Mkuu,
issue ya nyani inasumbua hata siku za mwanzo utakapootesha miti. Inabidi ulinde mwanzoni ili hawa binamu zetu wasing`oe miche na kuitupa. Hii ni tahadhari.
Tuje kwenye hoja. Ni wazo zuri, pili umesema vema kuangalia mti ambao hautachakaza ardhi yako kama mlingoti, huu mlingoti usioteshe kama una mpango wa kuja kulima tena hilo shamba.
Sijui ni pwani ya wapi, ila jaribu kuotesha mwarobaini (utavuna haraka kama mbao), mlonge (utavuna kama dawa ukipata soko au chakula cha mifugo), acrocarpus (fast growing, utavuna kama mbao), mianzi (ujenzi na mapambo),mitiki (utavuna kama nguzo na mbao), meria azarachy(fast growing, kwa mbao nyeupe), miembe (matunda na mbao), mikorosho(korosho na mkaa). Mivinje /mitiki ni long term investment.
karibu tena.