Habari za mida ndugu zangu nilikiwa naomba mchanganuo wa tikiti maji kianzia mbegu nzuri ya Arashani FI-kutoka syngenta-KUTEGEMEA NA NIA YA UMWAGILIAJI UTAKAYOTUMIA (MIFEREJI-FURROW AU DRIP) GHARAMA ITAVADY SANA, KAMA HUNA DRIP LINE (UMWAGILIAJI WA MATONE) KUNUNUA NA KUFUNGA DRIP LINE YA KUTOSHA EKA 1 SI CHINI YA MILIONI 2.5, na duka gan la pembejeo zinauzaje izo mbegu vile vile kwa ecar 1-KWA EKA MOJA KUTEGEMEA NA NAFASI YA KUPANDA UTAKAYOTUMIA UNAHITAJI TAKRIBANI MBEGU GRAM 250 HADI 300, BEI ZA MBEGU NYINGI KAMA UKIENDA KWA WAZALISHAJI WENYEWE MFANO SUKARI F1 GRAM 500 NI TSH 220,000, MASHIRIKA MENGINE MBEGU ZA HIZO GRAM 500, BEI NI KATI YA TSH 200,000 HADI 350,000. KWA USHAURI WANGU MTAFUTE MUUZAJI WA SYNGENTA KWA ZONE ULIPO ILIA AKUPE MBEGU HARISI, WATU SI WAAMINIFU KUNA MBEGU FEKI NYINGI SANA MASOKONI. tikit likikubali unaweza pata shilling ngap-KUU MAPATAO YANATEGMEA NA MSIMU, KAMA SASA BEI YA TIKITI IMESHUKA SANA, NA UJIPANGE MNOO KUHUSU MADALALI HAO NI WATU HATARI SANA KATIKA BIDHAA ZA KILIMO, BEI ZAO MARA NYINGI AKIJA SHAMBANI MWENYEWE, TIKITI LILE BORA KABISA LA KILO 12 ATAKWAMBIA TSH 700-25000 TSH AMBALO HILO SOKONI HUUZWA 3000-6000TSH, HIYO BEI YA TSH 2500/TIKITI NI ULE WAKATI AMBAO TIKITI NI ADIMU MNO SOKONI. KIONGOZI JIPANGE LENGA KWANZA KUZALISHA MAZAO BORA NA UHAKIKISHE KWANZA UNARUDISHA MTAJI WAKO, LKUNA UNCERTENITY NYINGI SANA KATIKA KILIMO, WAKO WANAOFANIKIWA NA WAPO WANAOANGUKIA HASARA, KWA EKA MOJA GHARAMA ZA UZALISHAJI SI CHINI YA 2.5 MILIONI vile vile mbolea ya samadi tan1 shillingi ngap-BEI YA SAMADI INATEGEA UNAENDA KUNUNUA KWA NANI, MANAJUANA? KUNA UMBALI GANI WA MAHALI ULIKO NA SHAMBANI, WENGINE HUFANYA TANI 1 TSH 80,000 HADI 150,000. Na mbolea yaramilanayo je- SINA HAKIKA SANA LAKINI MFUKO WA KILO 25 BEI YAO INACHEZA KATI YA TSH 60,000 HADI 85,000TSH- (Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi)? Msaada ndugu zangu naweek 3 2 zimebaki nianze mtad huo
WADAU WENGINE WATAONGEZEA.
KILA LAKHERI