From Sir With Love
JF-Expert Member
- Sep 13, 2010
- 2,076
- 3,797
A2G, tunashukuru kwa taarifa. Japo mkali kama umelima mitiki lakini faida yake bado hujaiona.Haya mnataka bei za mtiki ni hizi hapa
Kuhusu soko: Nenda Turiani morogoro kuna Viwanda vitano vinauza nje hii miti. Pia nilisikia kilombero kipo kimoja
Nenda pia NMB wanakupa mkopo mzuri ukiwa na shamba la miti.
Ukitaka kuamini zaidi tembele wakala wa miti ofis zao zipo Morogoro njia ya kwenda Dodoma , nenda wakakupe ushuhuda.
Taarifa mnazo sasa kimbieni shamba
NB: mitiki inaweza kuuzwa ukiwa na miaka 8, kwahiyo ondoeni fikira za kwamba watafaidi watoto.
A2G, tunashukuru kwa taarifa. Japo mkali kama umelima mitiki lakini faida yake bado hujaiona.
Uliyosema ni yetu kuchunguza na kutafiti.
A2G, asante kwa taarifa zaidi.Mimi sijapansa ila Nipo kwenye maandalizi ya kupanda. Concern zenu zipo sahihi kuna stori nyingi kuhusu mitiki ambazo hazipo verified Ila Mimi stori zangu nilizo wapa nina uhakika nazo sababu kabla sijafanya maamuzi ya kupanda nilizunguka kwa watu walionayo.
Ukitaka kujua thamani ya mtiki nenda Turiani Morogoro, ukifika muulize dereva bodaboda yoyote hivi mitiki inalipa? Halafu ujue hapa uniambie. ndio utajua kuwa mjini watu tunapoteza muda.
A2G, asante kwa taarifa zaidi.
Jamaa yangu niliyemwelezea ambaye amelima mitiki, aliniambia faida kubwa ya mitiki aliyopanda ni kuhifadhi ardhi. Alisema in case serikali imeamua kuchukua ardhi yake kwa vyovyote vile, faida yake ni mitiki aliyopanda kama fidia.
Asante A2G.
Sawa A2G, nitamwambia japo amepanda miti yake kibitiMpe pole na hongera sababu alikuwa hajui kuwa anapanda dhahabu bila kujua thamani. Huyo Jamaa ni tajiri mtarajiwa, kaa naye karibu.
Mwambie thamani ya mtiki ni kubwa kuliko hizo fikira zake
Nipo hapa kuwajibu wadau Kaina na From Sir With Love kuhusu kubeza upandaji wa mitiki na uhalisia wa thamani ya hii miti kwa sasa na baadae.
Binafsi ni mdau katika upandaji wa miti, nishanufaika nayo na ntaendelea kupanda kadri nafasi inapo ruhusu.
Upandaji wa miti ni utajiri na ni uwekezaji wa uhakika.
Licha ya kuipanda mitiki, najihusisha pia na uchakataji wa mbao na magogo ya mitiki kutoka kwa watu binafsi.
Huku Turiani mtaani tunanunua mti wa mtiki wenye miaka7-9wenye round kuanzia cm80-120(katikati ya mti) na urefu wa ft16-18,kwa sh30000.
Ukipeleka kiwandani miti ya ukubwa huu yenye kutoa magogo mawili ya ft8 kila mmoja, ikiwa mitano wanagrade kama cbm1 ambayo thamani yake ni sh400,000/=
Kwenye ekari1 ya mitiki kuna miti640.
Hivyo kama uta opt kuuza mitiki yako ya umri huu kiwandani utapata 640/5*400,000=51,200,000
Hii ni pesa ambayo angepata leo hii mtu aliyepanda ekari moja ya mitiki miaka7 iliyopita.
Kwenye ununuaji wa mitiki, kinacho angaliwa na outer round sio kukomaa kwa mti.
Mkuu A2G taarifa ulizo nazo si sahihi.
Required spacing ya upandaji mitiki ni 2.5m*2.5m. Ekari moja ina sqm4000, hii inamaanisha kwamba content ya ekari moja ni miti 640.
Na hii idadi utatakiwa kuipunguza(thinning) kadri umri na unene wa miti utakavyo kuwa unaongezeka.
Pia haishauriwi kuchanganya mitiki na alizeti kwenye eneo moja. Mimea yote hii ni heavy feeder, inatumia maji mengi sana na mbaya zaidi alizeti inapandwa mwishoni mwa msimu wa mvua wakati huo tayari mitiki itakuwa imepandwa, kitakacho tokea ni scrumble ya chakula na kwakua mtiki una tabia ya kufyonza na kuhifadhi maji mengi, matokeo yake atakae umia hapo ni mtiki make maji yote aliyojikusanyia kujihami na kiangazi, yatatumiwa na alizeti ambaye life span yake ni fupi.
Katika mnyukano huo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mavuno mabovu kwenye alizeti na pia ukaishia kuathiri mitiki make yenyewe itaendelea kuishi mpaka msimu mwingine wa kilimo.
Unaweza kuchanganya na mahindi sio mbaya sana japo mimi siafiki hilo kwa usalama wa miti kwenye palizi.
Nimeona kazi nzuri mkuu, hongera sana kwa uthubutu na utendaji wako kwenye uwekezaji huu!
Nina shida na mbegu za mitiki,tafadhali tuwasilianeMkuu mbegu ninazo mimi. Weka oda yako nikuandalie mzigo ambao utaupata kwa haraka na wepesi kulingana na shehena utakayo.
Karibu sana mkuu!
Miche 500 inaweza kucover ekari ngapi???Kama unahitaji miche wasiliana nasi sasa.
Gharama za miche ni shilingi 400@
Tunapatikana Boko -Timiza Kibaha.
Usafiri ni bure hadi mkoa husika ukichukua kuanzia miche 500.
Call/text/WhatsApp
0766006128
0655715184
0783579456
Sent using Jamii Forums mobile app