KILIMANJARO: Wahamiaji haramu 74 kutoka Ethiopia warudishwa makwao

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Taasisi ya kimataifa ya uhamiaji(IOM), inayojihusisha na usimamizi wa taratibu za haki za binadamu dhidi ya wahamiaji, imewarejesha makwao Waethiopia 74 waliokuwa wakishikiliwa nchini Tanzania baada ya kuingia kinyume cha sheria.

Wahamiaji hao waliondoka nchini kwa ndege ya shirika la Ethiopia Airlines kuelekea nchini mwao, wakitokea katiak gereza kuu la Karanga Mjini Moshi ambako walikuwa wamehifadhiwa.

Wahamiaji hao wamelazimika kurejeshwa makwao, baada ya Serikali ya Tanzania kuridhia makubaliano yaliyofanywa kati yake na IOM.

Safari ya kuwarudisha makwao imegharimu dola za Marekani 35,000 sawa na shilingi milioni 70 za kitanzania.
 
Back
Top Bottom