charles passian
Member
- Jan 12, 2014
- 10
- 1
Anayejua gharama za ulimaji mpaka uvunaji
Shamba lako lipo wapi. Gharama zinatofautiana kutokana na eneo ulipo. Nitakupa gharama ninazofahamu mimi kwa mahali nilipo.
1: Natumaini shamba unalo. Kama huna basi ekari moja ni 350k.
2: Kusafisha ekari moja, yaani kung'oa visiki, kukusanya na kuchoma moto uchafu wote ni 200k
3: Kulima kwa trekta (kukatua) kwa shamba jipya bei ni kuanzia 55k mpaka 65k. Si lazima lakini kama utapanda miti pekee.
4: Gharama za kuchimba mashimo na kuotesha miche kwa eka moja si chini ya laki 1 kutegemeana na makubaliano kati yako na kibarua lakini.
5: Mche mmoja unaanzia sh 300 hadi 500. Kutegemea na mazingira
6: Usafiri wa kuleta miche shambani andaa kitu kama elf 30 na kuendelea kitegemea na umbali lakini inaweza kuzidi hapo au kupungua
7: Kwa mwaka utapalilia mara 2 sawa na sh 80k zidisha mara 8 hadi 10. Baada ya muda huo nyasi zitakua ni chache sana maana miti itakua na ukubwa wa kutosha kutengeneza kivuli kingi na kusababisha kuzuia mimea mingine isikue
8: Utahitaji kila mwaka kukata matawi ya pembeni na kuacha moja linaloenda juu ili mti ukue haraka na unenepe pia. Gharama inaweza kuanzia 20k(makubaliano na kibarua). Lazima uwe na kifaa maalum cha kupunguzia matawi ili kuzuia mti kupata vidonda kwa ukataji mbaya wa matawi
9: Kuvuna ni kuanzia miaka 20 ili kupata faida kubwa zaidi. Chini ya hapo utavuna miti ambayo haina unene wa kutosha kutoa mbao. Unaweza kuvuna wewe mwenyewe au ukauza ikiwa shambani.
ANGALIZO
Kilimo cha mitiki ni uwekezaji wa muda mrefu sana. Usitegemee faida baada ya miaka 3. Hiyo ni ulinzi wako wa baadae. Thamani ya mbao haijawahi kushuka tangu mbao zimeanza kuzalishwa so tegemea faida nzuri tu baada ya muda mrefu lakini. Nakutakia kilimo chema. Nimekuwekea picha ya mitiki niliyopanda 2012.
View attachment 1233988