Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,874
Tangu mwanzo niliwahi sema na ninarudia kusema kwa kuishauri serikali, wahamiaji haramu hasa kutoka nchi mbalimbali na wengine hawa kutoka Ethiopia na Somalia wamejaa katika Magereza yetu.
Nilipokuwa Mahabusu Gereza la Iringa 2018 April, kulikuwepo na Wahamiaji wengi kutoka Somalia, wengine kama wafungwa wengine kama mahabusu .
Wengi walikamatwa wakiwa wanapita Tanzania ili waende nchi zingine na wengine walikamatwa wakiingia kinyemela Tanzania , ila mimi nimekuwa na fikra tofauti katika hili siku zote.
Sijawahi ona sababu ya kuwafungulia kesi na kuwaweka Gerezani kama mahabusu sababu hawa hawana ndugu hivyo Serikali kupitia DPP inapowafungulia kesi hawawezi kupewa dhamana hivyo wanakuwa kama mahabusu na kuwekwa Getezani.
Watakula bure na kuongeza gharama na msongamano katika magereza yetu , niliyo wakuta mahabusu Iringa walikuwa na miezi 8 kesi yao haijaisha , hivyo wanakula bure hadi kesi yao itakapoamuliwa na wakiamuliwa kufungwa watafungwa labda miaka 2 au 3 hivyo kuongeza gharama na msongamano Magereza.
Kuwafungulia mashtaka na kuwafunga haijawahi kusaidia hawa wahamiaji kusita kuingia nchini kinyume na sheria kwa kuogopa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Ushauri wangu , hawa Raia hasa kutoka somalia na Ethiopia ni wengi sana katika Magereza yetu wengi wakiwa mahabusu na wengine wafungwa na makosa yao ni aina moja .
Ushauri kwa serikali @tanzaniagovernment ,@wizaramnn , @katibanasheria_
na Mh. @samia_suluhu_hassan ili kukabiliana na msongamano na kupunguza gharama katika Magereza yetu .
1.Kesi za hawa wahamiaji hasa wa Somalia na Ethiopi ambao ni wengi na sasa ni Mahabusu zifutwe tuu ili warejeshwe kwao .
2.Kuna haja ya msamaha wa Rais ili wahamiaji wote ambao ni hao waethiopia ,somalia hata wengine wafutiwe kesi ili warejeshwe kwao kupitia Balozi zao .
3.Njia zingine za ziada zitumike kukabiliana na hawa wahamiaji na kuzuia kuingia nchini , ili kupunguza tatizo hilo .
Ila njia ya kuwafungulia mashtaka na kuwaweka ndani sioni kama ni dawa zaidi naona huongeza gharama na msongamano katika Magereza yetu.
Ahsante.