Kilimo cha mchicha


donata fredy

donata fredy

Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
45
Likes
81
Points
25
Age
26
donata fredy

donata fredy

Member
Joined Jul 22, 2016
45 81 25
Morning rafk zangu.habari ya jumapili. Leo naomba niingie kwenye kilimo cha mchicha na faida zake.

Mchicha ni mojawapo ya mboga za asili ambayo hulimwa katika mikoa yote hapa nchini. Mboga hii ina vitamin A, C, na madini aina ya chokaa na chuma kwa wingi Majani ya mchicha huliwa baada ya kupikwa au kutengenezwa supu.

Mbegu zake zinaweza kusagwa na kupata unga unaoweza kutumika katika mapishi mbalimbali kama vile kutengeneza ugali, uji, chapati na maandazi.

MAZINGIRA
Mchicha unaweza kulimwa karibu katika aina yeyote ya hali ya hewa na kwenye udongo wa aina yeyote ili mradi usituamishe maji.
Udongo wenye rutuba nyingi unafaa zaidi kwa ustawishaji wa zao hili.

AINA
Kuna aina nyingi za mchicha; zifuatazo ni aina zinazostawi hapa nchini:-
Mchicha Mweupe Aina hii ina majani marefu yenye rangi ya kijani ya kupauka. Huvunwa kwa kung’oa na huuzwa sana sokoni.

Mchicha Mpana
Ni ule ambao ni mnene na una majani mapana na yenye rangi ya kijani kibichi. Huweza kuvunwa kwa kurudiwarudiwa
Mchicha Mwembamba
Huu ni mdogomdogo na unaota shambani kama gugu. Majani yake ni madogo na huchanua mapema.

Mchicha wa Unga
Mchicha huu huwa mwekundu unapokuwa mdogo na hukua haraka. Hutoa mbegu nyingi ambazo zinaweza kusagwa unga, ambao unaweza kutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile, uji na maandazi. Majani yake hupikwa kama mboga au hutengenezwa supu.

HATUA ZA KUANZISHA KILIMO.

KUTAYARISHA SHAMBA
Tayarisha shamba mwezi mmoja kabla ya kupanda. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri ili kuongeza rutuba ya udongo. Mbolea hizi pia hufanya udongo ushikamane vizuri na kuhifadhi unyevu kwa muda mrefu. Weka kiasi cha ndoo moja yenye ujazo wa lita ishirini katika eneo la mita mraba mmoja. Changanya vizuri mbolea hii na udongo.

Wiki mbili kabla ya kupanda laininsha udongo na sawazisha udongo.

KUPANDA
Kuna njia kuu mbili za kupanda mchicha, Kupanda mchicha moja kwa moja shambani na kuotesha miche kwanza kwenye kitalu. Kupanda Moja kwa Moja Shambani Mbegu hupandwa moja kwa moja kwenye shamba la kudumu na baadaye mimea hupunguzwa na inayobaki huachwa katika nafasi ya sentimita 15 hadi 23. Mbegu huweza kupandwa katika sesa au matuta.

Kiasi cha kilo moja hadi mbili za mbegu kinatosha kuotesha katika eneo la hekta moja. Ili kuepuka mlundikano wa mbegu sehemu mmoja, changanya mbegu na mchanga kwa kiasi kinacholingana kabla ya kumwaga shambani. Kisha mwaga na funika kwa kiasi kidogo cha udongo au mbolea laini za asili. Tandaza nyasi kavu na mwagilia maji.

Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na jioni hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku tatu mpaka tano na baada ya kuota ondoanyasi. Kuotesha Miche Kwenye Kitalu Kutayarisha Kitalu: Sehemu itakayooteshwa mbegu inatakiwa iwe laini na yenye rutuba ya kutosha. Hivyo baada ya kulima lainisha udongo kwa kupigapiga mabonge makubwa.

Kisha tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na urefu wowote. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha debe moja au mbili katika kila eneo la mita mraba moja. Changanya mbolea hii na udongo vizuri, kisha sia mbegu zilizochanganywa na mchanga kwenye mistari yenye nafasi ya sentimita 10 hadi 15.

Baada ya kusia, funika mbegu kwa kiasi kidogo cha udongo au mbolea laini za asili. Weka matandazo na mwagilia maji. Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota. Baada ya siku 4 mpaka 6 ondoa matandazo na endelea kumwagilia maji.
( nawatakieni jumapili njema wakubwa zangu. )
 
ndege JOHN

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2016
Messages
6,080
Likes
9,500
Points
280
ndege JOHN

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2016
6,080 9,500 280
Siamini Kama maada Kama hizi zinakosaga WACHANGIAJI kabisa
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
32,823
Likes
97,996
Points
280
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
32,823 97,996 280
Mchicha jina lingnine huitwa amaranth na unga wa mbegu zake ni low in calories kwa wale wanaojali afya zao
 
Southern Highland

Southern Highland

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Messages
4,179
Likes
5,477
Points
280
Southern Highland

Southern Highland

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2017
4,179 5,477 280
Ngoja na mimi nichangie

Mchicha ni mzuri kwa afya.
 
tinkanyarwele

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Messages
1,183
Likes
960
Points
280
Age
47
tinkanyarwele

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2016
1,183 960 280
Shukrani sana
 

Forum statistics

Threads 1,273,286
Members 490,351
Posts 30,477,038