Kilimo cha nyanya wakati wa masika

kaligopelelo

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,764
3,940
Habari za weekend wanajamvi.

Wakuu naombeni ushauri wa mbegu bora ya nyanya ya kisasa inayostahimili wakati wa masika na bei yake. Naomba kuzijua mbegu zinazozaa vizuri wakati huo na zinazovumilia magonjwa.
Natumaini kuwa nitasaidiwa.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
 
Sawa mkuu nitaitafuta,vp hii mbegu ni ndefu au fupi? ili nijiandae mapema na miti ya kuinulia.
kama sikosei eden ni jamii moja na asila f1, eden ina sifa ya kufyonza maji asila ina sifa ya kuvumilia ukame! tafuta nyuzi za "kiimo maarifa" humu uzifwatilie...kachambua sana nyanya na mazao mengine.
 
Write your reply...Unataka kupanda kwenye open field au green house?
Harafu na kipindi cha masika tumia pia
AQUAWET STICKER
 
Habari za weekend wanajamvi.

Wakuu naombeni ushauri wa mbegu bora ya nyanya ya kisasa inayostahimili wakati wa masika na bei yake. Naomba kuzijua mbegu zinazozaa vizuri wakati huo na zinazovumilia magonjwa.
Natumaini kuwa nitasaidiwa.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
Mkuu panda hii mbegu

*MBEGU YA TO 135 F1*
Sifa Kuu
1. Ina matunda Makubwa na Magumu.
2. Inazaa Sana....Hadi kg 10 kwa mmea mmoja ikitunzwa vizuri
3. Inastahimili ugonjwa wa mnyauko wa Bacteria (Bacterial Wilt resistance)
4. Inastahimili ungojwa wa virus usababishwao na inzi weupe....pia hujulikana Kama Rasta au Kitaalamu unaitwa Tomato Yellow Leaf Curl Virus-TYLCV
5. Inastahimili ugonjwa wa mnyauko mcheleo....Late Blight.....
Na Bei yake ni Nafuu Sana. Kwa Mkulima gramu 10 ni TZS 60,000. Ekari moja inatakiwa Gram 50.
IMG_20191116_113816.jpeg
IMG-20191124-WA0005.jpeg
IMG-20191203-WA0027.jpeg
IMG-20191204-WA0003.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu panda hii mbegu

*MBEGU YA TO 135 F1*
Sifa Kuu
1. Ina matunda Makubwa na Magumu.
2. Inazaa Sana....Hadi kg 10 kwa mmea mmoja ikitunzwa vizuri
3. Inastahimili ugonjwa wa mnyauko wa Bacteria (Bacterial Wilt resistance)
4. Inastahimili ungojwa wa virus usababishwao na inzi weupe....pia hujulikana Kama Rasta au Kitaalamu unaitwa Tomato Yellow Leaf Curl Virus-TYLCV
5. Inastahimili ugonjwa wa mnyauko mcheleo....Late Blight.....
Na Bei yake ni Nafuu Sana. Kwa Mkulima gramu 10 ni TZS 60,000. Ekari moja inatakiwa Gram 50.View attachment 1289660View attachment 1289663View attachment 1289665View attachment 1289666

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante sana mkuu na hongera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom