Kilimo bora cha Mananasi: Uandaaji wa shamba, upandaji, utunzaji wa mimea na uvunaji wa mananasi

Wakulima wenzangu,ngoja nikili kuwa nililima kilimo cha kiswahili sana. Sikufanya utafiti wa soko kabla ya kulima, nililima tu kwakuwa nina ardhi na sikutaki ardhi ikae bure. Sasa natarajia kuvuna nanasi zaidi ya 200, 000 mwaka huu kuanzia Nov. Nahitaji yeyote anayefahamu soko la uhakika la nanasi na kama kuna mteja mkubwa tunayeweza kukubaliana katika reasonable price tuingie makubaliano. Bei ya viwandani siitaki kwakuwa ni dhuluma kubwa sana kwa mkulima.
 

Umelima wapi?
 
Kwa anayehitaji kupata ELIMU YA UZALISHAJI WA NANASI (general Knowlegde) mzigo huu hapa kwa kiswahili:

Utangulizi
Nanasi ni tunda la kitropiki, linapendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma. Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.

Hali ya hewa inayofaa kwa ukuaji wa nanasi
Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.

Udongo unaofaa kwa kilimo cha nanasi
Kwa kilimo cha nanasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga usiotuamisha maji. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.

Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa (flat-bed) au kwa matuta (furrows).

Kwa sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka mbolea kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya kuku, weka pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.

Upandaji wa mananasi
Zipo aina mbali mbali za ‘mbegu’ (machipukizi/maotea) lakini yale yanayochipua kutoka ardhini hufaa zaidi na hukomaa mapema. Chagua machipukizi mazuri yenye umri mdogo na yenye kulingana kwa ukubwa. Iweke miche kwenye kivuli kwa siku 3 kabla ya kuipandikiza iweze kutoa mizizi haraka. Pandikiza mwanzoni mwa mvua za masika. Nafasi iwe sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya mistari miwili. Pandikiza miche 50,000 katika hekta moja. Chovya miche kwenye dawa ya Diazinon au Fention kwa muda wa dakika 25 kabla ya kuipandikiza ili kuzuia mashambulizi ya wadudu.

Palizi - Kudhibiti Magugu
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu. Katika kilimo cha nanasi magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Matumizi ya viuagugu hurahisisha zaidi palizi ya nanasi ukizingatia kuwa nanasi huwa na miiba katika ncha za majani yake ambazo huchubua ngozi endapo palizi za jembe zitatumika. Njia nyingine ni matumizi ya matandazo (mulch) ya majani au plastiki (plastic mulch) maalum kuzuia magugu.


Shamba la mananasi

Mahitaji ya mbolea ya mananasi
Weka mbolea ya NPK gramu 50 hadi 70 kwa kila mche wakati wa kupanda. Weka tena gramu 85 kwa kila mche baada ya miezi 3 na pia miezi 3 baadae.

Wadudu na Magonjwa yanayosumbua minanasi
Nanasi ni zao lisilosumbuliwa na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hii ni faida kubwa sna kwa wakulima wa nanasi! Hivyo endapo patatokea mashambulizi ya wadudu na magonjwa, ushauri zaidi wa kitaalam utafutwe kukabiliana na tatizo husika. Hakikisha unakagua shamba ili kuzuia wadudu kama wataonekana.

Uvunaji wa mananasi
Nanasi huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana na aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya kutoa maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva. Katika kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti tofauti itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa sababu hiyo ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye umri na ukubwa sawa.
Kwa wanaofanya kilimo cha nanasi kibiashara (commercial pinapples production) hutumia kemikali aina ya Ethrel (@ 100 ppm) mwezi mmoja kabla ya kuanza kutoa maua ili mimea mingi iweze kutoa maua kwa wakaii mmoja, angalau 80% ya mimea yote. Vuna wakati kikonyo cha nanasi kimebadilika rangi kuwa njano ya dhahabu. Kata kikonyo cha nanasi chenye urefu wa sm. 30 kikiwa kimeshikana na nanasi na upunguzie majani ya kichungi chake.

Utunzaji wa mananasi
Hifadhi nanasi katika eneo lenye ubaridi huku kikonyo chake kikielekea juu. Hakikisha unauza nanasi mara tu au siku 2 hadi 3 baada ya kuvuna ili kutunza ubora wake.


Mananasi yaliyovunwa

Source: JInsi ya kufanya Kilimo cha Nanasi | Mogriculture Tz
 
bachelor sugu, njoo huku kumenoga!
 
Asante kwa somo murua
 
Habari wadau,

Naomba ufahamu kidogo kwa wenye utaalamu na zao la pineapple/Nanasi

1. Je kuna mbegu za kisasa (hybrid) za zao hili? Kama ndio zina sifa gani? Nkimaanisha uzaaji wake, umri na sifa zingine

2. Katika maisha ya nanasi, naweza kuvuna kwa muda gani/mara ngapi kutoka katika mche mmoja au nkitoa tunda moja tu basi napanda mbegu ingine?

3. Je zinauzwa mbegu za nanasi madukani au lazima nkanunue miche kwa wataalam wa kukuza miche?

4. Wapi naweza pata mbegu/miche ya zao la nanasi na BEI zikoje? Shamba liko Vianzi

Asante
 

NIMEITOA MAHALI

Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua:

Tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi.

gharama zitakuwa hivi:


  • ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
  • utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
  • gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
  • Mbolea 100,000.
  • matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
  • jumla 1,500,000/-


Mapato
nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)

Faida :
Ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..

Soko likoje
Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-
 
Njopekafarm tunayo miche ya nanasi ya kutosha lakini pia tunayo miche ya matunda kama passion ,malimao ,mindimu,mastafeli,michungwa,mipapai,mifenesi,piga simu au whatsapp +255625977427
 
Njopekafarm tupo mkuranga pwani wauzaji wa mbegu za minanasi lakini pia ni watalaamu wa kuandaa shamba tunakupandia ,tunakupa muongozo wa kuhudumia shamba la minanasi mpaka uvune pia simu au whasapp +255625977427
 
Njopekafarm wauzaji wa miche ya nanasi pia miche ya migomba aina zote fia 24 ,mzuzu,ngego kapale,mkono wa tembo,mtwike,malindi,n.k.pia tunayo miche mipapai,mistafeli,mifenesi,passion,miparachichi,piga simu +255625977427
 
Njopekafarm tupo mkuranga kwa mahitaji ya mbegu na upandaji na muongozo wa shamba na huduma piga simu au whatsapp +255625977427
 
Kwa ekari moja kwa hesabu za hapo juu inaonyesha unaweza kupata sio chini ya 5M ukiwa na ekari 10 unapata 50M
Duuuuu,sidhani kama hizi hesabu zipo realistic but all in all nisikukatishe tamaa just try but I'm sure kinalipa tu hicho kilimo

1: Ekali moja miche 16,000 hadi 20,000. Unapopanda mengi zaidi ukubwa wa nanasi unapungua. Faida ya kupanda mengi kwa sababu yatashikana mpalio sio mara nyingi.

2: Toka mpando hadi mvuno wa kwanza ni miezi 18.

3: Gharama kubwa ni Shamba, mbegu na mpalio pamoja na mbolea.

4: Soko sio tatizo kubwa wanunuzi wanafuata shambani. Hii ni kwa eneo la Kiwangwa sina hakika kwingineko.
 
Njopekafarm tupo mkuranga pwani wauzaji wa mbegu za nanasi na migomba simu 0625977427 bei shilingi mia moja nyoote mnakalibishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…