, lkn kama conc. ya chumvi ikiwa ndogo hamna tatizo
Mkuu Narubongo kuna drillers wowote wa Visima unawafahamu tokea Dodoma? Unaweza kujua na costs zao za kuchimbia kisima kwa meter? Nahitaji kuchimba kisima shambani Dodoma kwa ajili ya kuset irrigation system kutoa drillers Dar is a bit expensive,Please naomba Mwongozo wako
wakuu hv kuna kisima kinachoweza kumwagilia heka mia
siyo kisima ni bwawa (dam)
construction is either elevated or underground (excavated)
Mbona unanikatisha tamaa aisee ukiwa na kisima kirefu kama cha mita 100 utashindwa kumwagilia eka 100?
mkuu .... kisima cha depth ya 100m? .... my God .... depth ya bwawa ni around 5m na kubwa kwenye bwawa ni kutengeneza kingo imara .... gharama za bwawa zitakuwa ni equipments kama excavator .... bwaw utafanya irrigation traditional kwa kugawa maji kwenye mifereji (channel irrigation) bwawa ni environmental friendly na samaki utafuga
Gharama ya bwana ni kubwa sana ukilinganisha na uchimbaji wa kisima, Kisima cha 100M kinaweza kukugharimu only 15M hadi kinafanya kazi bwawa bila 100M plus mmmmmmh sidhani
Ahsante mheshimiwa Narubongo ntamcheki Mgombezi mimi kwa sasa hivi shida yangu ni kuchimba kisima kwanza ntatumia sprinkler irrigation kwa sasa hivi cost zake zipo chini ukilinganisha na drip irrigation .
It's a bit big project so ntakuwa nawafanyakazi permanent hapo Shambani so ulinzi sio ishu afterall sehemu ninapolima hakuna wizi ni bush kidogo hata hizo pump hawazijui
installment cost ya drip system ni kubwa hata hivo running cost ni ndogo ukilinganisha na sprinkler system kutokana maji ya yanoyotumika kidogo ,na yanakuwa pumped at low pressure saving energy. Indeed a solar powered drip system inawezekana sana.
mkuu .... nimegundua kumbe tumepishana lugha .... kisima ulimaanisha drilled water well au borehole .... mimi nilijikita kwenye kuhifadhi maji ya kumwagilia .... okay, kumbuka ukishachimba maji hayo ya kisima utahitaji kuyahifazi kwanza kabla ya kuanza kuyasambaza kwenye umwagiliaji hivyo itakubidi ujenge matanki ya concrete au mabwawa .... heka 100 let say utahitaji storage ya maji 1,000 cubic meters (1,000,000litres)