ST farms agribusiness

ST farms agribusiness

Mhina Martin

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Posts
217
Reaction score
263
KILIMO CHA TIKITI MAJI TANGA KOROGWE . 0716898393
St farms ilianza na maandazi ya shamba kama inavyoonekana.

baada ya kumaliza kulima tulianza mchakato wa kutengeza mifereji na matuta au majaruba kwa vipimo tuta hadi tuta umbali wa mita mbili mpishano wa mifereji ya kupitisha maji ni mita moja.

baada kumaliza kuchora majaruba shambani tulianza na zoezi la kuchimba mashimo kwa vipimo shimo hadi shimo mita moja na nusu.

baada ya zoezi la mashimo kuisha St farms tuliandaa mbolea ya samadi ya mavi ya ng'ombe na mbuzi ya kutosha so samadi hyo ilichanganywa na kuwekwa kila shimo shamba zima.

baada ya zoezi la mbolea kuisha tulinywesha shamba zima maji kwenye mashimo ili kuwe na unyevu mzuri ili kurahisisha mbegu ikipandwa iote bila kukwama na kwenye mifereji kuona uwezo wake wa kupitisha maji wakati wa kunyweshea ili kurekebisha kwenye changamoto.

baada zoezi la kumwagilia maji siku inayofuata ni upandaji ambapo St farms tulichagua mbegu aina ya SUKARI F1 500gram inapanda ekari moja na robo kila shimo tuliweka mbegu mbili mbili kwa kuwa kulikuwa na unyevu na tulifukia kwa mchanga mwepesi bila kukandamiza mbegu baada ya siku ya nne zote zimechomoza vizuri naendelea .

Tafadhali Naomba like,share na follow kwa kupata ujuzi,masoko , taarifa na dondoo za uhakika kutoka shambani ST FARMS
View: https://www.instagram.com/p/DfzlI_uoMTM/?dlrf=MXRyMXB3cDExd2U0eg==
 

Attachments

  • file_000000001ef08208b66ce97f72bd58c1.png
    file_000000001ef08208b66ce97f72bd58c1.png
    2.1 MB · Views: 5
  • FB_IMG_1794369194032.jpg
    FB_IMG_1794369194032.jpg
    520.1 KB · Views: 5
  • IMG_20260926_101748.jpg
    IMG_20260926_101748.jpg
    834 KB · Views: 4
  • IMG_20260806_140314.jpg
    IMG_20260806_140314.jpg
    1.1 MB · Views: 4
Follow
 
Kwa kilimo ninavyokijua hapo ni asilimia 0.01 ya matokeo, kuna zoezi gumu la post harvest management. Unaweza kuvuna vizuri ila matikiti yakaenda kuozea sokoni
 
St farms tulifanikiwa kupanda na ilipofika siku ya nne zikachomoza vizuri nasi tukawa tumeandaa dawa ya wadudu wanaokata aina ya dudukiller pamoja na busta aina ya fastgrow tulipuliza shamba zima ili kuweka mmea salama.

Baada ya hapo tukanza ratiba ya kunyweshea Maji kila baada ya siku tano mpaka saba kulingana na unyevu uliopo shambani.

St farms tuliendelea na ratiba za kupuliza busta ya fast grow mix na dawa ya wadudu au fast grow mix dawa ya ukungu kila baada ya wiki.

Tikiti ilipotimiza siku ya 32 maua yalianza kuonekana tukachana kabisa kupuliza busta ya fasta grow pamoja na dawa za wadudu maana tunaelekea kwenye kipindi ambacho wadudu tunawahitaji kwa ajili ya uchavushaji na pia hatuhitaji majani mengi kwenye mmea.

Hivyo mbadala tukapuliza busta ya kuongeza vichocheo vya homoni ya maua na kulinda matunda inayoitwa PLANT ONE hii tulipuliza mara moja na siku ukipuliza unapuliza asubuhi Sana au jion na mmea lazima usizi siku ya pili unaweza ukachanganyingikiwa ila baada ya siku mbili inaamka kwa nguvu kubwa yenye ubora maua ya kutosha mpaka unashanga.

Siku ya 38 st farms tuliweka mbolea mfuko mmoja tu ilitosha kwa kuwa shamba letu bado bikra tulitumia aina CAN kwa ajili ya kujenga tunda lenye muonekano mzuri,tunda gumu na tunda kubwa angalau tupate tunda lenye 9Kg mpaka 16Kg.
IMG_20261028_175104.jpg
IMG_20261012_174630.jpg
 
Kwa kilimo ninavyokijua hapo ni asilimia 0.01 ya matokeo, kuna zoezi gumu la post harvest management. Unaweza kuvuna vizuri ila matikiti yakaenda kuozea sokoni
Kilimo cha sasa si cha kizaman unalima hujui soko slogani ya kilimo cha kisasa ANZIA SOKONI nenda shamba karibu St Farms
 
Back
Top Bottom